Wakuu hivi juzi kati nimempata mchumba though hatujatambulishana kwa wazazi tumekua tukiibana kila mtu giza litakapomfikia analala kwa mwenzie.
Ngoja nije kwenye maada Nimekua nikila kwa mama Ntilie mda mrefu nikaamua ninunue bidhaa za vyakula ndani ili angalau akija Siku ya ijumaa aweze kupika na kweli alivyoona kila kitu kipo huyu binti alianza kupika taangu wiki iliyopita alipika wali umeshikana naona aliweka maji mengi sana nyama alizipika kwa mda mrefu imagine hata vipande vya nyama vyenyewe vilikua vinagawanyika kama Nyama iliyosagwa.
Kwa kweli niliona ni bahati mbaya japo ilikua Long dinner kwangu lakini weekend hii ndo nimegundua Kuwa kumbe hajui kupika totally alirudia kupika wali vile vile kwenye kula navunga nilivunga tuu kuonesha sijagundua chochote.
Leo kabla hajaondoka amepika ugali yaani unanata kwenye mkono haujaiva kabisa.
Nishaurini Jamii forum nataka nimpige chini huu ni mzigo kupika wali hata mimi sishindwi but huyu binti ambaye kamaliza chuo hivi karibuni inaonekana malezi yamemuharibu.