Ushauri katika uingizaji wa kuingiza bidhaa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri katika uingizaji wa kuingiza bidhaa nchini

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Candid Scope, Feb 25, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naona jukwaa hili linazidi kupata umaarufu. Kwa ushauri tu kuna wajasirimali wengi tu wanaokusudia kuanzisha biashara, tatizo baadhi ya bidhaa upatikanaji wake huwa mgumu na pengine gharama na matatizo ya visa huwagharimu zaidi kwa kufikiria kila mmoja ajipange kivyake.

  Ushauri wangu ni bora kuwa na mshikamano kwa wafanyabiashara wadogo kadhaa kuwa katika vikundi kwa kufanya ushirikiano wa kuingiza bidhaa kwa pamoja. Tanzania ya leo si kama ya miaka 10 iliyopita, kuna wenye nafasi ya kupenda sehemu nyingi bila vikwazo, hivyo bora katika kundi kuwa na mmoja anayeaminika kuwa importer wa bidhaa. Tatizo hapa si kila mmoja wa kuaminiana, napengine ingefaa kuwa na mikataba inayowalinda wote.

  Njia hii ni nzuri kwani hata mwenye mtaji mdogo hata wa 1,000,000 anaweza kupata bidhaa zake na gharama za usafirishaji kwa pamoja huwa nafuu kuliko pengi kujipanga kivyake.

  Binafsi na mpango wa kuanza shughuli hii, napenda kupata vijana kadhaa ambao wana malengo kweli ya ujasirimali, ambao mitaji yao huanzia 3,000,000 and up, ambao biashara zao zinatokana na bidhaa za kutoka nje ya Tanzania. Kukusanya nguvu ya vijana kama watano hivi wa biashara ndogo kuna uwezo wa kuanza na container moja na likishafika kila mmoja anachukua chake.

  Lakini lazima kuwepo na utaratibu maalumu ambao utafanywa kimkataba. Uwezo wangu wa kuleta bidhaa ni kutoka Europe na USA. Ni pendekezo kwa wadau, kwani tukiunganisha nguvu ndio kufanikiwa kwetu.
   
 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Safi sana mkuu.

  Mwenyewe hapa nimepata kibali kuwa msambazaji wa Manukato kutoka kiwanda cha BI-ES Perfumes kwa kuanzia. Wana bidhaa zao nzuri sana na hasa kwa ajili ya watoto. Watu wazima na vijana pia bidhaa zao ni nzuri mno ukilinganisha na bei.

  http://www.bies.nazwa.pl/public_html/index.php

  Kwa watoto wana kibali/wanashirikiana na DISNEY katika kutengeneza bidhaa kwa ajili ya watoto. Hivyo, wana bidhaa kama Hanna Montana, High School Music:
  http://www.bies.nazwa.pl/public_html/index.php?show/grupa/13/

  Kwa sasa nimeshaanza ila katika scale ndogo maana na tatizo la fedha nalo hapo nyumbani, imekuwa kasheshe. Lengo hasa ni kuwa msambazaji kwa East Africa.

  Kama kutakuwa na watu wapo interested kununua kwangu moja kwa moja kama washiriki basi ntahakikisha kuwa kila bidhaa, yeye anapata faida zaidi kuliko mie. Mie faida yangu itakuja tu pale ambapo ntaanza kuuza katika kiwango kikubwa. Na kama kutakuwa na watu wameandikishana na mie mkataba na kuwa wanalipia mapema bidhaa zao, basi bei pia ntahakikisha inashuka zaidi.

  Hiki kiwanda, bidhaa zao wanazitengenezea Czech Republic na Poland. Hizi nchi ndiyo watengenezaji wakubwa wa bidhaa nyingi sana duniani hasa inapokuja kwenye manukato kama AVON, zinafyatuliwa hapa. Pia la muhimu zaidi ni kuwa yale mafuta ya Perfume (Concentrated Perfumes) yanatoka Ufaransa ambako ndipo nyumbani kwa manukato. Kama mtakavyosoma kwenye maelezo chini, mara nyingi hiyo Perfume inakuwa kama asilimia 2-15 tu. Ndiyo maana kuna nyingine unajipulizia baada ya masaa kadhaa zimepotea na nyingine zinadumu sana. Bidhaa zangu wengi wanasema kuwa wanakuwa nazo siku nzima hadi wanakwenda kuoga (EDP).

  Kwa wale watakaopendelea ushirikiano, basi tuwasiliane kwa email: SSAMBALI@hotmail.com

  Kwa wanaoanza, zijue terminology na mgawanyiko wa Perfumes duniani:


  These terms refer to the strength of the fragrance, or more specifically, to how much high grade alcohol and/or water that has been added to the fragrance oils. Parfum (generally the most concentrated form you can buy) has 15-25% perfume oil dissolved in alcohol. Any mixture with a lower proportion of oil to alcohol is known as an Eau.

  Eau Fraiche (Usually 3% or less perfume oil)
  Eau de cologne - EDC (2 - 5% perfume oil)
  Eau de toilette - EDT (4 - 10% perfume oil)
  Eau de parfum - EDP (8 - 15% perfume oil)
  Soie de Parfum (15 - 18% perfume oil)
  PARFUM (15 - 25% -- also sometimes referred to as Extract or Extrait)
  Perfume oil (15-30% perfume oil in an oil rather than alcohol base)

  You may also see the term Parfum de Toilette. Most companies use this term to describe a concentration that is either the same as Eau De Parfum, or between Eau De Parfum and Parfum.

  The 3 most common perfume fragrances you will purchase are:

  PARFUM - This is one of the strongest perfume fragrance available. This means that you need to use less and the fragrance will last much longer depending on skin type. Will last 6 to 8 hours.

  EAU DE PARFUM - EDP This is lighter than the Parfum and is less expensive, but still has long lasting fragrance smell. Will last from 3 to 5 hours.

  EAU DE TOILETTE - EDT This is a lighter fragrance and is therefore most used for the casual everyday use. It is less expensive than Eau de Parfum. Will lasts for 2 to 4 hours.

  FRAGRANCE TIPS:

  Spray a mist of your favorite fragrance scent on your hairbrush. The aroma will last for hours and make your hair smell wonderful!! Some people will even spray a few squirts of thier favorite fragrance directly into their shampoo and/or conditioner for a added fragrance smell.

  As we all know, fragrance scent rises, so for a longer last to your perfume smell, spray all your pulse points, from your ankles, behind the knee, wrist, inside your arm, neckline, ect.... Remember to FIRST put on your fragrance scented body lotion or body creme before your perfume, this will help ensure your smell will last hours longer and you will not need to use as much of your perfume :). So, if you get the gift set with all those added fragrance goodies, use them!!

  Thank you for reading this Guide, hope it has helped

  From: eBay Guides - What does EDT, EDP, EDC, etc.. mean PERFUME TIPS
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  heshima juu candid hili ni bonge la idea hofu yangu ni kwa wale ndugu zetu wa bandarini na mapato
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mkuu mimi nipo tayari kukuunga mkono. tafadhali nipelekee simu namba yako tulijadili.
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Hiii aidea ni nzuri sana, na si jmabo la kuishia kwenye kuiport tu, hata baishara za ndani inawezekana kabisa mkuu, mitaji yetu ni midogo sana na endapo watu wangeunganisha nguvu wangeweza kufanya mambo makubwa sana.

  Mfano
  - Vijana wenye fani mabalimbali wanaweza jiunga pamoja kama watano hivi na hata mtaji wa milioni 3,000,000 kila mmoja na wakafanya mambo makubwa.

  - Kuna weza kuwepo na mtalamu katika
  1. Uhasibu- akawa anadili na maswala ya fedha za kapuni

  2. Mtalamu wa masoko- akadili na mauzo ya biadhaa za kampuni

  3. Mtalaamu wa IT- Akadili na IT

  5. Mtalaamu wa rasilimali watu- Akadili na maswala ya kujairi na utawala kwa ujumla

  6. Mtalaamu wa sheria- Kadili na mikataba ya kampuni

  7. Engenear- akadili na mwaswala ya ujenzi kama kampuni ni ya ujenzi

  8. Mtalamu wa ugazi- Akadili na manunuzi na utunzaji wa vifaa vya kampuni

  Kwa kifupi kuna fani nyingi ila huo ni mfano wa hizo fani nyingi zinazo zinazo weza kuungana.

  Tatizo linakuja kwamba sisi watanzania tuna ubinafisi sana kila mtu anataka aonekane yeye mwenyewe asifiwe na ndugu zake yeye mwenyewe,

  - Ila bila kuunganisha mitaji kama jamaa anavyo sema hapo kwenye maada tutaishia kulalamika na hatutaweza kushindana na makampuni makubwa.

  Na hii ni katika baishara nyingi kama vile
  1. Kilimo
  2.Ufugaji
  3.Usafirishaji
  4,Ujenzi
  5. Utalii
  6. Madini
  KWA KUUNGANISHA MITAJI ITAWEZEKANA KABISA, ILA LAZIMA WAUNGANISHA MITAJI WAWE NA NIA MOJA, WAAMINIFU, WANAOPENDANA SANA, WANAOJUANA TABIA TANGIA ZAMANI,
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni kweli tatizo ni hapo, lakini tunatakiwa kutokuwa na hofu sana kwa vile vihunzi kadhaa tutafipitia hadi kufikia mafanikio. Kikundi hicho lazima kiratibiwe hadi serikalini kijulikane kama ni njia mbadala ya vijana kujiajiri kwani kwa njia moja au nyingine itakuwa imetoa mwanga kwa vijana wengine kujifunza. Papo kuisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakuunga mkono kwa hoja yako, kwani si kuingiza bidhaa za nje tu, ila kutafuta soko la bidhaa za nchini mwetu na kuziuza nchi za nje. Kuna mazao kadhaa ya biasharaka kama kahawa, pareto, chai nk hayajatangazwa kutosha huko nje, ni jukumu letu kuangalia pande zote mbili namna gani tunaweza kudeal biashara na walimwengu.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Napenda vijana wenye kujiamini kama wewe, na cha msingi kuaminiana, kujituma na kutokata tamaa, kwani mwanzo huwa mgumu, na hatima yatatimia ya mchumia juani kulia chini ya mwembe.

  Nipo nalifanyia kazi jambo hili na natarajia within two weeks nitaweka bayana kituo na namba za simu, maana mambo kama haya hayataki kufanyika barabarani au kwenye stand ya mabasi. Ila tuendelee kuchangia mawazo katika kipindi hiki. Kwani nimaona kudeal na mtu mmoja mmoja tu husumbua akili kwa vile hatuko katika mtazamo wa pamoja katika kufikia malengo, bora watu wenye kuwa kikundi chenye makusudia na malengo ya pamoja na kukusanya nguvu kujikwamua kiuchumi.
   
 9. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ni wazo zuri sana.

  Mimi niko kwenye mchakato wa kufungua biashara, nanitakuwa ninaagiza vitu kutoka Europe hasusani Germany na Bulgaria lakini itachukuwa muda, labda mwisho wa mwaka huu nitaunga bogi.
   
 10. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mimi nazani kinacho takiwa na vitendo na inahitajika itengenezwe chombo kitakacho kuwa kinawaunganisha Vijana wenye mawazo yanayo fanana
  MFANO:
  1. Agriculture- Hapa wenye ndoto na nia ya kuwekeza kwenye kilimo wanaweza kutana na kuona wataunganisha vipi nguvu zao na kuja na kampuni ya uhakika

  2. Ufugaji- Wanaotaka kufuga, iwe ng'ombe, kuku na kazalika wanaweza unganisha nguvu zao

  3. IT- wanaunganisha mitaji yao

  4. Transportation- Wanaunganisha nguvu
  5. Procesising- wanaunga

  Na nyingine nyingi sana, wakuu sisi huku ndo tumelala jaribu kupitia website ya African Report muone vijana wa nchi zingine za Africa wanavyo kuja na Aidea zilizo enda shule na wanatafuta watu wa kuingia nao ubia
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Good Idea, tunahitaji kuadilika kimtazama na kugundua njia mbadala za kujiajiri badala ya kubaki kuilalamikia serikali tu wakati elimu tunayo.

  Kuna wengine ambao ni wafanya kazi na wana ndoto za kuanzisha kitu fulani, nafasi ya kusafiri kutafuta bidhaa ni ngumu, njia hii inaweza kuwa mbadala napapo kujenga mtandao wa kusaidiana katika kuimarisha biashara.
   
 12. l

  lumbagengata Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa muungozo huu na hatua hizi twaweza timiza azma ya wazo hili,hebu jitahidi ndani ya wiki hizi ulizoahidi kutimiza azma hii, ili tuanze kujenga misingi chanya yenye mtizamo wa mbali kwa wazo hili mwanana. Nasubiri hiyo hatua ili tuanze kuchanganua. Nakutakie mafanikio mema ktk hatua hii ya awali.
   
Loading...