Wakuu kila siku tunakumbushana humu kuwa mchumba hasomeshwi iweje mkuu Amoxlin umshauri mwenzio akamlipie mchumba ada ya mapishi?
kama alishindwa kuelewa kupika kwa miaka yote aliyoishi kwao atawezaje kujua kwa muda wa miezi miwili?
Nyumbani ni shuleni ndiko tunakojifunza usafi, mapishi, tabia njema, kusameheana, kuhurumiana n.k.
kama shule ya nyumbani imemshinda ya ulimwenguni ataiweza kweli japo wanasema asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, ila kajaribu mkuu ataweza kujua kupika huyo mchumbako wa voda fasta.