Ushauri gani unaoweza kumpa mtu anayeanza kujenga?

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,276
Reaction score
3,939
Habari Wakuu,

Nimeona niulize hili swali maana wengine bado tupo kwenye nyumba za kupanga mara wengine kwa wazazi lakini purukushani zinatufosi tuwaze au hata tayari tumejipata tunataka kuanza kujenga. Pia Naamini wapo ambao tayari wapo kwenye nyumba zao hivyo wana uzoefu sana katika masuala ya ujenzi.

Stori nyingi tunazozipata ni heka heka za kusimamia mafundi na kuogopa kupigwa gharama za vifaa na sasa mijadala imekuwa mingi kuhusu kuwa makini na umiliki kwenye hati.

Hivyo, unamshauri nini Mtu anayeanza kujenga?
 
1. Hakikisha kiwanja hakina mgogoro kuhusu umiliki wake.
2. Pata ushauri wa ramani lakini hakikisha inakua ni ramani inayokidhi mahitaji yako. Usijenge nyumba kwa ramani ya fundi au msanifu.

Nnachomaanisha, mwambie fundi/ mchora ramani mahitaji yako na vitu vya muhimu kama idadi ya vyumba, mpangilio, ukubwa na vitu vingine, kisha yeye akushauri na kuchora ramani kulingana na muongozo wako. Ni rahisi sana kuonyeshwa ramani ukaipenda na kukubali kwenda nauo lakini kumbe sio kitu ulichokihitaji. Inakua ni nyumba yako iliyojengwa kwa matakwa ya fundi.

3. Pata makadirio ya gharama za ujenzi kulingana na ramani yako kwa hatua zote nikimaanisha msingi, boma, lenta, kuezeka, na finishing. Itakusaidia sana hasa kama unajenga kwa awamu.

Mengine watakuja kuongezea wengine.
 
Asante sana Mkuu
 
Habari Wakuu,

Nimeona niulize hili swali maana wengine bado tupo kwenye nyumba za kupanga mara wengine kwa wazazi lakini purukushani zinatufosi tuwaze au hata tayari tumejipata tunataka kuanza kujenga. Pia Naamini wapo ambao tayari wapo kwenye nyumba zao hivyo wana uzoefu sana katika masuala ya ujenzi.

Stori nyingi tunazozipata ni heka heka za kusimamia mafundi na kuogopa kupigwa gharama za vifaa na sasmijadala imekuwa mingi kuhusu kuwa makini na umiliki kwenye hati.

Hivyo, unamshauri nini Mtu anayeanza kujenga?

1. Hakikisha una hela inayojenga hadi ulipokusudia tofauti na.hapo utajuta.kuzaliwa.

2 Usijenge jumba kuuubwa usiloweza.kulimudu utalia materials yapo juu sana.
 
Back
Top Bottom