Kwa namna yoyote ile huwezi kuifananisha (kwa ubora) elimu ya kikoloni na elimu baada ya ukoloni.
Elimu ya kikoloni haikulenga kumuelimisha kikamilifu muafrika wa Tanganyika na Zanzibar. Lengo la elimu hiyo ilikuwa kutengeneza kada ya waafrika weusi ambao wangeweza kufanya shughuli ndogondogo za kusaidia utawala wa kikoloni. Walitaka walimu ambao watafundisha waafrika weusi elimu ya msingi, walitaka kupata wasaidizi wa ofisini na matarishi ili kurahisha shughuli za utawala.
Kama haitoshi elimu ya kikoloni ilikuwa ya kibaguzi huku ikilenga watoto wa kiume wa viongozi (machifu) na watumishi wa kanisa (kwa upande wa Tanganyika).
Hata aidiolojia ya elimu ya kikoloni ililenga kutengeneza watu wanaoabudu na kusifu utamaduni wa mtu mweupe. Ukiongea kiingereza unaonekana wewe ni mtu wa maana (hi ipo mpaka leo).
Kuhusu walimu kuwa hawana sifa hapana hiyo ninakataa. Tunazo shule za serikali ambazo zinafanya vizuri sana. Zipo shule binafsi ambazo nazo zinafanya vizuri sana. Walimu wake ni hawahawa tunasoma nao kwenye vyuo hivihivi vya Tanzania. Ni imani yangu kuwa uongozi wa sehemu husika, uzalendo pamoja na uwekezaji mzuri zaidi vikizingatiwa vitaboresha kiwango cha ubora cha walimu wetu. Vigezo vya kujiunga na mafunzo ya ualimu viko vizuri.
Sasa mkuu unakataa nini unakubali nini?
Ikiwa ulibahatika kuingia darasa hilo miaka kidogo kabla ya uhuru na miaka michache baada ya uhuru utaona tofauti kubwa.
Kwanza kulikuwepo eneo rasmi liliotengwa kujenga shule ikiwa na vyumba vya madarasa,ofisi za walimu,maktaba,nyumba za kuishi waalimu ,vyoo ,messroom,viwanja vya michezo,usigeweza kujenga shule ambayo haina kiwanja cha mpira au shule imezungukwa vilabu vya pombe,au ma guest house,wachuuzi n.k
Pili idadi ya wanafuzi katika darasa mmoja hawakuzidi wanafunzi 45.wote walipata madawati.
Ilibidi mwanafunzi awe amefahulu sawa sawa kabla ya kupanda darasa,sio mambo ya sasa mwanafunzi anamaliza darasa la 7 hajui hata kuandika au hesabati harafu eti kafaulu kuingia sekondari!
Shule zilishehena vifaa vya kufundishia wanafuzi.
Kulikuwepo na elimu mahususi ya kazi za mikono kama masomo ya carpentry kwa wavulana ,domestic science kwa wasichana,ufugaji na kilimo kwa wanafunzi wote.zukimaliza std 8 ungweza ukajiajiri kama umeshindwa kupata nafasi ya kuendelea na masomo.
Somo la michezo lilikuwa lazima na mashindano yalifanyika kati ya darasa hadi shule na shule mbali mbali ndio waliibuka wanamichezo wengi kuliko sasa ambako hata uwanja wa mpira hawana.
Mkuu acha propaganda elimu ya shule zetu ipo kisiasa zaidi kuliko uhalisia kama ulioni hilo imekula kwako.
Hivi unadhani kwanini baadhi ya wazazi husaka elimu tena kwa gharama kubwa ndani na nje ya nchini kutokea kindergarten hadi elimu ya juu?
Kwasababu wanajua fika kuna kasoro kubwa na hawana muda wa kusubiri.
Hapa kuna mjadala kwanini watu wengi wanahitimu vyuo vyetu kwa malaki lakini hawapati ajira.Majibu mepesi wanadhani ajira ni ya ndani ya nchi yetu tu,lakini tumeshindwa kutoa elimu bora yakuweza kufanya kazi nchi za nje kama mataifa mengine.
Tuna walimu,wanasheria,madaktari, wahandisi,wahandishi,mafamasia,Bwana shamba na fani nyingine wamekosa ajira,lakini kama wangetayarishwa Kibiashara wangeweza wakafanya kazi nje tukavuna pesa za kigeni.
Kupanga ni kuchagua.