Ushauri: Kuhusu mama chui na watoto wake

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
7,798
20,745
Mama Chui akizaa watoto wake anawalea wakishakua anawaacha anaenda porini anakaa kama juma hivi akirudi anawatisha watoto wake. Yale watoto walioshtuka wakakimbia hawawi chui tena ila wale watoto waliomtambua mama yao wanabaki na mama yao na wanakuwa chui (katika uhalisia wake). Kwa sisi wachaga wale chui walioogopa mama yao anaitwa Isana; huyu isana anaenda kuishi porini huko linakuwa linazura na linakuwa kama lipaka la kawaida ambalo linaishi porini lenyewe. Huko nyumbani Isana huwa yanakuja kuiba nyama jikoni ila ukiliangalia unaweza sema chui ila lioga haliwezi fanya chochote kile kukudhuru.

Funzo:
Katika maisha changamoto ziko nyingi sana na mwanadamu huwa anapitia changamoto hizi na mwanadamu anaweza kufikiri kuwa Mungu kamuumbia matatizo, kitu ambacho si kweli. Shida zinakuja kwa mwanadamu ka kujitakia wenyewe kulingana na maisha ambayo tunapitia. Kwa mfano: Kuna watu wana

Watu wanataka urahisi wa kupewa majibu katika maisha na wengi wao hawaendelei mpaka waonyeshwe njia. Nafafanua: Kwa mfano mwalimu wengine wanasahihisha njia na sio majibu ila wenhine wanasahihisha maibu sio njia. Maisha yako hivyo vivyo kuwa kuna watu wanapitia majaribu mengi katika maisha yao ila majibu ya yanakuwa mafanikio na wengine katika njia hizi wanapopatia mafanikio.

Wadhungu wanasema: What does not kill you makes you stronger (kama sijakosea maana yake: kisichoweza kukuua kinakufanya uwe jasiri). Binadamu wanaopitia changamoto wengi wao zinawajenga na kuwafanya imara katika maisha yao na njia zao au majibu yao huwaleta mafanikio. Isana hana ujasiri tena ila litafanana na chui litakuwa halina asili ya uchui tena. Hivyo kuna watu katika maisha wanakuwa kama Isana mwisho wake wanazunguka tu dunia mpaka kifo kinapowakuta. Watu hawa hawana ujasiri kabisa na mwisho wanajikuta wanafanya mambo kama wanyama japokuwa ni binadamu. Mfano:

  • Unawakuta watu wako vijiweni au online tu kwenye mitandao ya kijamii kazi kutongozana ila haimletei mafanikio yeyote anajificha kwenye mahusiano na watu wengi akidhania maisha yake yanasonga mbele kumbe hana mbele wala nyuma.
  • Unakuta wanafanya mapenzi kwa njia ya haja kubwa, natoa rai kwa watoto wa kike huyo mwanaume anayekutongoza kwanza mulize una kitanda? Chumba? Unajikuta mnapotezewa mda sana muda ambao huwezi kuurudisha tena. Kama anakupenda aje kwenu akupende mbele ya wazazi wako
  • Unakuta watu kila wanapoenda wanaleta maugomvi, matabaka, chuki na mizizi ya fitina kwa wenzao. Kazi yao kubomoa maisha ya wenzao
  • Wanakimbia familia zao, unakuta hana ujasiri wa kuongoza familia. Mfano kwa mwanaume sifa kubwa unayopata ni pale watoto wanaposhindana kwenda chooni. Mwanamke sifa yake ni pale familia inaposimama katika maadili
  • Wanajivunia vitu vya msingi kama umalaya, unakuta kazi yao ni kushinda kwenye porn au kushadadia mambo ambayo yanakuwa ya ngono mda wote. Ukimuliza sifa yake kubwa anakujibu nilitembea na Malaya Fulani.
  • NK
Watu wadhani technology ndio itawapa jawabau kila kitu mtu unataka ku google, ukitaka kuoa lazima ugoogle: mwanamke mzuri wa kuoa. Mavi yakishindwa kutoka unauliza google: Kwa nini leo mchonyo hautoi mavi?. Ukitaka kutatua matatizo unadhani google ndio jibu wakati watu wamezungukwa na wenye experience.

Natoa fundisho kubwa sana kwa vijana wenzangu jitahidini kujifunza kutokana na makosa ya wengine sio makosa yako mwenyewe maana kuna makosa ukiyafanya huwezi kurudi nyuma (to undo what happened). Ushauri usiyakubali maisha ya Isana, wenzako wanaishi usikubali kusindikiza, uwe na faida kwenye jamii na maisha yako yawe na maana na sio kutumia oxygen bure. .
 
Kuna watu wanauliza alafu unakuta wana majibu yao mfukoni. Katika maisha unatakiwa uweke upeo wa kujifunza, tena unaweza kujifunza kwa yule ambaye hukutegemea kabisa. Ukitaka kuuliza usiulize kwa kutaka kubishana uliza kwa kutaka kujifunza. .

Hapa sijamwandikia mtu mie nimetoa elimu kwa vijana wenzangu, sijandika ili kumsema mtu kwa hiyo kama umeamka au umeshinda vibaya hasira zako nenda katafute pesa sio kuhangaika na mimi. Sipendi na sina mda wa kukwazana na watu wasiojielewa. .

Kuna watu wanapenda kuwafanya wenzao wajisikie vibaya sana wakati maisha yao hayana cha maana. Ukiona mtu anakazania kumfanya mwenzake awe chini au kumdhalilisha ili yeye ajisikie yuko juu au ajione yuko duniani huko basi maisha yake mabovu sana. Hata humu JF kuna watu kazi zao kuwashambulia wenzao ili tu waonekane mbele za watu kuwa wao pia ni watu.
 
Nikweli linakua punguani au mtazamo wa chui mama au ni story za kitaa
 
Nikweli linakua punguani au mtazamo wa chui mama au ni story za kitaa

Kila nililolieleza ni kweli kabisa
Wtakuja watu wanaojua wataeleza nao
Hii sio story ya kitaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom