Ushauri kuhusu mkopo wa gari

Forester hautaiweza niliagiza kutoka Dubai hadi inaingia nchini ilnighalimu kama 5.7 m hivi lakini niliiuza kwa 4m kutokana na spea kuzingua ilikuwa mpaka nizifate Mombasa ndio kuna wakala wa Subaru
hapo kwenye forester mbona umeguna,tatizo ni bei,spea au unywaji wa fuel?
 
kwa nini msimshauri anunue carina my road ya cc 1450 ya 2003. mbona naziaminia sana kwa kila kitu
 
Spea sio issue maana hawa dada zetu wanatumia gari vizuri, so nashauri nunua corola haina ufundi, pia inaweza kwena masafa marefu...haya mengine yanaweza kuchemsha anytime. kuhusu mkopo please angalia interest rates...you should go for the lowest.
 
Kamata tuktuk tu mwisho wa matatizo. Itaendana na kipato chako.
Ukiweka wese la buku 5 unazunguka round 4
Gari kwa sasa mafuta bei juu lt1=2000 ambapo kwa wiki utatumia mafuta si chini ya 80,000 pamoja na misele yako ya hapa na pale kwa mwezi piga hesabu hapo na kipato chako ni hiyo kilo 4 + na makato ya kwenye mkopo utajikuta unapokea take home chini ya laki 4 aangalia usije ukalipaki ukawa unatembelea week end tu kwa ajili ya maumivu ya mafuta.












Wewe inaonekana unafanya kazi serikalini,kwa kuwa serikali unaweza kuishi bila kutegemea mshahara (posho hazikosekani) mi nakushauri nunua gari ya maana na imara.Nunua RAV 4 old model utaitumia hadi uta-ejoy maana si gari inayosumbua na hata kwa bahati mbaya ikila mzinga haiumii sana tofauti na magari ya sasa hivi mlevi akiipiga ngumi bodi inabonyea
 
Dada, hongera kwanza una kiwanja tayari, wewe ni mtu wa maendeleo, napiga parapanda wana jamii tumsaidie mwenetu, hasa nyie mlioko huko ughaibuni si msaidieni yeye alipe ushuru jamani mbona mnakuwa hivyo, MUNGU hapendi ila.
 
Kamata tuktuk tu mwisho wa matatizo. Itaendana na kipato chako.
Ukiweka wese la buku 5 unazunguka round 4
Gari kwa sasa mafuta bei juu lt1=2000 ambapo kwa wiki utatumia mafuta si chini ya 80,000 pamoja na misele yako ya hapa na pale kwa mwezi piga hesabu hapo na kipato chako ni hiyo kilo 4 + na makato ya kwenye mkopo utajikuta unapokea take home chini ya laki 4 aangalia usije ukalipaki ukawa unatembelea week end tu kwa ajili ya maumivu ya mafuta.
jamani, me naona mnamtisha sana kuhusu wese. kama akinunua toyota permio 4A-FE engine ambayo ina cc 1587
atatumia mafuta wastan wa km 12 kwa lita 1. ruti na missele ni yeye tu
go on girl
 
Habari wanajf;
mimi ni mtumishi wa umma na kipato changu ni Tsh 400000/=(take home)
nataka kukopa mojawapo ya gari hizi forester/ suzuki escudo/corona premio.
Naomba ushauri kama kuna sehemu naweza kupata mkopo wa aina hiyo(achilia mbali kukopa fedha taslimu kutoka bank)
msaada jamani nshachoka kupanda dala dala.
vipi bidada, ulikwisha fanikiwa huo mpango?
 
bahati mbaya sidhani kama kuna banker atakaye kubali kukukata 80% kama loan repayment. The max they can go ni kati ya 40-60%. fanya uchunguzi kwanza, pia fikiria fuel, maintenace, kama utalaza ofisi ya chama-ulinzi, gharama zako mwenyewe za kuishi, etc
Mwenzako anatumia pesa toka kwenye mshahara wa kununulia nguo, vipodozi na kwenda saloon. Hayo mambo mengine kuna mapipa na vidumu...
 
I like the way you respond most of you.it show good familiality,
Naomba tuebndelee kusaidiana.
kuna baadhi ya premio corona zinakuwa na tatizo la kuchanganya oil na gas/petrol. please naomba msaada ili kuzifaham aina yake ni ipi.
thanks waungwana.
 
dada Uda vipi,huu mpango ulizaamatunda?ulitumia njia gani na sisi wadogo zako tufwate nyayo?
 
Last edited by a moderator:
Mie naomba kujuzwa anaye fahamu tax exemption kwa baadhi ya watumishi wauma wakati wakuagiza gari kutoka nje.Je ni watumishi wote wa umma au ni baadhi tu.Kama ni baadhi ni wapi wanufaika?
 
Daladala ni shida wazee, unyunyu wote unaisha ukitoka unanuka mchanganyiko wa pafyumu na vikwapa
me nakushauri uchukue ka-starlet ndugu yangu kanaserve the purpose, na hako kampunga kalivyo kaduchu utamudu tu.
SWALI KWA WANAJF: kati ya CAMI(TOYOTA) na TERRIOS(DAIHATSU) ipi bora coz naona zinafanana ila sijajua ki-maintenance na spares ziko vipi, naomba msaada wenu kabla sijaangukia pua.

Cami na terrios hamna tofauti,ukitafuta spea kwa jina la toyota cami hupati spea zake zote ni terrios,na hizo gari nilihangaika na spea mpaka nikaamua kuuza
 
Duet na raum napendekeza. Kuna mtu aliniuzia mitsubishi lancer cc 1597, sport car speed 220, tatizo ni spea hazipatikani sana, japo spea kama shockup na nyinginezo zisizo husu injini au gearbox ni za magari mengine ya toyota tu. Ninachopendea ni ulaji wa mafuta na speed ya kutosha kwa safari ndefu. Najaribu kuongezea kwa mtoa comment mmoja aliyesema gari ni mafuta, spea kama hazipatikani sana, lakini zikipatikana zinadumu, basi ishu iwe mafuta ambayo ndio shughuli ya kila mara inayofanya watu wayachoke magari.
 
habari wanajf;
mimi ni mtumishi wa umma na kipato changu ni tsh 400000/=(take home)
nataka kukopa mojawapo ya gari hizi forester/ suzuki escudo/corona premio.
Naomba ushauri kama kuna sehemu naweza kupata mkopo wa aina hiyo(achilia mbali kukopa fedha taslimu kutoka bank)
msaada jamani nshachoka kupanda dala dala.

si useme tu we ni mwalimu wa shule fulani mwenye diploma ya kisw na hist
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom