USHAURI: Gia namba nne kukosa nguvu na brake kutokumata mpaka upump zaidi za mara moja

Gitifii

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
248
137
Wakuu wangu wa JF heshima mbele, nina Jambo nilikuwa naomba kuuliza kwa ushauri wa kitaalamu nikiamini jukwaa hili ni la manufaa na limesaidia watanzanzia wengi. Baada ya salamu naomba kuelezea tatizo langu, Nina gari ya Town Ace manual pick up, mpaka asubuhi ilikuwa vizuri tu bila shida, Ila mchana huu wakati narudi katika mihangaiko nimegundua gia namba nne inakosa nguvu na breki inakataa kukamata hata ukikanyaga mpaka mwisho inakuwa nyepesi sana na haishiki mpaka ukanyage zaidi ya mara moja, sijwahi kupata hii experience na imeniwia vigumu sana maana nilikuwa morogoro road na posta na kibamba na jumasosi njia inakuwa na malori mengi. Nimewiwa kutoa heshima kubwa JF ili kupata abcd za kitaalamu kabla sijaingia gereji zetu za mtaani ili hata nijue nashughulikia Nini. Heshima zaidi kwenu wadau nawasilisha kwa msaada.
 
Bro hilo goma peleka gereji mafundi wacheze nalo..... au unataka kulitengeneza mwenyewe ukishapata ushauri hapa..
 
Cheki mafuta ya breki mkuu, kwenye hilo la breki.
hilo la gia kukosa nguvu, inawezekana likachangiwa na mengi ila moja wapo ni uchafu kwenye oil filter au cabreta haifanyi kazi vizuri.

Vipi inakuwa na miss?
 
Hapana halimiss mkuu
 
Bro hilo goma peleka gereji mafundi wacheze nalo..... au unataka kulitengeneza mwenyewe ukishapata ushauri hapa..
Hapana sitaki kutengeneza mwenyewe mkuu Ila gareji zetu za mtaani walau ukipata abcd mafundi hawakuzingui sana
 
Back
Top Bottom