Ushauri: Huyu binti kumbe hajui kupika

Ushauri: Huyu binti kumbe hajui kupika

Mmmh kwanza una mpango wa kumuoa au wataka kumchezea tu? kama vipi usimpotezee muda wake kutokujua kupika sio sabab ya kumuacha mwanamke kama kweli unampenda, Au unataka wale wanaojua kupika lakini ni wasaliti??? anaweza akajifunza ndani ya miezi michache tu na akawa mpishi mzuri tu.
Nimekuelewa
 
Usimpige chini buana...mtaftie a place akajifunze...hata mimi am still learning hapa hapa home....sometimes hizi shule za boarding zinatuharbu dooh...tena ukikaa chuo campus za ndani ndo kabisaaa...kupika unasikia kwa wenzio tu...give her time mbona atakua expert tu very soon....
 
Mmmh kwanza una mpango wa kumuoa au wataka kumchezea tu? kama vipi usimpotezee muda wake kutokujua kupika sio sabab ya kumuacha mwanamke kama kweli unampenda, Au unataka wale wanaojua kupika lakini ni wasaliti??? anaweza akajifunza ndani ya miezi michache tu na akawa mpishi mzuri tu.
Wee Dada NAKUPENDA
 
Kesi za aina hii hazija wahi kuniboa.
Wangu nikienda kwake gheto nazama kwajiko, kisha nafyatua kile roho ya mimi inatamani kumeza. Na hata akikuja kwangu mwendo ni uleule napika kama kawaida, maana nilicho gundua kwa wadada wanapata wakati mgumu sana kwenye kuwapikia wanaume ambao wameishi wenyewe huku wakijipikia kwa muda mrefu.
Wanaume tulio ishi wenyewe kwa muda mrefu tunajua kila kinacho husu jikoni, hadi kuonja chumvi...
 
Kama mwenyewe ana bidii ya kupika na mnapendana, mfundishe taratibu. kama demu hataki kupika anataka mkale hotelini hiyo ni shida ila kama ana bidii ya kupika na ana vigezo vya kuwa mke yaan heshima n.k chukuwa huyo. kujua kupika ni sehemu ndogo sana kwa mke utamfundisha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mmenitanya niwaze hadi kuvuka mlicho kiandika
Mkuu unaweza kumpata mtu ubongo uko holiday, anasubiri ubongo wako ufikirie, umeona wapi samaki wanachemshwa, lakini unarudi na mfuko anauliza "hawa samaki ni kaange au nichemshe?"
 
Duh ugali una mshinda na hapo mpo kwenye mahusiano,ukimuoa si atakup tabu,sasa km ugali una mshinda vingine ataviweza,piga chini huyo atakutia aibu
 
Back
Top Bottom