Jana usiku tulikuwa kwenye sherehe ya Harusi pale Isamilo Lodge. Ilipofika muda wa saa tano na nusu ghafla umeme ukakatika. Nilitumaini kwa hadhi ya hoteli kama ile kungekuwa na jenereta ya tahadhari (standby generator) ili ratiba iendelee kama ilivyopangwa.
Baada ya kusubiri ili jenereta iwashwe lakini hata hivyo hakuna kilichofanyika. Ilibidi ratiba zilizobaki zivunjwe na wote kutoka ukumbini.
Nimeelezwa kuwa Mmiliki ya ile Lodge ni Mheshimiwa mmoja mkubwa katika Mkoa wa Mwanza. Hivi kweli logde kubwa kama ile inakosa jenereta?.
Tulikuwa na Mhe. Mbunge wa Magu na nilimueleza amfikishie ujumbe mmiliki wa lodge hiyo mapungufu yaliyoonekana ili ayarekebishe vinginevyo atakuja kukosa wateja siku za usoni.