Ushauri kutatua tatizo la wafugaji

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,596
8,738
Ndugu zetu Wamassai na Wamang'ati wamekuwa na ufugaji kiholela karibu Tanzania nzima. Kwa ufupi hawa wafugaji wanaishi kwa utaratibu wao wenyewe bila kufuata sheria yeyote. Lakini kibaya zaidi wanaharibu mazingira sana na ni lazima kuwekwe utaratibu. Huko Arusha ndiyo kabisa kumekuwa kama jagwa na sasa wameingia Ngongogoro.

Ushauri wangu ni kwa serikali kuanzisha mbuga maalumu za wafugaji. Mbuga hizi ziwe na wataalamu wa mazingira, lakini wawekewe huduma muhimu kama Watanzania wengine. Mbuga hizi za wafugaji ziwe kila pande kuu za nchi . Kwa mtazamo wangu mbuga kuu kumi zinatosha. Huko ndani watengenezewe mabwawa, kuwe na utaratibu wa mupanda miti na majani ya chakula cha mifugo. Kitu kizuri kimoja ni kwamba mchango wa kuingia huko au kodi ni hiyo hiyo mifugo. Hivyo wafugaji ni lazima wachangie mifugo kama kodi ili waweze kuwekewa huduma za mbuga na uwekezaji. Kwa ufupi serikali iwasaidie wawe na ushirika wa wafugaji ndani ya hizi mbuga maalumu. Serikali itafaidika kwa mambo yafuatayo

1. Itasaidia kulinda mazingira
2. Itasaidia wafugaji kuweza kuuza mifugo yao kwa utaratibu
3. Itapunguza migongano ya wakulima na wafugaji
4. Itasaidia kuwatambua na kuwapa vibali wafugaji
5. Itasaidia wafigaji kupata huduma kama za Afya na Elimu
6. Itasaidia serikali kupata kodi

Bila hizi tutakuwa na matatizo. Ngombe wao hawana afya nzuri, pesa hawana na wanakaa na ngombe mpaka wafe. Lakini kwa hali ya hewa inavyoendelea tutakuwa na migogoro zaidi.

Zitto ,Mwigulu Nchemba
 
Wafugaji wa Ngorongoro wana ng'ombe 1M sasa wanaosema wataenda kuongea nao je watueleze maongezi ya nini? Kuna sehemu nyingine ya kuwapeleka? Ushauri wangu ni mbuga maalumu tu ndiyo suluhisho
 
Ongezea na wasukuma

Ova
 
Ranchi si zilikuwepo?
Nani aliziua hizo ranchi

Ova
 
Ranchi si zilikuwepo?
Nani aliziua hizo ranchi

Ova

Bahati Mbaya wakati wa Mkapa Lowassa alipewa hii wizara akagawa zile Ranch kwa marafiki zake na wafanyabiashara. Baba yangu mdogo mfano alipewa Handeni, Lowassa naye Handeni hata morogoro ..... hizi sio za wale fafugaji wa kimasai. Nashauri mbuga kabisa sio ranch bali mbuga za kukaa watu mpaka 50,000 kwa mbuga na ng'ombe 1m kwa mbuga
 
Back
Top Bottom