KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Pamoja na kukubaliana na uliyoandika hapo juu kuhusu ajenda zinazowagusa wananchi kwa haraka na moja kwa moja, sikubaliani kabisa na kipande hiki nilichokinyanyua hapo juu.Tuachane na siasa za kukariri ajenda za nchi zilizo endelea, wao wamesha endelea hivyo hawashughuliki sana na shida tunazosumbuka nazo sisi nchi maskini. Tunashirikiana tatizo moja tu la ajira lakini hayo mengine kwetu siyo ipaumbele chetu watanzania ambao bado tunapigania uhakika wa matibabu , mavazi na chakula.
Huwezi kuniambia kwamba mwanakijiji au mzee mjini haoni thamani ya kura yake anapokwenda kupiga kura, na kwa hiyo mshindi yeyote atakayetangazwa kwake ni sawa tu.
Kwa nini udhani tu kwamba huyo mzee mjini au raia kijijini hataki kusikia michango anayotoa mwakilishi wake bungeni kutetea waliyomtuma kuyawasilisha?
Kwa nini wewe unadhani watu hawa wanapoonewa huko walipo, na hata wakabambikiziwa makesi ya hovyo, kwao isiwe mhimu kuondoa ukiritimba huo, wewe unaona hayo ni yale yanayowahusu binaadam tofauti kabisa na wao wanaoishi nchi zingine?
Kila binaadam anataka atendewe HAKI, awe ni wa nchi zilizoendelea au hizi zetu za kiafrika.
Hizi mbinu mnazotumia kuwatishia ndizo mnazozigeuza kueleza kwamba wao haki zao sio mhimu kwao?
Hizo ajenda za mazao na mengineyo uliyotaja utazitenganisha vipi na hizi ajenda za msingi unazoona wewe kwamba sio mhimu kwa wananchi?
Kiongozi akiamua tu kwa hiari yake bila hata kujua taratibu zilizopo, akaingilia manunuzi ya mazao ya wakulima, kwa madaraka yake tu bila kufikiri madhara yanayoweza kuwapata wakulima kwa kukosa kabisa faida ya mazao yao, wewe hilo huoni kabisa kwamba ni ajenda inayostahili kufikisha kwa wananchi waelimishwe na wafanye maamuzi sahihi wasiendelee kupata hasara ya kazi zao?
Ajenda za msingi katika kampeni hii ni kuwaelimisha wananchi wajue haki zao, wasinyimwe haki kwa mabavu tu ya mtu mmoja kwa kutumia majeshi.
Wananchi wakizijua haki zao watakataa kuendelea kuonewa.
Tuachane na "siasa za kukariri..." - Hebu nieleze kama uliyoandika katika mstari huo sio mambo ya kukariri tu na kutumia mipasho unayoisikia ikitumika bila kuipa uzito wa fikra nyuma yake!