Ushauri: Hapendwi na wasichana

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
Nina rafiki yangu kipenzi sana ambaye tumetoka nae mbali sana, huyu jamaa huwa analia na kuumia sana kwa tatizo kubwa moja, anadai kuwa hapendwi na wasichana lakini hajui ni kwanini.

Jamaa ni msafi sana, anatupia kama kawaida na pia ni handsome kiasi chake ila kinachomsibu ni kuwa jamaa ni bingwa wa kukataliwa na wasichana siku zote kila akirusha voko anachomolewa.

Ingawa ni mpole na hana shobo wala masifa ya kijinga, mimi nashidwa hata cha kumshauri.

Tafadhalini wakuu nisaidieni ushauri juu ya huyu jamaa yangu nini afanye ili kuondokana na tatizo hilo hasa ushauri wa kisaikolojia.
 
Acha kutupima akili manawake wamejaa kila sehemu ndyo akataliwe hata dada poa wamechomoa?hapana si kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom