Ushauri:Huku niendako ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri:Huku niendako ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ndebile, Nov 5, 2011.

 1. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  Elimu yangu ni ya kuunga kwa gundi:darasa la saba nilisoma huku nauza mandaazi ya mama J akinilipa ujira wa sh.250 (mwaka 1987) huku nikiwatunza wadogo zangu baada ya wazazi wetu kufariki. (kama unavyoina makete kwenye tv) nilipomaliza std 7 nikaingia mtaani ambapo kila kazi nilifanya.

  Miaka miwili mtaani niliokotwa na taasisi moja ya kusaidia watoto yatima ambapo nilipelekwa sekondari na kusoma hadi f2,taasisi hiyo ilikosa wafadhi nami ukawa mwisho wa kusoma! Nifupishe habari hii ikikugusa niPM....Hatimaye nilipata kozi flani inayohusiana na mambo ya afya na nimeajiliwa serikarini,mwaka juzi nilifanya mtihani wa kidato cha nne kama private candidate ambapo nilipata dv III,sitaki kuongeza chumvi kwenye habari hii ili nisaidiwe,nilijisomea bila mwalimu na kwa miezi saba tu(walimu waliyenisaidia ilikuwa ni kwenye practicle za biology,chemistry na physics)math niliweka namba tu kwenye paper. Kumbuka nimeajiliwa na majukumu ya familia(nina watoto wawili)

  Baada ya kukamilisha kusimamia ujenzi wa ka-kiabanda kangu ka kuishi nimeanza kujisomea bila mwalimu masomo ya A-Level, combination ninayochukua ni PCB,nina recources za kutosha japo sijawahi kuvaa suti lakini kwenye kununua vitabu sina ubahili. Nataka mwaka 2013 nifanye NECTA Je,nitamudu? Nishauli kama ulishawahi kuona kitu hiki,hata kama ni kunikatisha tamaa we sema tu
   
 2. H

  HAKIKISHAKAULI Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu asante kwa kutaka kujiongezea elimu kila kitu kinawezeka jitahidi kupata mwalimu hayo si masomo ya kukomaa peke yako
   
 3. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  asante mkuu,ila hakuna watu wanadengua kama walimu wa sayansi! Kwanza ni wachache pili dau lao...utamsikia...Organic chemistry topic 40,000. Alafu kazi zetu wengine hazina fixed time,mara asubuhi, ukiku au jioni..hata hivyo nitazingatia ushauri wako
   
 4. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hongera coz umepiga hatua kubwa tayari!
  Upo umuhimu wa kutafuta mtu wa kukuelekeza ita mwalimu japo sio lazima awe ameusomea, hii ni ili kuokoa muda!
  Biology ina mambo mengi sana japo inaeleweka tu kirahisi, suala ni kujua kipi usome kipi uache, na hapo ndo unakuja umuhimu wa mwelekezaji na na zaidi sana ni kuwa na sylabus! kingine ni kutafuta examination format ili kujua uzito wa kila topic kwenye mtihani hii ni muhimu sana!
  Physics inaeleweka japo inataka mwelekezaji muelewa sio aliyekariri coz kuna vitu ambavyo ukivielewa havitoki tena, ukikariri utasahau, na ukisahau utahitaji muda wa kuvipitia tena na utasahau tena na hiyo circle itaendelea... wakati muda hauko upande wako, naongelea 2013.
  Chemistry yenyewe kwa mgawanyo wake itataka muelekezaji kwenye Organic coz hata zile equations zina formula zake na inorganic ambayo ina vitu vichache kwa uwiano na mengine( nikitegemea mambo hayajabadilika sana siku hizi...). Physical chem ni formula na maths!
  Kikubwa ni kuwa na nia, ambayo unayo tayari....!
  Ila pia ni muhimu utambue kwamba kufaulu ni zaidi ya kununua vitabu na kuvisoma! na kwakuwa wewe ni mtu wa familia na majukum ni mengi, ni lazima usome vitu sahihi ili kuokoa muda!
  Nakutakia kila la kheri.
   
 5. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  asante Bob Lee Swagger!ushauri wako nimeunakili kwenye note book yangu hasa hapo kwenye bold,pia nashukuru kunitahadhalisha kwenye MUDA. Ninazo syllabus mpya ila nilikuwa sijuhi kuhusu exam.format,hivi ninaweza kuzipata kwenye bookshops? Leo hii naanza kutafuta mwelekezaji...Kweli humu jf ni kisima cha maarifa!
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Mkuu,hayo masomo ni noma,nakushauri utafute mtu wa kukusaidia,co ya kukomaa mwenyewe.
   
 7. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  Senetor walimu wengine ukiacha matatizo niliyoyataja hapo juu ni MAKALIMANI,yaani anatumia muda mwingi kutoa tafsiri english to kiswahini hawana mbinu za kukupa ili u-master somo husika,hata hivyo nitatafuta mwalimu hasa pale nitakapo kwama kabisa,naogopa hizo bra bra..asante mkuu
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  kwan we uko wapi ndugu?
   
 9. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  Nipo Mwanza...jijini
   
 10. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  asante,....wakati ninafundishwa practicles za o-level mwalimu wa chem aliniambia hivi: huwezi kusoma from what is chemistry to Soil chemistry bila mwalimu! Nilimwambia nabahatisha tu,...
   
 11. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  kuna mwalimu yuko pale bwiru boys,ni mzuri sana kwa chemistry.
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Kama umeweza kutoka 1-4 kwanini ushindwe 5-6?!. Uoga ni mchawi mkubwa wa maendeleo yako.

  Jitahidi upate mwalimu akuelekeze. Hiyo dhana ya kuwa waalimu ni wakalimani sio kweli, mbona hao hao ndio wanaofundisha shule na watoto wanafaulu vizuri.

  Nakutakia kila la kheri.
   
 13. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi hebu pitia thread yangu hii!
   
Loading...