Ushauri kwa Mheshimiwa Magufuli: Biometric time attendance machine

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,551
1,777
Habari wana JF,

Katika wiki mbili zilizopita kumekuwepo na mijadala mingi kuhusiana na suala la wafanyakazi hewa.Ukweli no kwamba suala hilo limekuwepo miaka nenda rudi lakini hakuna aliyethubutu kulichukulia hatua kutokana na uzembe wa viongozi ambao kwasababu wanazozijua wao leo tumefika hapa.

Suala la wafanyakazi hewa haliishii kwenye waliokufa na ambao hawapo kwenye workstation zao, bali kuna wale ambao hutumia masaa mawili au matatu kukaa ofisini na muda unaobakia huenda kufanya mambo yao binafsi na kufanya utendaji kuwa mbovu na wakusuasua (group hili ndilo kubwa zaidi kuliko mengine yote).

Ushauri wangu kwako mheshimiwa Rais ni kwamba ni aibu kwa taifa kubwa kama Tanzania karne ya 21 taifa kuzizima kwa ajili ya wafanyakazi hewa maana nahisi kinachofuata itakuwa watanzania hewa n.k.

Ni wakati muhimu kwetu kwa gharama yoyote kuondoka na mfumo wa log book kwa ajili ya attendance, badala yake Biometric attendence machines zitumike.Salary ya kila mtumishi itokee kwenye biometrics machines. Kipindi cha ku instal tutatujua mpaka sasa kuna watumishi wangapi,waliokufa watajulikana na watoro watakula kwa jasho lao.

Nawasilisha.

Asubuhi njema
 
Hongera sana Mkuu kwa wazo lako safi! Mawazo kama haya ndiyo yanatakiwa kutolewa na GT hapa JF na siyo kukashifu au kubeza jitihada zinazofanywa na serkali bila ya kupendekeza suluhisho!
 
Naam hilo litakuwa jibu la wale walioajiriwa serikali kwa kujuana. Utamkuta mtu haijulikani anafanya kazi gani lakini yupoyupo na kila safari hukosi jina lake!
 
Hakuna haja ya ku invest mapesa mengi kwenye suala hili.

Wanaweza kutumia miondombinu iliyotumiwa na tume ya uchaguzi au hata ile wanayotumia TRA katika kutoa lesseni au ile inayotumia kutolea Passports au ile ya NIDA:).
 
mtoa mada unajua kuwepo kazini hakuna uhusiano na mtu huyo kufanya kazi? mahudhurio sio ishu kabisa.
 
Hii ikiwekwa sawa kabisa, najua itaanza na wakuu wa vitengo ndo watoro kuliko
 
Hakuna haja ya ku invest mapesa mengi kwenye suala hili.

Wanaweza kutumia miondombinu iliyotumiwa na tume ya uchaguzi au hata ile wanayotumia TRA katika kutoa lesseni au ile inayotumia kutolea Passports au ile ya NIDA:).
Mkuu unaweza ukawa sahihi kutokatona na jinsi ulivyonielewa ila nna haya ya kukueleza
1. Kwanza ni sahihi kutumia pesa nyingi kwenye hili kutokana na ukweli kuwa pesa zinazopotea ni nyingi kuliko tutazotumia kununua biometric machines.ndio maana hata fence za umeme zipo uzunguni na kwa matajiri kwa hofu ya kupoteza kikubwa dhaidi ya thamani ya electric fence..Swahili wewe ukiwa muoga sana uta

1. Kwanza ni sahihi kutumia pesa nyingi kwenye hili kutokana na ukweli kuwa pesa zinazopotea ni nyingi kuliko tutazotumia kununua biometric machines.
2. Suala la wafanyakazi hewa ni suala endelevu na si la mpito, sababu watu tunakufa na watu bado tunatoroka workstations zetu,how can the government monitor its employees's daily movements? Sababu kupitia fingerprint yako ndo utapata mshahara..kama umekufa watu watajua sababu hutopunch biometric halikadhalika kwa atakae kimbia workstation yake...sasa tukiazima za NIDA zitakuwa na msaada kwa kufanya surveillance ya daily movement za wafanyakazi.
Maana hapa u kiingia una punch in, lunch una punch out na kurudi una punch in,na ikifika mda wa kutoka una punch out ,hapo mfanyakazi hewa hapatikani Daima .
 
mtoa mada unajua kuwepo kazini hakuna uhusiano na mtu huyo kufanya kazi? mahudhurio sio ishu kabisa.
Mahusiano yapo mkuu...Bora mtu awepo hata kama hajishughulishi..
MF. Mwalimu akiwepo hata kama haingii class still wanafunzi wanaweza kumfuata kuuliza maswali
 
muhimu ku address sababu ya wao kutopenda kazi zao na kuzishughulikia
 
Mkuu unaweza ukawa sahihi kutokatona na jinsi ulivyonielewa ila nna haya ya kukueleza
1. Kwanza ni sahihi kutumia pesa nyingi kwenye hili kutokana na ukweli kuwa pesa zinazopotea ni nyingi kuliko tutazotumia kununua biometric machines.ndio maana hata fence za umeme zipo uzunguni na kwa matajiri kwa hofu ya kupoteza kikubwa dhaidi ya thamani ya electric fence..Swahili wewe ukiwa muoga sana uta

Mkuu unaweza ukawa sahihi kutokatona na jinsi ulivyonielewa ila nna haya ya kukueleza
1. Kwanza ni sahihi kutumia pesa nyingi kwenye hili kutokana na ukweli kuwa pesa zinazopotea ni nyingi kuliko tutazotumia kununua biometric machines.
2. Suala la wafanyakazi hewa ni suala endelevu na si la mpito, sababu watu tunakufa na watu bado tunatoroka workstations zetu,how can the government monitor its employees's daily movements? Sababu kupitia fingerprint yako ndo utapata mshahara..kama umekufa watu watajua sababu hutopunch biometric halikadhalika kwa atakae kimbia workstation yake...sasa tukiazima za NIDA zitakuwa na msaada kwa kufanya surveillance ya daily movement za wafanyakazi.
Maana hapa u kiingia una punch in, lunch una punch out na kurudi una punch in,na ikifika mda wa kutoka una punch out ,hapo mfanyakazi hewa hapatikani Daima .
Nilikuelewa vizuri tu mkuu. Hoja yangu ni kuwa hakuna haja kwa serikali kuwa na duplicate systems. Tunaweza kuweka utaratibu mzuri tu ambao unatumia system mmojawapo kati ya ambazo tayari zipo (hata kwa kuongezea uwezo hapa na pale) . Ndio sababu nikasema wanaweza kutumia system ambazo tayari zipo badala ya kuanzanza kununua mitambo mengine kwa gharama kubwa. Kwa mfano ile ya tume ya uchaguzi kwa sasa hizi inafanya kazi gani? Au hata ya NIDA nayo inafanya kazi gani?
 
huku kwetu halmashauri ya wilaya ya mvomero alipopatia ajali sokoine hizo mashine tumeanza kuzitumia muda tu,mwezi wa sita huu,unasign kwa finger print tu,kuingia na kutoka ofisini,then kila ijumaa afisa utumishi anaprint ripoti ili kuona watoro na hatua gani za kiutumishi za kufuata,displine ya kazi imerudi aisee,no utoro,mtu asipokuja ofisini ni kwa sababu maalum tu
 
Back
Top Bottom