Ushauri: Huyu binti kumbe hajui kupika

Ushauri: Huyu binti kumbe hajui kupika

Mmmh kwanza una mpango wa kumuoa au wataka kumchezea tu? kama vipi usimpotezee muda wake kutokujua kupika sio sabab ya kumuacha mwanamke kama kweli unampenda, Au unataka wale wanaojua kupika lakini ni wasaliti??? anaweza akajifunza ndani ya miezi michache tu na akawa mpishi mzuri tu.

Hivi nini maana ya 'kumchezea'? Kwa sababu mwanaume na mwanamke wakikutana uwanjani ni kama vile wote wanacheza mpira na sio mmoja kuwa mpira. Wote wanapigiana pasi mpaka magoli yanafungwa. Mfano mwingine, hivi mwichi na kinu au kijiko na kikombe cha chai au kibao cha kusukumia chapati na ule msukumio kipi kinamchezea mwezie? au vinachezeana? Au hakuna cha kumchezea mwenzie?
 
Nimesoma comments nimesikitishwa wadada/wanawake wanateteana sana kwa mtu anayejua kuchemsha maji tuu at least wanaume wametoa mawazo ya kiume.

Unatakiwa kumuuliza kama anajua kupika na kwao anapika. Unaweza kukuta kwao kumejaa ma-rice cooker, tosters, steamers, na kadha wa kadha. Huyo ungempa feedback ya ukweli lazima angeomba mafunzo tu. Halafu ukiangalia kwa kina ni kosa la nani? Uoni kama ni kosa la wazazi wake?

Wewe unatafuta tu sababu za kuingia mitini. Kama kujua kupika ndio kigezo chako kikubwa basi kaoe pale uliposema unaendaga kula! Natanguliza samahani!!
 
Wakuu hivi juzi kati nimempata mchumba though hatujatambulishana kwa wazazi tumekua tukiibana kila mtu giza litakapomfikia analala kwa mwenzie.

Ngoja nije kwenye maada Nimekua nikila kwa mama Ntilie mda mrefu nikaamua ninunue bidhaa za vyakula ndani ili angalau akija Siku ya ijumaa aweze kupika na kweli alivyoona kila kitu kipo huyu binti alianza kupika taangu wiki iliyopita alipika wali umeshikana naona aliweka maji mengi sana nyama alizipika kwa mda mrefu imagine hata vipande vya nyama vyenyewe vilikua vinagawanyika kama Nyama iliyosagwa.

Kwa kweli niliona ni bahati mbaya japo ilikua Long dinner kwangu lakini weekend hii ndo nimegundua Kuwa kumbe hajui kupika totally alirudia kupika wali vile vile kwenye kula navunga nilivunga tuu kuonesha sijagundua chochote.

Leo kabla hajaondoka amepika ugali yaani unanata kwenye mkono haujaiva kabisa.

Nishaurini Jamii forum nataka nimpige chini huu ni mzigo kupika wali hata mimi sishindwi but huyu binti ambaye kamaliza chuo hivi karibuni inaonekana malezi yamemuharibu.
Kama kweli wampenda uyo mwanadada kupika isiwe kikwazo cha upendo wenu.... Isitoshe suala la upishi ni jambo la kurekebishika tu... Unaweza mfundisha we mwenyew taratibu na kuelewa... Natumaini hata wewe binafsi hukuzaliwa na kujua kupika papo hapo.....
Ifike kipindi uone ni hali ya kawaida...
Chakuongezea niwatakie Mahusiano mema
 
Wakuu hivi juzi kati nimempata mchumba though hatujatambulishana kwa wazazi tumekua tukiibana kila mtu giza litakapomfikia analala kwa mwenzie.

Ngoja nije kwenye maada Nimekua nikila kwa mama Ntilie mda mrefu nikaamua ninunue bidhaa za vyakula ndani ili angalau akija Siku ya ijumaa aweze kupika na kweli alivyoona kila kitu kipo huyu binti alianza kupika taangu wiki iliyopita alipika wali umeshikana naona aliweka maji mengi sana nyama alizipika kwa mda mrefu imagine hata vipande vya nyama vyenyewe vilikua vinagawanyika kama Nyama iliyosagwa.

Kwa kweli niliona ni bahati mbaya japo ilikua Long dinner kwangu lakini weekend hii ndo nimegundua Kuwa kumbe hajui kupika totally alirudia kupika wali vile vile kwenye kula navunga nilivunga tuu kuonesha sijagundua chochote.

Leo kabla hajaondoka amepika ugali yaani unanata kwenye mkono haujaiva kabisa.

Nishaurini Jamii forum nataka nimpige chini huu ni mzigo kupika wali hata mimi sishindwi but huyu binti ambaye kamaliza chuo hivi karibuni inaonekana malezi yamemuharibu.
Yaani umuache kwa sababu hajui kupika! Kama umempenda kweli mfundishe, we siunajua! We kua nae jikoni upike aone tofauti. Akiwa mgumu kujifunza ukioa mpeleke shule ya mapishi. Ukimpeleka sa ivi anaeza akafaidi mapishi mwanaume mwenzako we ukabaki mdomo wazi.
 
Wadada wengi hasa watoto wa kishua huwa hawajui kupika cha msingi mpeleke tu chuo cha mapishi au mshauri aende mwenyewe kwafaida yake mwenyewe sio kwa faida yako
 
Mmmh kwanza una mpango wa kumuoa au wataka kumchezea tu? kama vipi usimpotezee muda wake kutokujua kupika sio sabab ya kumuacha mwanamke kama kweli unampenda, Au unataka wale wanaojua kupika lakini ni wasaliti??? anaweza akajifunza ndani ya miezi michache tu na akawa mpishi mzuri tu.
mbona rahisi tu. amshauri aende chuo cha mapishi kwa faida yake mwenyewe. uzuri kishagundua hajui kupika. mbona kitu cha kawaida tu hicho. je angepata asiejua kusoma?
 
Nilikutana na hiyo kitu wa baby wangu. Basi nilichofanya ni kuwa,nikiona kapika chakula cha ovyo, namwambia,hicho chakula mimi napendelea kipikwe hivi na naingia jikoni. Uzuri ni kuwa kwenye mapishi mimi ni kama nimesomea,najua kupika sana. Basi nakipika chakula vizuri kabisa na kwa jinsi kilivyo,atajilamba mpaka basi. Basi next time naanza kumuelekeza hatua kwa hatua namna ya kukipika mpaka aelewe. Wakati mwingine ni kusacrifice kwa ajili ya wale tunaowapenda, kupika ni kipengele kidogo sana kama unampenda mtu kwa dhati.
 
Unachotaka anakupa vizuri...?? Anakatikiana?? Ikiwa unaridhika hapo seals la kupika dogo sana ikiwa nawe unajua kupika
 
Kama kweli unampenda na bado mpo huru,huu ndio muda muafaka,mwambie ukweli,akikubali kuwa hajui mfundishe tu mkuu hakuna namna! Akileta kujuwa mpige chini
 
mbona rahisi tu. amshauri aende chuo cha mapishi kwa faida yake mwenyewe. uzuri kishagundua hajui kupika. mbona kitu cha kawaida tu hicho. je angepata asiejua kusoma?
ha ha ha ha ha yani wala usiseme, ila nimecheka.
 
ha ha ha ha ha yani wala usiseme, ila nimecheka.
Binti umecheka niniii? unajua vitu vingine ni aibu kuja kusema hapa. ushajua hajui kupika mshauri tu kwa upole na unyenyekevu.

Nenda kajifunze kupika kwa faida yako na familia yako.
Kumuacha utakua hujamtendea haki japo najaua hata huwezi kumuoa unapiga tu.
 
Mkuu kama ishu ya mapishi haina haja ya kupiga maana unaweza kutrain tu na mambo yakaenda pouwa tu.
 
Binti umecheka niniii? unajua vitu vingine ni aibu kuja kusema hapa. ushajua hajui kupika mshauri tu kwa upole na unyenyekevu.

Nenda kajifunze kupika kwa faida yako na familia yako.
Kumuacha utakua hujamtendea haki japo najaua hata huwezi kumuoa unapiga tu.
huu ndo ushauri wa kuchukua, amfundishe au ampelekea kwa wanaojua.
 
Jamani umuache mtu kisa hajui kupika au humpendi si umwambie baby hujui kupika vizuri na ww umesema unajua kupika wali si umfundshe mwambie Fanya hv Fanya vile...
 
Pale magomeni kuna sehemu wanafundisha mapishi. Vipindi vyao vinaoneshwa ch.10

Msalimie sana.

Wakuu kila siku tunakumbushana humu kuwa mchumba hasomeshwi iweje mkuu Amoxlin umshauri mwenzio akamlipie mchumba ada ya mapishi?

kama alishindwa kuelewa kupika kwa miaka yote aliyoishi kwao atawezaje kujua kwa muda wa miezi miwili?

Nyumbani ni shuleni ndiko tunakojifunza usafi, mapishi, tabia njema, kusameheana, kuhurumiana n.k.

kama shule ya nyumbani imemshinda ya ulimwenguni ataiweza kweli japo wanasema asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, ila kajaribu mkuu ataweza kujua kupika huyo mchumbako wa voda fasta.
 
Back
Top Bottom