Ushauri wa jinsi ya kumfungulia mashtaka Mkurugenzi mkuu wa PSSSF kwa kushindwa kulipa mapunjo ya mafao

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,160
11,483
Ndugu wanajamvi,

Baba yangu ni mstaafu miaka 6 iliyopita. Wakati yuko kazini, mwajiri ambaye ni taasisi ya umma haikupeleka baadhi ya michango zaidi ya milioni 2. Ameandika barua ya kudai mapunjo na kufuatilia katika ofisi za PSSSF na kila akienda wanasema wanalifanyia kazi. PSSSF ikienda kwa mwajiri, mwajiri anamwambia waende hazina kwasababu mshahara ulikuwa unatoka hazina na michango ilikuwa inakatwa juu kwa juu na kupelekwa PSSSF na kwamba suala la mapunjo ya mwajiriwa halimuhusu! Alichokifanya Mwajiri ni kuandika barua kwenda hazina kumkumbusha alipe hayo mapunjo na nakala akapewa mstaafu na nakala nyingine akapewa PSSSF basi!

Sasa mstaafu kila akienda ni longolongo zisizoisha wakati mifuko ya hifadhi ya jamii ndo imepewa mamlaka kisheria kukusanya michango ya wanachama wake hata kuwapeleka mahakamani waajiri ambao wanakaidi! Sasa huu ni mwaka wa sita (6) hakuna maendeleo yanayotia matumaini kama huyu mstaafu atalipwa.

Najua kwa vile hapa JF kuna wataalam wa kila nyanja, nishauri huyu mstaafu afanyeje? Nilimshauri afungue kesi mahakamani kumshitaki mkurugenzi mkuu wa PSSSF kwa kushindwa kumbana mwajiri apeleke michango ya mstaafu kwasababu sheria inaitaka mifuko ndo ikusanye michango kwa ajiri ya mwajiriwa!

Naomba ushauri wenu nianzie wapi?
 
Ndugu wanajanvi! Baba yangu ni mstaafu miaka 6 iliyopita. Wakati yuko kazini, mwajiri ambaye ni tahasisi ya umma haikupeleka baadhi ya michango zaidi ya milioni 2. Ameandika barua ya kudai mapunjo na kufuatilia katika ofisi za PSSSF na kila akienda wanasema wanalifanyia kazi. PSSSF ikienda kwa mwajiri, mwajiri anamwambia waende Azina kwasababu mshahara ulikuwa unatoka Azina na michango ilikuwa inakatwa juu kwa juu na kupelekwa PSSSF na kwamba suala la mapunjo ya mwajiriwa halimuhusu! Alichokifanya Mwajiri ni kuandika barua kwenda Azina kumkumbusha alipe hayo mapunjo na nakala akapewa mstaafu na nakala nyingine akapewa PSSSF basi!
Sasa mstaafu kila akienda ni longolongo zisizoisha wakati mifuko ya hifadhi ya jamii ndo imepewa mamlaka kisheria kukusanya michango ya wanachama wake hata kuwapeleka mahakamani waajiri ambao wanakaidi! Sasa huu ni mwaka wa sita (6) hakuna maendeleo yanayotia matumaini kama huyu mstaafu atalipwa.
Najua kwa vile hapa jf kuna wataalam wa kila nyanja, nishauri huyu mstaafu afanyeje? Nilimshauri afungue kesi mahakamani kumshitaki mkurugenzi mkuu wa PSSSF kwa kushindwa kumbana mwajiri apeleke michango ya mstaafu kwasababu sheria inaitaka mifuko ndo ikusanye michango kwa ajiri ya mwajiriwa! Naomba ushauri wenu nianzie wapi?
Andaa pesa mawakili waingie kazini chap Kwa haraka
 
Hivi kwa vile madai yako wazi na viambatanisho vipo, na hata wakienda kwenye mfumo wa PSSSF nyaraka zoote za hizi danadana kati ya PSSSF makao makuu, PSSSF alikofungulia madai, na PSSSF katika mkoa wa mwajiri unaohusika na mafao wataona, akienda mwenyewe mahakamani kuna ubaya?
 
Back
Top Bottom