Ushauri: Kuongeza Tax base, Rais na Wabunge walipe Kodi

Ushauri: Kuongeza Tax base, Rais na Wabunge walipe Kodi

Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Hili limefika hapa Kwa sababu nyingi ambazo tumekkuwa tukizipigia kelele Kila kukicha,

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

2. Wabunge mishahara Yao ukatwe Kodi na posho zao zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Yakifanyika hayo, wote tutakuwa sawa mbele ya Sheria na tulipe Kodi na wote tuhisi uchungu wa kulipa Kodi Ili pia tuzisimamie vizuri.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏

Taabu zaidi ni pale bungeni wapinzani na CCM kwenye maokoto yao lao, moja.
 
Hapo kwa Rais tunaweza kuacha, kuna mawaziri, wabunge, majaji etc hawa walipe kodi kwa mafao wanayapata. Haileti maana mtu wa kawaida hata ukilipwa laki tatu unapaswa kulipwa kodi huku watajwa hapo juu wakibeba mafurushi ya fedha bila kulipa hata mia.
Babu yangu alikuwa judge, alipostaafu aliendelea kulipwa 80 ya mshahara wake Hadi mwisho wa uhai wake.

Sasa hii haitakiwa Kwa nchi maskini.
 
Mimi ningekuwa Rais mkaniletea hilo pendekezo ningevunja bunge ili turudi kwenye uchaguzi.... nafikiri ni rahisi zaidi kupitisha sheria inayosema wenza wa marais na wabunge pia wasilipe kodi
 
Ila kweli na pia hawajui Bei ya LUKU Wala gesi na tuliokuwa tumeanza kujaribu kupikia umeme tumekwama ! Maana unit ya umeme Bei JUU huruma !
Wao kuongelea matatizo ya wananchi ni maigizo tu,

Hawa he angaiki kulipa Kodi ya pango, hawalipi ada, umemea Bure, maji Bure, vyakula vinajaa stoo,

Ni raha mustaehe!!
 
Hata Lissu, Lema na Mbowe hili hawatolikubali, watakwambia Eti KAZI Yao ni ngumu hivyo mishahara ya wabunge ni kiduchu🤔

Tuige Uingereza, wabunge wanalipwa kiduchu sana, ni KAZI ya kujitolea.

Ni kama wale wenye kusema ruzuku ni kwa mujibu wa sheria.

Kwamba eti wasilaumiwe wao, hali hawafanyi lolote kuonyesha ruzuku ni unyonyaji.
 
Salaam, Shalom!!

Akiongelea Suala la Kodi, Mh Rais amesema kuwa tax Base ya nchini petu ni chini ya milioni mbili.

Hili limefika hapa Kwa sababu nyingi ambazo tumekkuwa tukizipigia kelele Kila kukicha,

Kwa kuwa kiongozi wetu amedhamiria kuongeza Tax base Ili wengi zaidi wapate hamasa ya kulipa Kodi, ninamshauri yafuatayo:

1. Kiongozi wetu Mh Rais SSH aelekeze hazina Ili mshahara wake utajwe hadharani na ukatwe Kodi na posho zote zikatwe Kodi.

2. Wabunge mishahara Yao ukatwe Kodi na posho zao zikatwe Kodi.

Si vyema watunga Sheria na sera za Kodi nchini wasamehewe kulipa Kodi ilhali viongozi wa juu Wachache hawalipi Kodi, hii Si HAKI.

Yakifanyika hayo, wote tutakuwa sawa mbele ya Sheria na tulipe Kodi na wote tuhisi uchungu wa kulipa Kodi Ili pia tuzisimamie vizuri.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Naunga mkono
 
Sasa hapa mada inataja wabunge kama ndio ushauri.
Labda aweke hivi....kila mwanasiasa akipokea pato akatwe X% itakayohudumia shughuli za siasa na maendeleo.hiyo ndio significant number in taxation.yaani unaanzia mjumbe wa serikali ya mtaa hadi kada wa chama...that is number!!that is inclusion.
Hata ukipokea zawadi ya pesa ukatwe Kodi. Hata posho za vikao vya bunge zikatwe Kodi.

Tuanzie na hao wa juu kuja chini, Si kuanzia chini kuja juu hapana.
 
Hata ukipokea zawadi ya pesa ukatwe Kodi. Hata posho za vikao vya bunge zikatwe Kodi.

Tuanzie na hao wa juu kuja chini, Si kuanzia chini kuja juu hapana.
waliopo juu ni wachache sana hakutakuwa na significant impact.Tax base lazima iwaguse watu sio chini ya Milioni 40 ...hapa ninatoa wazee na watoto.number my friend!!number!!
hata hii tume isipokuja na number itabidi irudishe posho.
Zaidi TRA Ianze kutoa takwimu za nyumba ambazo tulisajili mwaka juzi na zilizolipa kodi ya jengo...kila mwezi.
 
Ni Kweli,

Numbers don't lie,

Rais na wasaidizi wake na wabunge na high ranking Government officers ni kundi dogo lisilolipa Kodi ila ndilo litumialo pesa za umma Kwa ukubwa sana kuliko walimu wote nchini ambao ni 150,000+

Numbers don't lie!!
 
Back
Top Bottom