Ushauri kwa Ester Matiko (MB)

Ushauri kwa Ester Matiko (MB)

Pascal sasa hivi ashatiwa upofu na teuzi maana kila teuzi zikitoka yeye anapigwa za shingo tu
Kama mawazo ya kuona mbali ni 2020, bado watakua hawaoni mbali! Mwaka huo siyo mwisho wa Tanzania, Tanzania itaendelea kuwepo wakiwa wameoza makaburini! Ona mbali, Paskali!
 
Kweli kabisa!

Wewe uliona wapi eti kwenye sera cha chama wanaweka picha ya mwenyekiti wao kjonesha kwamba huyo ni wa kudumu
 
Pascal siku hizi ashakuwa zuzu au vuvuzela lisilo na mpulizaji
Sikutaka ku comment uzi huu !!, lakini nilipoona nawe unapotosha umma nikashangaa !!.

Hivi kweli Pascal, wabunge woote wawe CCM ndiyo tutapata maendeleo yalishindikana kwa miaka 60 ?!. Walioiharibu Tz yetu ni nani kama siyo hawa hawa CCM ?! Kweli Pascal nawe unaamini kuua upinzani kwa gharama za dola ndiyo malengo ya taifa!!!

WaTz ni waswahili na wanafki !! Yaani wote wakawe wapiga meza na kusema ndiyoooooo!! Mungu anawaona, acheni turudi kwenye u communist. Lakini tutaendelea kurudi nyuma ki maendeleo, kama ilivyokuwa huko awali .
 
Unajisumbua tu kwani mteuzi alisha kupuuza kwenye kikao kile ulipojaribu kujitambulisha kwake kuwa nawewe ni msukuma akatumia busara kukutupa na ungekuwa na akili usingeendeleea kujikomba komba na kujipendekeza maana hutokaa upate uteuzi
Kwenye siasa za Tanzania, tuna makundi matatu ya watu, the dreamers, the wishful thinkers, and the realists.
Dreamers wao wanaota tuu. Wishful thinkers wao wana wish, na realists wao wanausema ukweli uliopo, hivyo ukweli wa siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa 2020 ni huu
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
P.
 
Mh. Ester Matiko. Napenda kukupokeza kwa Kazi nzuri unazozifanya jimboni. Wewe ni Mbunge makini lakini hauko kwenye chama makini. Nakushauri hamia CCM ambacho ni chama makini ili uweze kufanya vizuri Kazi za kuwaletea maendeleo wananchi wako. Fuata nyayo za Mbunge wetu wa Serengeti Marwa Ryoba. Ni matumaini yangu utanisikiliza.
Mtaendelea kuwarubuni hao hao lakini sio kwa Ester Matiko, anajitambua.
 
Mh. Ester Matiko. Napenda kukupokeza kwa Kazi nzuri unazozifanya jimboni. Wewe ni Mbunge makini lakini hauko kwenye chama makini. Nakushauri hamia CCM ambacho ni chama makini ili uweze kufanya vizuri Kazi za kuwaletea maendeleo wananchi wako. Fuata nyayo za Mbunge wetu wa Serengeti Marwa Ryoba. Ni matumaini yangu utanisikiliza.
Ni mpuuzi pekee atakaefurahia upinzani kumalizwa......Ili tusonge mbele lazima kuwe na watu wa kutukumbusha na kufungwa gavana pia.
Mark my word
 
Upinzani ndo unawafanya mpige kelele na kujiona mko kwenye raiti traki. Ngoja 2020 mbaki wenyewe. Tutaona vituko sana.
Rais hatakuwa na muda tena na wananchi. Hizo ziara zake za kampeni za sasa hazitakuwa na maana tena.
Ndo utakuwa muda wake mahsusi wa kuwashughulikia ccm wenye viherehere wanaotaka kumgusa mkono wakati wa mlo wake wowote ule.
Lazima mtasaga meno.
 
Msiwapotoshe watoto wetu maana mpaka sasa watoto wadogo mashuleni wanaamini kuwa mpinzani ni kosa kumbe ni utaratibu rasmi wa kuwa watu wenye mawazo mbadala na ndio maana bungeni kuna mawaziri vivuli na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani ambaye anagharamiwa na serikali. Hapo tu inaonyesha upinzani ni kitu ambacho kinakubaliwa kwani hata kama utakuwa hujashika uongozi lakini bado unaweza ukawa na mawazo mbadala ambayo yanamsaidia yule anaetawala kuweka mambo sawa.

Hata huyo mbunge unaemwona makini bado ana fursa ya kuijenga nchi akiwa huko huko alipo
Mkuu siasa nyepesi na zinazofanywa na wanasiasa uchwara hasa wa awamu hii zimeua kabisa uwezo wa watanzania wengi kufikiria hivyo hawawezi ona hiki ulichoandika hapa wala kujua dhamani yake. Kiukweli Tanzania awamu hii imepatwa, si viongozi, si wananchi wote bahati mbaya, yaani mpaka nabubujikwa na machozi
 
Ccm ndio kuna maendeleo?... mbona miaka 50 mnayo lkn bado tunahangaika kupata maji tu.
... Maendeleo hayana chama (jinga voice)
 
Back
Top Bottom