Ushauri kwa serikali

Ushauri kwa serikali

Kaka hakuna Mkataba usiokuwa na kipengele cha kuvunja Mkataba.

Kila Mkataba lazima HICHO kipengele kiwepo, Mbona enzi za JPM wale Barrick walibanwa mpaka wakakubali kulipa fidia ya mamilioni ya Dola na Mkataba mpya ukaandaliwa na Sasa hivi Tanzania tuna hisa ya 16% kwa Barrick na tuna watu wetu ndani ya Barrick KUSIMAMIA hilo.

Na hiyo 16% ni ya kuanzia lakini Kila baada ya miaka 5 inaongezeka hiyo asilimia kwa asilimia 3% hadi 10% kadri Hali itakavyokuwa inaruhusu na bado Barrick walidhia hilo.

Ni kichaa pekee ndiye atashindwa KUSIMAMIA RASIMALI za nchi ili ziwanufaishe wananchi na kuondokana na umasikini tulionao na kupunguza ugumu wa maisha badala ya kukimbilia tozo.

Kwa kifupi Tozo yeyote itakayowekwa na Serikali itaongeza ugumu wa Maisha kwa Mwananchi masikini wa Tanzania.

Tafuta Blueprint document iliandaliwa enzi za JPM iliangazia sekta zote za uchumi na utitiri wa Kodi, ushuru, Tozo, n.k. ulikuwepo na ilivyomshauri JPM kuondoa hizo Tozo na Kodi zilizokuwepo enzi hizo JPM akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara nchini
Mkuu umeongea vizuri sana hasa ulipo gusia mambo ya mikataba maana hapo ndio sehemu tunapo anzia kupigwa.

Je viongozi wakuu hawaoni namna ambavo wanaweza kurekebisha hii mikataba ili inufaishe watanganyika wote.

Tubadili ushauri kwamba selikali iuze mlima Kilimanjaro pesa itakayo patikana watu watibiwe bure
 
Sijalipwa na yeyote mimi ni job less hapa yenyewe nimeweka bando la jero 245mb na VPN inavopeleka moto sizani kama saa Tisa mbs zitatoboa. Nirudi kwako mbona matusi mkuu
Hakuna jobless mwenye akili zimevimba km busha. Kwa rasimali na mikopo iliyokopwa kwanini usiseme ielekezwe huko kwenye huduma za afya mpaka useme wananchi wabebeshwe zigo la ongezeko la kodi ilihali tayari wana mateso ya kodi zinazowaneemesha watawala.!! Pumbavu
 
Ziliongezea tozo
Kodi za majengo zimekua well implemented
Cha ajabu zinanunulia bugatti
Hapo ndo roho inaanza kuuma. Yaani Kodi na tozo watu wanazolipa wananunua bugati aisee aijakaa sawaa
 
Waweke bima za bei ndogo hata mtu alipe laki 1 kwa mwaka atibiwe yeye na familia yake kwa mwaka
Kwa maskini ukitaja laki lazima akushangae sana!

Bima zote washafirisi, kikubwa ni kubuni vyanzo ili wananchi watibiwe bure.

Mbona Nyerere na Mwinyi snr hatukusikia ada za shule ama kulipia matibabu, wao waliwezaje?
 
Hakuna jobless mwenye akili zimevimba km busha. Kwa rasimali na mikopo iliyokopwa kwanini usiseme ielekezwe huko kwenye huduma za afya mpaka useme wananchi wabebeshwe zigo la ongezeko la kodi ilihali tayari wana mateso ya kodi zinazowaneemesha watawala.!! Pumbavu
Mkuu ni wazi kwamba hatuna uwezo wa ku utilize rasilimali kuwa na dhamani bila ya kutegemea watu kutoka nje.

Vilevile pesa zamikopo wamesha nunua ma rozi loisi na kujenga majumba ya kifahari kwa wao na familia zao.

Nasikitika kusema akili zako zimevimba kama busha la mbwa kwa maana huna hata mawazo mbadala
 
Kwa maskini ukitaja laki lazima akushangae sana!

Bima zote washafirisi, kikubwa ni kubuni vyanzo ili wananchi watibiwe bure.

Mbona Nyerere na Mwinyi snr hatukusikia ada za shule ama kulipia matibabu, wao waliwezaje?
Waliweza kwasababu idadi ya watu ilikuwa chache sana kipindi hiko
 
Kiongozi pekee aliyehakikisha muwekazaji haji TANZANIA kuibia nchi alikuwa JPM tu bahati mbaya hatunaye ameshafariki hadi atokee mwingine itachukua muda
 
Kiongozi pekee aliyehakikisha muwekazaji haji TANZANIA kuibia nchi alikuwa JPM tu bahati mbaya hatunaye ameshafariki hadi atokee mwingine itachukua muda
Mungu ni mwema tutapata mwingine mzuri zaidi yake.
 
Kuhakikisha kila mtu analipa kodi mtu yoyote mwenye Nida awe na acc inayotrack ulipaji wake wa kodi ili imsaidie balance yake ktk kupata huduma zingine za kigavoo, yani ukinunua kitu ata vocha ile kodi inayokatwa ijulikane imetoka kwako kwaoyo jukumu la kulipa kodi ulisimamie binafsi ili balance yako isome vuemaa target iwe atleast 100k kupata huduma ya afya bure
 
Tukiondoa kiinua mgongo cha milioni 400 kwa kila mbunge, na kupunguza malipo ya wabunge mpaka kima cha wafanyakazi wa kawaida (milioni 1-2). Pesa tutakayookoa inatosha kutoa huduma ya matibabu bure nchi nzima
 
Kwa maskini ukitaja laki lazima akushangae sana!

Bima zote washafirisi, kikubwa ni kubuni vyanzo ili wananchi watibiwe bure.

Mbona Nyerere na Mwinyi snr hatukusikia ada za shule ama kulipia matibabu, wao waliwezaje?
Kutibiwa bure ni ngumu hata hii nchi tukiwapa wazungu
 
Ushauri mzuri ni huu japo najua wakubwa na wabunge hawataupenda
1.Raisi matumizi yake yote chakula,kusomesha wanawe atumie mshahara wake kama Marekani wanavyofanya.
2.Wabunge wote wawe wanakatwa kodi sababu utatungaje sheria ya kodi wewe unajitoa kando
3.Maraisi wastaafu wasilipwe chochote zaidi ya pension yao japo wasinyanganywe ulinzi maana lazima katika kutawala kwao hawatakosa maadui huwezi pendwa na kila mtu hata uwe nabii kumbukeni YESU pamoja na kuleta neno la MUNGU bado walimsulubu
4.Wake wa maraisi wastaafu wasilipwe chochote japo sina uhakika kama hili linafanyika.
5.Magari ya kifahari ya wabunge na mawaziri yawepo lakini yasiwe ya bei kubwa
6.Wabunge nao waingie kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kama PPSF na NSSF

Haya yakifanyika matibabu yanaweza kuwa bure nchi nzima.Na tutakuwa na wabunge ambao kweli wamekwenda bungeni kutetea wananchi sio kutegemea kitu nchi kama Holand ndivyo ilivyo na ndio wanatupa misaada wanatucheka mno.
 
Na pipi, sindano na vingine vidogo vidogo vipande sio... Hivi unafikiri nchi hii ni maskini kiasi hicho? Au umeamua kutungamcha tu.
 
Back
Top Bottom