Ushauri kwa vyama vya upinzani juu ya vyombo vya habari

jo mose

JF-Expert Member
Aug 5, 2020
3,477
4,072
Kutokana na figisu figisu na yanayoendelea na yanayotegemewa kutokea kuhusu wapinzani kunyimwa airtime kwa maagizo toka juu ili wananchi wasipate kusikia sera za upinzani baada ya wao kutamba miaka 5 pekee yao wakiongelea vitu vilivozoeleka kwa wananchi huku wakiwa hawana kipya cha kuwaeleza wananchi, kipya zaidi ya kurudia rudia maneno kama mabeberu, SGR, ndege, Stiglers, flyover ambavyo wananchi awali awashibi vitu hivyo.

Mfano huwezi ukawambia watu wa Kasulu au Chunya eti nimenunua ndege, nimejenga flyover wakakuelewa.

Wapinzani waongee na vyombo vya habari binafsi vya nchi jirani ambavyo vinapatikana kwenye decoder zetu zote ili wawarushie matangazo yao kupitia live au recorded na kutuma kwenye vyombo hivyo nje pasipo lazima vyombo hivyo kuja nchini, then kupitia decoda watapata kuona na kusikia kampeni za wapinzani nao watazirekodi na kurushiana kupitia Bluetooth, CD, flash nk.
 
Kasheshe ni kuwa wangapi tuna simu janja nchi hii?

Wenye simu janja wanaishi na watu, hivyo watawapa elimu wasio na hizo simu. Mfano mimi binafsi huwa nawapa watu wasiopungua kumi habari hizi, na elimu ya uraia juu.
 
Back
Top Bottom