Wakuu nawaomba mnisamehe.. Naomba mnishauri,
Miaka sita iliyopita niliomba kazi ofisi ya serikali na kwa kuwa aliyekuwa mchumba wangu alikuwa rafiki wa mkurugenzi, haikuwa shida nikapata.
Nimeendelea kufanya kazi vizuri tu kwa miaka sita bila doa lolote.
Juzi nimeitwa kwa mkurugenzi mpya ananiambia vyeti vyangu sio halali.
Nimepewa wiki moja niwaletee vyeti original. Kusema kweli mimi sina hivyo vyeti kwani niliishia form two na mkurugenzi wa mwanzo analijua kwani yeye na Charles ndio walitafuta hiko cheti.
Nafikiria kuomba likizo isiyokuwa na malipo ili niweze kurudia mitihani ya form four.
Chondechonde, naomba mnishauri hii itawezekana? Je, kwa kuwa kazi naiweza hivi cheti kina umuhimu gani au ndio majungu yenyewe kwa kuwa nilikuwa namshabikia mgombea upinzani?
Please please nishaurini nifanyeje maana hali ngumu.Jamii itanionaje mimi mtaani mwanangu ataishije?