SoC04 Ushauri kwa Serikali juu ya kuongeza na kuboresha huduma za Ofisi za NIDA

Tanzania Tuitakayo competition threads

SEMBOJE

Member
Aug 31, 2017
6
10
chanzo ni; yotube

Hata sasa kwa Nchi ya Tanzania , Huduma ya upatikanaji wa namba za nida au vitambulisho vya nida bado imekuwa changamoto na mfumo huo kusumbua. Ofisi inayohusika na namba za nida utaikuta ipo wilayani tu au mkoani tu , yaani ofisi hizi za nida zinapatikana katika halmashauri za mji lakini halmashauri za vijijini hazipo wala huwezi ukazipata, Tena utakuta hata hapo wilayani au mkoani ni ofisi moja tu inayohusika na kushughulikia namba hizo za nida.

Ambavyo kutokana na uchache wa ofisi zinazotoa huduma hizo za namba za nida zimepelekea kuwa na foleni ndefu maana wahitaji ni wengi zaidi kuliko watoa huduma, pia wakati Mwingine kutokana na uchache huo wa huduma kunasababisha mhitaji kukosa kabisa namba ya nida au kupelekea mhitaji kujiandikisha zaidi ya mara moja au zaidi ya kituo kimoja baada ya kuona namba ya nida haitoki zaidi ya miezi miwili, na kusababisha kuwa kikwazo kikubwa kwake kwa kuzuia namba kutoka kwani hairuhusiwi kujiandisha zaidi ya kituo kimoja hata kama namba haijatoka zaidi ya mwaka mmoja..

Hata hivyo kutokana na wahitaji kuwa wengi, imepelekea hata wahudumu wa ofisi za nida kuzidiwa na kuacha kabisa kushughulikia baadhi ya fomu ambazo tayari wamezipokea kwa wateja wao, na wamekwisha zishughulikia kwa hatua ya kwanza, wanashindwa kumalizia hatua zinazoendelea kulingana na wingi wa fomu na foleni za watu wapya au wahitaji wapya waliokuja ofisini kufanya mchakato wa kupata namba ya nida kwa mara ya kwanza kabisa.
Angalia picha za foleni katika ofisi za nida
xmass-pic.jpg
nida-pic.jpg
nida-pic-data.jpg
pic-nida.jpg
Picha hizi zote chanzo chake ni; Source; www.mwananchi.go.tz

Kutokana na foleni hizo, zinapelekea baadhi ya wateja au wahitaji kutopata huduma kutokana na mda wa kazi kuisha na kuambiwa warudi tena siku nyingine ambayo watakutana na wahitaji wengine. Hata hivyo wajawazito, wazee na walemavu hushindwa na kuchoka kuvumilia kusubilia wanaamua kukata tamaa na kurudi majumbani kwao.

CHANGAMOTO ZINAZOTOKANA NA MFUMO HUU WA UHABA WA WAHUDUMU AU WAFANYAKAZI WA NIDA NA UHABA WA OFISI ZA NIDA

Changamoto zilizopo katika ofisi za nida na zinazotokea kwa wateja wake wenye uhitaji wa huduma za namba za nida ni kama zifuatao;​
  • Wahudumu au wafanyakazi kushindwa kumdu foleni zilizotamalaki ofisi za nida.​
  • chanzo chake; youtube
  • Mhitaji kutopata ujumbe Kwenye namba ya simu alioombea namba ya nida, unaompa namba yake ya nida baada ya namba ya nida kutoka.​
  • Wananchi kuibiwa pesa zao, wanatoa fedha kwa wahudumu ili wasipage foleni na fomu zao zishughulikiwe mapema na wapate namba za nida mapema. Ambapo wakati mwingine wanatoa pesa lakini hata hivyo ingawa wametoa pesa zao namba za nida hawapati na wanapanga foleni kwa sababu wametoa pesa kwa watu wasio sahihi au wasiohusika.​
  • chanzo chake; youtube
  • kusajiliwa namba zao za simu kwa namba ya nida ya mtu mwingine. Ambavyo ikitokea wametofautiana kidogo na mtu huyo aliemsajilia laini, mwenye namba ya nida anaamua kumfungia laini yake.​
  • Wahitaji kujiandikisha zaidi ya kituo kimoja na kupelekea kuchelewa au kutopata kabisa namba ya nida kutokana na sabau ya kujiandikisha zaidi ya kituo kimoja, kwa maana haieuhusiwi kujiandikisha zaidi ya kituo kimoja.​
  • Wananchi kukata tamaa ya kupata haki yao ya namba ya nida na kupelekea kukosa mahitaji baadhi, au kukosa ajira na kazi mbalimbali, kutokana na kutokuwa na namba ya nida.​
  • Wafanya biashara kushindwa kukata leseni za biashara kwa kukosa namba ya nida au kutokuwa na namba ya nida.​
  • Wanafunzi wa vyuo kushinwa kuomba mkopo na kukata kadi za benki kwa sababu ya kukosa namba ya nida au kutokuwa na namba ya nida.​
  • Kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali kushindwa kuomba ajira na kukosa kazi hata kama wana sifa, kwa sababu ya kutokuwa na namba ya nida.​
  • wahudumu kupoteza fomu za wateja​
NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO HIZO
Napenda kuishauri serikali pamoja na mamlaka husika ya nida ili kupunguza changamoto hizi zilizopo;​
  • Serikali pamoja na mamlaka husika waongoze wafanya kazi au wahudumu wa ofisi za nida ili kumdu foleni za watu.​
  • Serikali pamoja na mamlaka husika waongeze ofisi za nida, japo ofisi za nida ziwepo kwa kila halmashauri za mji na halmashauri za vijijini, ikiwezekana waboreshe na vifaa vya kupiga picha na vya kuwekea vidole viwe vidogo kama vya kusajilia laini, ikiwezana waweke na mawakala wa namba za nida kwa kila kata.​
  • Serikali pamoja na mamlaka husika irudishe tena mfumo wa kutuma ujumbe wa namba ya nida kwenye namba za simu za wananchi walizotumia kuombea namba ya nida, kwa namba ya nida iliyotoka ili mteja kupata wepesi wa kuipata, ili kuepusha pia kwenda kupanga foleni ya kuangalia na kuuliza namba ya nida kama imetoka.​
  • Serikali pamoja na mamlaka husika waweke utaratibu wa wahudumu wa namba za nida kuwafuata wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita ili kuwasajili kwa lengo la kwamba mda wa kuomba mkopo ukifika ukute tayari wananamba za nida.​
FAIDA YA KUTATUA CHANGAMOTO HIZI

Serikali endapo itaongeza wafanya kazi na wahudumu wa ofisi za nida, pia wakaongeza ofisi za nida zikapelekwa kwa kila halmashauri ikiwezekana kukawa na mawakala kwa kila kata itasaidia sana kwa sababu ;​
  • Itapunguza Foleni​
  • Itaajiri watu walisoma kozi za komputa ( IT) na kupunguza wasioajiria mitaani.​
  • Itarahisisha upatikanaji wa namba za nida pamoja na vitambulisho vya nida kwa wananchi.​
  • Itawarahisishia wafanya biashara kukata na kupata leseni za biashara.​
  • Itapunguza lawama kwa wasio na nida​
HITIMISHO

Endapo Serikali na mamlaka husika itaongeza ofisi za nida pamoja na wahudumu wa nida na kuboresha huduma zinazotolewa ofisi za nida, Hakika wananchi watafurahia huduma zinazotelewa na ofisi za nida wala hawatapata uvivu na ugumu wa kutafuta namba ya nida kwa wale ambao hawajapata namba na wale ambao wametimiza umri wa miaka 18. Pia hata wahudumu watapumua hawatachoka sana kama sasa na rushwa pia itapungua.

chanzo chake; youtube

NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWAKO MSOMAJI PIA NATUMAINI WARAKA WANGU UTAFIKA MAHALI HUSIKA


 

Attachments

  • NIDA__MKOAN_MOROGOR_YASEMA_CHANGAMOTO_YA_UANDIKISHAJI_SI_KUBWA(144p).m4v
    18.3 MB
  • Azimia_kwenye_foleni_akisubiri_kupata_namba_ya_NIDA(144p).mp4
    1.6 MB
  • Wananchi kuibiwa pesa zao, wanatoa fedha kwa wahudumu ili wasipage foleni na fomu zao zishughulikiwe mapema na wapate namba za nida mapema. Ambapo wakati mwingine wanatoa pesa lakini hata hivyo ingawa wametoa pesa zao namba za nida hawapati na wanapanga foleni kwa sababu wametoa pesa kwa watu wasio sahihi au wasiohusika.​
  • Wananchi kusajiliwa namba zao za simu kwa namba ya nida ya mtu mwingine. Ambavyo ikitokea wametofautiana kidogo na mtu huyo aliemsajilia laini, mwenye namba ya nida anaamua kumfungia laini yake​
Baadhi ya vitu kama hivi ni mtu pia anajisababishia. Muda mwingine yakiwakuta wajifunze pia.

Japo changamoto nyingi umeelezea kwa kweli tunahitaji suluhisho.

NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWAKO MSOMAJI PIA NATUMAINI WARAKA WANGU UTAFIKA MAHALI HUSIKA
Ahsante nawe kwa kuandika mawazo
 
Back
Top Bottom