Ushauri kuhusu kupewa likizo bila ya malipo

sauda chaka

Member
Jan 18, 2017
52
16
Mi ni mtumishi wa uma nataka niombe likizo ya bila malipo kwa mwaka mmoja nikafanye kilimo cha umwagiliaji Iringa-Luwaha je inaruhusiwa kirahisi ruhusa hiyo na nani anauelewa wowote nà kilimo cha huko?Maana kazi za serikali tunapoteza muda mno nna mtaji wa sh.2milioni ntatoka kweli?Napenda sana ujasiriamali kuliko kazi nishaurini.
 
Wala hakuna haja ya kuomba likizo isiyokuwa na malipo maana wewe mwenyewe unasema hizi kazi za serikali tunapotezeana muda mno. Hapo acha kazi kabisa mkuu ukawe mkulima tu!!
 
Chukua likizo yako ya kawaida ya mwezi mmoja,"annual leave" nenda huko ukajaribu hicho kilimo au ukaone utaratibu wa kilimo kwenye hilo eneo ulilolichagua,

Ikiwa kama utafanikiwa kuanza hicho kilimo katika huo mwezi mmoja unaweza kutafuta msaidizi ili asimamie hilo shamba lako,ni vizuri zaidi ukamuweka mtu wa karibu yako,

Usiache kazi kwa kutegemea kufanya hicho kilimo ambacho bado hata hujakifanyia utafiti wowote, kumbuka mshika mawili moja humponyoka au mtaka yote hukosa yote,

Good luck.
 
Oooook sawa ndugu sante
 
Likizo bila Malipo ni rahisi kuipata ila ni ngumu kurudi kazini kijana,,kurudishwa lazima kuwe na bajeti iliyotengwa ya mshahara pia kuwa na nafasi ngumu zaidi kuwe na kibali cha katibu mkuu utumishi,,
 
Wala hakuna haja ya kuomba likizo isiyokuwa na malipo maana wewe mwenyewe unasema hizi kazi za serikali tunapotezeana muda mno. Hapo acha kazi kabisa mkuu ukawe mkulima tu!!
Si kwamba naacha kazi naomba likizo ya bila malipo kwa muda mfup
 
Kwenye serikali ya awamu hii vitu vingi vimevurugwa sana kutokana na kuongozwa na watu wenye akili fupi! Zamani ilikuwa rahisi sana hata kama utaomba ya miaka mitatu ulikuwa unapewa maana ni moja ya miongozo ya utumishi wa umma. Sasa hawa vichwa maji wameingia wakawa wamezuia hizo taratibu zote sasa hivi ukipewa likizo isiyokuwa na malipo kurudi mpaka usali sala zote ndo ukubaliwe, vinginevyo ndo utakuwa umejitoa kimtindo!
 
Inaonyesha unapenda zaidi kujiajiri kuliko kuajiriwa... mi nafikir jipange hata kama sio leo basi kesho fanya ukipendacho... uamuzi wa mambo hayo yanahitaji ujasiri wa pekee ukipenda kitu hata changamoto zake utaona kawaida
 
Hapo umenena ndugu mzee anatuvuruga mpaka hatuelewi picha hili litaishije nashukuru kwa ushauri
 
Inaonyesha unapenda zaidi kujiajiri kuliko kuajiriwa... mi nafikir jipange hata kama sio leo basi kesho fanya ukipendacho... uamuzi wa mambo hayo yanahitaji ujasiri wa pekee ukipenda kitu hata changamoto zake utaona kawaida
Serikalini hali mbaya japo wengi wanatamani kuingia bila kujijumlisha wafa maskini,nashuru hata hivyo
 
Back
Top Bottom