Habari Zenu Wakuu. Mimi ni kijana wa miaka 22. Nilimaliza kidato cha nne mnamo
mwaka
2018. Mwaka
2019 nikajaribu kuapply course ya Computer Science
DIT pale baada ya kupiga short
web development course kwenye college fulani hivi
(Kwa kipindi kile sikuwa na ufahamu kuhusu course za computer na sikuwa na mtu wa kunionesha njia kwahiyo sina uhakika kama nilitaka kuapply Computer Science au IT,etc ila nilikuwa tu interested na masomo ya technolojia
).
Kwa bahati mbaya nilikataliwa kujiunga na course hiyo sababu nilifeli somo la Chemisry kidato cha nne. Kwakweli hio sababu haikuniingia akilini ila nikasema sawa. Kipindi hiko pia nilikuwa niko interested na masuala ya Production. Niliweza kujifunza video production, graphics design pamoja na 3D animation kwa kutumia internet. Niliendeleza hii process mpaka mwaka jana
2021 baada ya kuwa na experince ya kutosheleza na kuwa comfortable kwenye production pipeline.
Niliona ndio muda sahihi wa kuanza kujifunza Computer Science
mtandaoni. Nikafatilia kazi mbali mbali za computer science na njia zake za masomo. Nikachagua language yangu ya kwanza ambayo ni
python. Nikakomaa nayo mwaka mzima nikafanya na baadhi ya projects ndogo ndogo. Baada ya kuwa comfortable na python nikaingia kwenye
web development. Haikunichukua muda nikapiga
HTML, CSS na Javascript pia nikawa comfortable nazo nikafanya na baadhi ya front-end projects. Muda huu ninavyo andika huu uzi niko zangu napiga back end development ili niwe Full stack web developer na nina malengo ya kuongeza ujuzi zaidi.
Dhumuni la kuandika uzi huu ni kuomba ushauri kuhusu kurudi chuo kwa ajili ya
Degree au niendelee kuchapa vitu mtandaoni. Na kama ni kurudi chuo. Je itanibidi nianzie wapi ili niweze kupata angalau
barchelor's degree. Asanteni.