Ushauri kuhusu kupandikiza mmea wa chainizi (Chinese cabbage)

Ushauri kuhusu kupandikiza mmea wa chainizi (Chinese cabbage)

Acehood

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,700
Reaction score
2,904
Habari wakuu.
Naomba kujua kama ni sahihi kupandikiza mimea miwili ya chainizi kwa shimo Moja, endapo nitaweka mbolea nyingi zaidi ya sehemu niliyopandikiza mmea mmoja.
 
Habari wakuu.
Naomba kujua kama ni sahihi kupandikiza mimea miwili ya chainizi kwa shimo Moja, endapo nitaweka mbolea nyingi zaidi ya sehemu niliyopandikiza mmea mmoja.
kupandikiza miwili lengo lake ni ikishashika kama mche mmoja umekufa mwingine uendelee au yote ikishika utauondoa ule ambao hauna afya ubaki mmoja.

inatakiwa ubaki mche mmoja kwenye shimo ili ukikua upate nafasi ya kutosha.
 
Asante sana mkuu. Nadhani nitumie njia hii
 
Sidhani kama ni sahihi.. hata kama ni kwa bustani ya nyumbani. Ile mboga iko so weak kupatwa na wadudu, sipati picha vikikaribiana km vitaweza kumea vzuri.
Asante sana mkuu. Ni kwa ajili ya biashara napeleka mashuleni. Nadhani mche mmoja utakuwa vizuri kama ulivyosema
 
Siyo sahihi. Chainisi (Chinese cabbage) iwpo una mbolea ya kutosha hiyo mboga hustawi mno na kuwa na majani makubwa na marefu zaidi hivyo ukiiweka karibu karibu utaibana na haitasitawi kwa uzuri.

Iwapo utaachia nafasi kubwa tegemea shina moja tu litatosha kuchumwa majani ya matumizi ya nyumbani kwako kwa wastani wa majini6-8 hii yatatosha kabisa.

Tumia mbolea ya samadi zaidi kisha nujua ya kuku ku boost mimea kila baada ya michumo3-4 unaweka mbolea ya kuku.
 
Back
Top Bottom