Ushauri: Chadema jaribuni kumtumia Prof Lipumba kutengeneza Bajeti Mbadala.

kutokana na aibu iliyotufika kambi ya upinzani katika kikao cha bajeti kilichomalizika jana, kwa kutengeneza bajeti mbovu na isiyoeleweka, mpaka wabunge wa CCM kuifananisha na bajeti ya Harusi, hii inaonesha kuwa kambi ya upinzani bado hatujajipanga kuongoza serikali na ilhali kambi ya upinzani tunao wachumi wazuri mf. Prof Lipumba kulikuwa na ugumu gani kumshirikisha katika kuandaa Bajeti mbadala? au ndio ubinafsi ule ule unaofanywa na ccm dhidi ya kutowashirikisha wapinzani, Prof kahigi kalisema hili wakati akichangia, serikali inaona ugumu gani kumtumia Prof Lipumba? na upinzani nasi tunafanya yale yale, je? kwa hali hii watanzani tutapata Maendeleo?
Uroho wa madaraka, kupenda kukumbatia kila jukumu.
Mbaya zaidi mlionywa na wapinzani wenzenu na mkabisha.
Sasa mtazamo huu unawatia aibu, kutengeneza bajeti ya makorokocho!
 
licha ya chdm kutokua na uhusiano mzuri na cuf kwa ss, lkn lipumba asichafuliwe kiuwezo! siyo sahihi. maprofesa wengi wa chuo kikuu mlimani wanamkubali sn na wanamuita mara kwa mara kushauriana kuhusu mambo ya uchumi. kimataifa anakubalika sn! museveni alimtumia kwa miaka 2 na kweli uchumi wa uganda ni mzuri sn. nyerere alikiri kuwa ujamaa ulifeli. alipoona umaskini umekithiri akang'atuka! NYERERE AMEIFANYIA MENGI NCHI YETU. HANA MFANO! LKN MWENYEWE ALIKIRI KUWA KIUCHUMI ALIFANYA VIBAYA. mwinyi alishauriwa na lipumba kufuata mtindo awa soko huria na kuondoa vikwazo. uchumi ambao tunauona angalau unakua, chanzo chake ni mwinyi. tuache udini tunapochangia. JF NI HOME OF GREAT THINKERS! tusipotoshe sera ya JF. mkapa aliendeleza pale mwinyi alipoachia. na mkapa aliweka misingi mizuri ya uchumi licha ya matatizo ya hapa na pale.


kuhusu ubinafsi wa zitto siyo yeye peke yake. chdm kuna hali ya kuviziana kwa kutafuta sifa. watu 4 wanachuana sana kujijenga kama wao. zitto, mbowe, slaa na lissu. juzi lissu aliiokosoa bajeti kuwa haiitwi mbadala bali MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU BAJETI YA SERIKALI. mbowe akmuunga mkono. lilikua kombora kwa zitto. zitto hakuwa bungeni siku hiyo. nadhani hilo lilimkera sn. kama viongozi wa juu wa chdm wanapigana madongo hadharani, umoja utakuepo kweli! natabiri kuwa chdm kitayumba sana kabla ya mwishoni mwa 2013
Lipumba ni mwenyekiti wa taifa wa chama kilichounda serikali ya mseto na CCM huko Zanzibar. Kwa kuwa chama chake kina ushirikiano na CCM, na kwa kuwa bajeti ya serikali ndiyo inayotekelezwa, basi ashauriwe kuwasaidia washirika wake CCM kuaandaa bajeti itakayoleta unafuu kiuchumi kwa wananchi.
Kuhusu utabiri wako wa CDM kuyumba, hauko peke yako. Hata mzee Wasira katueleza hivyo juzi. Tusubiri tuone.
 
FJM

Kwa hiyo Prof Lipumba hawezi kutoa msaada wowote kwa Chadema? Wakati mwingine ukiangalia unaona hakuna tofauti kati ya Chadema na CCM wote wamejaa ubinafsi, uwezi kumtumia Lema au Sugu kwenye kuandaa bajeti ukamuacha Prof Lipumba.

Ila unaweza kumtumia PROFESA MAJIMAREFU na JOHN DAMIEN KOMBA kutengeneza bajeti kwa kutumia tunguri na mpangilio wa sauti ya kwanza mpaka ya nne kupanga BAJETI
 
Last edited by a moderator:
FJM

Kwa hiyo Prof Lipumba hawezi kutoa msaada wowote kwa Chadema? Wakati mwingine ukiangalia unaona hakuna tofauti kati ya Chadema na CCM wote wamejaa ubinafsi, uwezi kumtumia Lema au Sugu kwenye kuandaa bajeti ukamuacha Prof Lipumba.

Profesa Lipumba hawezi kutoa msaada kwa CHADEMA kwa sababu ya mtizamo tofauti. Pia ni sawa CDM(wanasiasa) pekee hawawezi kuandaa bajeti iliyo bora. Kazi ya kuandaa bajeti ni ya kitaalam unaozingatia matakwa ya kisiasa. Bajeti ya serikali inayoundwa na kuongozwa na CCM imeandaliwa na wataalam wa bajeti na mipango kwa kuzingatia matakwa ya CCM.

CDM kama chama cha siasa kinahitaji wataalam watakaoandaa bajeti kwa kuzingatia political interest ya CDM. Ni kweli CDM inawanachama wenye utaalam wa uchumi ambao wanaweza kuandaa bajeti. Lakini si kazi ya chama cha siasa kuandaa bajeti kama nilivyosema hapo juu. Ni kazi ya wataalam wanaoongozwa na utashi wa kisiasa wa chama kinaongoza dola. Siku CHADEMA kitakapopewa ridhaa ya kuongoza serikali kitawatumia wataalam waliopo kutengeneza bajeti inayotafsiri political interest za CDM.

Kuhusu uhodari wa Lipumba katika mambo ya uchumi, ni kweli yeye ni profesa wa uchumi; lakini uwezo wake haukusaidia Tanzania wakati wa utawala wa Mwinyi alipokuwa mshauri wa uchumi. Kama walivyosema wengine hata huko Uganda Lipumba hakuweza kutoa ushauri uliosaidia kunyanyua uchumi wa nchi hiyo. Kama kuna mtu ana ushahidi wa kazi ya Lipumba auweke hapa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom