Ushauri kwa Sekretarieti ya Ajira Serikalini (PSRS)

guojr

Member
Dec 4, 2015
55
82
Habari za muda huu wana jukwaa, leo ningependa kutoa ya moyoni kuhusu majanga yaliyonikuta katika mchakato wa kuomba kazi Serikalini. Huenda sio mimi tu bali wengi wetu yametutokea au yanatukwaza kwa namna moja au nyingine.

Nitazungumzia mambo matatu ambayo kwa maoni yangu yanapaswa kuangaliwa na chombo hiki muhimu cha ajira za Serikali. Lengo la kuandika bandiko langu hili ni kuangazia changamoto zilizopo na namna ya kutatua.

Moja, unapofanya maombi ya kazi kwenye mfumo wa ajira portal hakuna ujumbe wowote unaoupata kwenye barua pepe wala simu. Namna hii inaweza kubasabisha mtu akapishana na tarehe za usahili kwani hupigiwi simu wala kutumiwa ujumbe wowote kama wanavyofanya makampuni binafsi.

Maana yake unatakiwa kila mara uchungulie kwenye mfumo wa maombi, kwa karne hii ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni kwanini basi Sekretarieti isifanye jambo hili kuwa jepesi kwa kuwatumia wahusika ujumbe aidha kwa simu au barua pepe? Hili bila shaka linawezekana na lipo ndani ya uwezo wenu, naomba mlifanyiekazi.

Pili, kuna ulazima gani mtu atoke mkoani aende hadi Dar es Salaam au Dodoma kufanya mtihani wa makaratasi? Kampuni nyingi kubwa na ndogo duniani zinafanya usaili wa awali kupitia mtandao.

Kama ni maswali yanawekwa kwenye mfumo wa usaili na mtu anafanya maswali hayo akiwa popote duniani na hata usaili wa ana kwa ana siku hizi unafanyika kwa mtandao. Hii inasaidia kuwapa fursa watu wengi zaidi na pia inawapa nafasi watu wengine waliotamani kushiriki ila wana dharura mbalimbali.

Tatu, kuna sehemu kwenye mfumo wa ajira unachagua aina ya notification na aina za jira unazotaka ili ikitokea utumiwe ujumbe lakini sidhani kama zinafanyakazi. Nadhani mna kazi kubwa ya kufanya ili kuuboresha mfumo huu, naamini inawezekana na italeta tija.

Wasalaam.
 
Au wawatume maafisa wao kila mkoa kwa ajili ya usaili wa kuandika na warudi na majibu makao ya tume ili wasahishe na kisha watoe majina ya usahili wa ana kwa ana, hao ndio wafanye mahali pamoja (ikiwa wa njia ya mtandao utashindikana).

Ni rahisi sana kulipa posho na nauli watu 24 (ukiachana na Dar na Dodoma ambako tuke wana ofisi zao) waende mikoani kuendesha mitihani kuliko kusafirisha watu elfu 9 ili tu waje uwapunguze kwenye orodha na kuonekana mchakato ulikua fair. Inauma sana umeingia gharama kusafiri na ukafeli usahili
 
Tatizo mifumo hyo notification haifanyi kazi kabisa kwa kweli atleast wkwemy oral au paper wawe na ofisi za kanda iwe rahsi kidogo ila watahiniwa achague afanye popote.
 
Sisi ofisi ya utumishi tunafanya hivi ili kupunguza idadi ya watu wanaoomba hizo ajira na ukizingatia tunakuwa na vijana wetu tumewahifadhi kwenye data base na pia kijana usitufundishe kazi sio lazima kila mtu aajiriwe. Tukiajiriwa wote nani atakuwa kibarua wa shambani?
 
Sisi tunajadili issue ya maana analeta utani
tatizo kuna baadhi ya watu hawatumii akili zao kufikiri bali wanatumia vijambio vyao kufikiri, wanaleta utahira kwenye sensitive issues, zile pesa zilizotupwa kwenye interview ya mwisho iliovuja wanalifumbia macho na kutuletea mawazo mavi
 
Sio kwamba hayo uliyosema hawayajui ila Tatizo ni posho, hayo mawazo yakifanyiwa kazi inamana posho kwa wale maafisa pale zitakata kitu ambacho wao hawapo tayari
 
Ndo mpaka wakusikie sasa 2030 umeshazeeka..
Mara 100 wangekiua hiki chombo PSRS Kama ndio hivo waachie waajiri mamlaka au taasisi husika iajiri kinazidi kukandamiza watoto wa maskini kwa gharama zinazo wagharumu kwenda UDOM mji wa gharama TZ na madudu yanayo jitokeza
 
Back
Top Bottom