Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,171
- 3,346
Kwa ushauri tafuta Collora XE/SE 110 au Collora Filieder ZNE Vvt i ni gari zinatumia mafuta kidogo (CC 1500) kulinganisha na gari kama Premio (CC 1800- 2000). Spea zake zinapatikana kwa wingi bila shida kifupi Nairobi haitakuhusu kabisa.Habari wanajf;
mimi ni mtumishi wa umma na kipato changu ni Tsh 400000/=(take home)
nataka kukopa mojawapo ya gari hizi forester/ suzuki escudo/corona premio.
Naomba ushauri kama kuna sehemu naweza kupata mkopo wa aina hiyo(achilia mbali kukopa fedha taslimu kutoka bank)
msaada jamani nshachoka kupanda dala dala.
Taratibu za Exemption ni hizi:-
- Mshahara wako uaanzie TGSD (kwa wewe ume qualify)
- Kodi zinazo samehewa ni Import Duty (25% ya CIF) na Execise dut(5% kwa gari zenye CC (0-1500) na 10% kwa gari zenye (CC 1501- ). Uchakavu hausamehewi na ni 20% kabla ya VAT(18%). Uchakavu ni kwa magari yote yalitengenezwa zaidi ya miaka kumi, hivyo ukiagiza gari la mwaka 2001 kwa saizi hadi lifike litakuwa tayari limeshamaliza miaka kumi toka kutengenezwa hivyo uchakavu ni lazima ukuhusu.
- Unaandika barua kupitia mwajiri wako kwenda Sub Treasury baada ya kujazwa fomu toka TRA ambayo inajieleza. Viambatanisho katika barua hiyo ni Salary Slip (Current), barua ya kupandishwa cheo kama ulikuwa hujafikia daraja hilo, TIN namba.
- Gari liwe kwa matumizi ya kawaida na siyo biashara.
Kama unataka kukopa ni bora ukakope kwenye bank/ SACCOS (kama mnayo kwa minajili ya riba) kuliko kwenda kwenye makampuni yanayouza magari watakupiga riba kubwa sana.
Ushauri wa mwisho, kabla ya kukopa hakikisha umesave angalau 1.6m -2.0m ili ujazie hicho kiasi kingine na ubakie hata na salio kidogo la kulihidumia gari hilo kwa kuweza kulipa motorvehicles license na mingeneyo ya barabarani.
Kila la kheri katika safari yako ya kutaka kutembea huku UMEKAA.