Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Wadau heshima kwenu.
Taifa lolote likitaka kufanikiwa ni lazima liwekeze kwenye elimu. Uongozi wa awamu zote umefanya ulivyoweza Kuboresha elimu nchini Tanzania. Serikali ya awamu ya tano nayo haiko nyuma na imejitahidi sana katika Kuboresha elimu.
Serikali ya awamu ya tano ndiyo inayotekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014. Sera hii inataka wanafunzi wa elimu ya awali na msingi wapate elimu bila malipo katika shule za umma. Moja ya mafanikio makubwa ya utekelezaji huo ni ongezeko la uandikishaji wanafunzi na ufaulu (tembelea tovuti za wizara ya elimu, sayansi na teknolojia na TAMISEMI kwa taarifa zaidi).
Katika jitihada hizo, serikali ya awamu ya tano inatoa shilingi bilioni 23 kila mwezi kwaajili ya elimu bila malipo. Katika kipindi cha miaka 4 mpaka mwaka wa fedha uliopita (2016 - 2019), serikali ilitumia shilingi bilioni 42 kukarabati shule zake kongwe 42 kati ya 88 zilizopo sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Kila shule kongwe ilipata bilioni 1 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa, mabweni, maabara na nyumba za walimu. Bajeti ya mwaka Jana ilitengwa shilingi bilioni 450 kwaajili ya mikopo ya elimu ya juu.
Hizo ni jitihada kubwa na kipekee niipongeze serikali. Pamoja na jitihada hizo ninaamini zipo changamoto mbalimbali.
Je, changamoto hizo ni zipi? Upi ushauri wako kwa serikali ili kiwango cha ubora wa elimu nchini Tanzania kiwe kikubwa zaidi?
Amani Msumari.
Tanga