stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 17,989
- 27,750
Mkuu TO2004 hebu tuchanganulie hiyo tofauti kati ya Subaru Forester na BMW kama alivyofanya hapo juu ChelseaBlue!
Last edited by a moderator:
chukua BMW kiongozi, ni gari nzuri sana na spea zake zipo za kutosha kariakoo pale huangaiki na ni bei nzuri. Service yake ya kawaida sana, oil filter 10,000/=, engine oil bei zile zile. Unawezalitumia hata mwaka halijakanyaga garage, ni mwendo wa service tu muda unapofika. Gari kama Benz na BMW ni magari magumu sana na pia appearance zake za kiExecutive, linapendezea kwa watu wa ofisini na kila mahali, imagine umegonga suti unaingia kwenye subaru na mwingine kala suti kazama kwenye BMW, yupi katokezea???
zipo Model nyingi za BMW 3-Series..
BMW E21 (19751983) 3 Series
BMW E30 (19831991) 3 Series
BMW E36 (19912000) 3 Series
BMW E46 (19992006) 3 Series
BMW E90 (20052011/EUR, 20062011/US) 3 Series saloon
BMW E91 (20052011/EUR, 20062011/US) 3 Series Touring (Sports Wagon)
BMW E92 (20072011) 3 Series Coupé
BMW E93 (20072013) 3 Series Convertible
BMW F30 (2012) 3 Series saloon
BMW F31 (2012) 3 Series Touring (Sports Wagon)
kwa Case yako nadhani unaongelea BMW 318i au 320i ambazo zinaangukia kundi la E46,, Asilimia kubwa ya hizo BMW zinatumia Automanual transmission yaani kama unapenda Manual utaendesha na kama Automatic utaendesha pia.
![]()
kama wewe ni mtu wa Sports kidogo, unataka kuPush the limits kidogo basi BMW pia linakufaa,, ni gari tulivu lisilo na mbwembwe "kama Simba alielala'' ila ukilifungua linafunguka vibaya sana,,Speedometer inasoma 250km/h kitu ambacho ni no match kwa hizo Subaru..
![]()
![]()
![]()
![]()
kwa upande wa bei hazijatofautiana sana. Kama unategemea kuImport, bei itakuwa ndogo ukilinganisha na kununua hapa TZ..Bei around 10 - 11Mil each,,
![]()
![]()
![]()
Naipenda sana hii gari, muonekano wake tuu.
sina uzoefu na magari maana ndo hii ya kwanza nataka ninunue
mazingira yangu ni barabara vumbi na mashimo ya hapa na pale
naombeni mnipe uzuri wake
ubaya/matatizo yake pia ntafurahi kuyapata.
ila kiukweli naipenda kutoka moyoni.
na je, ninunue yard(mwanza) ama niagize nje?
NB: najua kuna uzi kadhaa zihusianazo, naomba nami mnipe mawazo yenu bila kuchoka.
asanteni
Chelseablue katoa maelezo mazuri,mimi naongeza kidogo tu.....ukiendesha BMW unaonekana exec fulani,ukiendesha IMPREZA unaoneka BOY RACER.....
Dah, natamani nipate pesa mapema!!
ni kweli kabisa mkuu..siku zote magari yanayotoka ujeruman ni magumu sana
Umechanganua vizur sana, hakika umetuimpress wengi tuwe mafans wa hyo bmw.
chukua BMW kiongozi, ni gari nzuri sana na spea zake zipo za kutosha kariakoo pale huangaiki na ni bei nzuri. Service yake ya kawaida sana, oil filter 10,000/=, engine oil bei zile zile. Unawezalitumia hata mwaka halijakanyaga garage, ni mwendo wa service tu muda unapofika. Gari kama Benz na BMW ni magari magumu sana na pia appearance zake za kiExecutive, linapendezea kwa watu wa ofisini na kila mahali, imagine umegonga suti unaingia kwenye subaru na mwingine kala suti kazama kwenye BMW, yupi katokezea???
ukaamua kuIpimp kidogo, Xenon Headlights, Angel Eyes na 20" Alloy Rims..
Mkuu hivi kuna uwezekano wa kupata Xenon Headlights kwa gx100 cresta?
Hilo gari au takataka?lita 9.8 kwa Kilometre?lol kwa hiyo ukienda Arusha utahitaji pipa la mafuta uende nalo!
acha kutoa lugha za kijinga. Kila mtu ananunua gari kulingana na uwezo wake. Kama wewe uwezo zako ni gari za km 14 kwa lita usitukejeli wenye uwezo wa km 7.
Samahani mkuu hiyo oil filter ya 10,000 unapataga wapi maana kule ilala ni 40,000. bei ya kuweka ndio 10,000. Nadhani mimi hua naibiwa. ila jamani BMW ni gari nzuri sana. ukitaka raha yake safiria umbali mkubwa. speed 250kph
mafuta dar songea sio zaidi ya laki 2. nawashauri pia kuyajua magari yetu ili tuweze kufanya service ndogo ndogo.
hahahaaaHilo gari au takataka?lita 9.8 kwa Kilometre?lol kwa hiyo ukienda Arusha utahitaji pipa la mafuta uende nalo!
Unajitafutia matatizo. Opt for IST Or RUNX or ALlEX.
Nahitaji vw polo. Kama unayo weka hapa, mwaka 2005 kuendelea
Mkuu hzo lak 2 ni go and return au single route ?