Prof. Lipumba amkumbusha Rais Magufuli kiporo cha Katiba Mpya alipomkaribisha kusalimia. Jaji Mutungi amjibu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,834
2,000
Kwanza sielewi kiitifaki imekaaje pale mteule wa Rais anapoamua kujibu kwa niaba ya Rais pasipo kuagizwa tena Rais mwenyewe akiwepo mahali hapo.

Pili, Prof Lipumba alitoa ombi/ kumbusho na siyo swali kwamba ikimpendeza Rais Magufuli atuachie katiba mpya.

Tatu, Jaji Mutungi amemtaka Prof Lipumba ahakikishe wabunge wa upinzani hawasusii vikao vya bunge ili kutokwamisha utendaji wa bunge. Kwani wapinzani wako wangapi bungeni kwamba wakisusa shughuli za bunge zitasimama?

Leo niamini CCM iko kila kona kwakweli.

Maendeleo hayana vyama!

=============

Leo Rais Magufuli alikuwa kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya mahakama na alipomaliza hotuba yake alimkaribisha Profesa Ibrahimu Lipumba,Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) kusalimia, ifatayo ni sehemu ya salamu yake.

MAGUFULI: Mwenyekiti Lipumba, njoo usalimu hapa kidogo professa, tukae tu tumsikilize kidogo apige lugha, hatujamuona halafu amenenepa kweli baada ya uchaguzi. Mzee Lipumba njoo usalimu hapa angalau dakika moja tafadhali. Kwa ruhusa yako mheshimiwa Jaji mkuu naomba asalimu kidogo.

LIPUMBA: Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Jaji mkuu, itifaki imezingatiwa. Mimi nikialikwa na majaji lazima nifike, mahakama inaponialika siku ya sheria najitahidi kuja kwa sababu hujui IGP Sirro anaweza akakupeleka huko. Kwahiyo wakiwa wanakuonaona wanajua kabisa kwamba huyu ni mtu wetu.

Jaji mkuu ameeleza vizuri kazi ambayo Rais umeifanya ya kuweza kuisaidia mahakama kujenga miundombinu, nakumbuka ulipoingia madarakani 2016 palikuwa na tatizo ya bajeti ya maendeleo, kwenye siku ya mahakama ulipokwenda Dar es Salaam ukasema bajeti yote ya maendeleo ya mahakama naipitisha hapa na kwa mara ya kwanza fedha yote ya bajeti ya maendeleo wakaipata idara ya mahakama kama ilivyopangwa.

Ulipokuwa unatoa hotuba tarehe 20 Novemba 2015 ulisema kwamba pana kiporo kiliachwa cha kukamilishwa swala ambalo watanzania wengi walishiriki kutoa maoni yao ili iweze kupatikana katiba mpya, ukasema kwenye hotuba hiyo, hilo umelipokea na wewe utalitekeleza.

Na vilevile ulipokuwa unapokea ripoti ya tume ya uchaguzi 2016 ulisema kabisa kwamba, masuala yale ambayo yamo kwenye katiba iliopendekezwa na kama kuna watu wana maoni mengine, serikali yako iko wazi itapokea.

Kwahiyo mimi nashukuru kwa kusema kwamba vile viporo vyote ulivyovitoa ambavyo havijatekelezwa 2015 alivyovieleza katika, miaka hii mitano utavitekeleza.

Na natoa wito na nakuombea kwa Moyo wa dhati kabisa, mwenyezi Mungu akupe nguvu, hivi viporo vyote katika kipindi hiki uweze kuvitekeleza, unapomaliza kipindi chako watu watakaoweza kuyalinda mafanikio uliyoyaleta katika nchi yetu ni kuwa na Katiba inayotokana na mapendekezo ya wananchi wa Tanzania.

Natoa wito na kwa bahati wewe mwenyewe ulikuwa mjumbe wa Bunge maalum la Katiba na mama Samia ndio alikuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba, kuna wazee wazito kina Prof. Kabudi, huyu bado kijana lakini ndio walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Warioba, kuna vijana wako, Polepole ndio alikuwa mjumbe wa Tume ya katiba, kuna watu wamekuzunguka wajumbe, Naibu Spika tena tulikuwa nae kwenye kamati moja na yeye ndio aliongoza kamati ya Chuo Kikuu.

JAJI MUTUNGI: Mimi nimesimamishwa hapa kama Msajili wa Vyama vya Siasa, bila kigugumizi chochote naweza nikasema hata vyama vya siasa vimekuwa na imani kubwa na mahakama zetu ndio maana unaona kila nikitoa maamuzi wanakimbilia mahakama.

Ninachowaomba kama alivyosema mheshimiwa Rais, msitumie mahakama kwenda kupaki kesi za msajili ila mzidi kuonyesha imani yenu kwa mahakama, kitendo ambacho naomba tuwapigie tena makofi kwasababu vyama vya siasa mpaka kuiamini mahakama kuleta kesi zao kwako, mheshimiwa Jaji mkuu mahakama mnastahili kupigiwa makofi.

Kwasababu sikupewa nafasi kubwa ya kuhutubia, nirudi kwa ndugu yangu mwenyekiti wa chama cha CUF, mheshimiwa Rais nimesikia anakuomba kuhusiana na Katiba, nilijua lazima wanasiasa watakumbushia mambo ya katiba lakini naomba kumuambia mheshimiwa mwenyekiti akawaambie wenzanke ule mchezo wa kutokatoka kwenye mabunge kukwamisha shughuli ya haya masuala muhimu ya kitaifa basi wayapunguze, mwaka 2021 tuwe ni watu wenye uzalendo tukiwa na masuala ya kitaifa, mambo ya kuinuka inuka kutoka kwenye Bunge hayo tuyaache. asanteni sana.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,256
2,000
Kuna viongozi katika awamu hii wanajua kujipendekeza kwa raisi kuliko changudoa anavyojipendekeza mbele za wenzake mwanaume aondoke nae yeye!

Kuna wakati kujipendekeza kwao kunaleta hadi karaha, hakuna tofauti na changudoa kuwa anasema my Tigo is good.
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,644
2,000
Mambo ya Chama Dola

Mutungi anajaribu kuendelea kumuipress boss wake ili aendelee na nafasi yake.

Hata hivyo si unajua NEC ndiyo ilipewa mahela mengi kwa ajili ya Uchaguzi, zaidi ya 350B, kwahiyo Mzee anajaribu kujiweka upande wa Jumba jeupe ili CAG akikagua matumizi yake asimlipue.
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,945
2,000
Kwani na wewe umetumwa na nani hadi umjibie Jaji.Mutungi?
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,644
2,000
Bwashee huyu Mutungi hayuko NEC, yeye ni msajili wa vyama vya siasa!
Nilijua yuko kule, manake ukiondoa Wizara ya Ujenzi na Maji, hakuna Mtu kapewa hela nyingi kama yule wa NEC so I bet lazima awe na vimeo vya kutosha kwenye matumizi yake.

Bwashee kwani umechukua nafasi ya Msemaji wa Rais, these few days umekuwa Chato na Sasa Dodoma ukituhabarisha, congrats 😂😂
 

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,722
2,000
Huyo hata kumuita "jaji" ni kuiaibisha taasisi ya mahakama.

Angejifunza kwa majaji wenzake aone jinsi wanavyojibeba kwa composure ya hali ya juu kama yule Jaji wa Rufani mteule wa magufuli anaitwa Sivangilwa Mwangesi (kamishna wa maadili) — Jaji anajibeba kwa nidhamu na utulivu mpaka unasema kweli hiki ni chuma.

Licha ya kuwa ana nafasi ya kisiasa, as a retired judge, huwezi kuropoka hovyo hovyo kama mlevi.

Hata mwenzake wa Tume ya uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage, ambaye ana cheo cha kisiasa zaidi kuliko yeye, huwa hajibu kipumbavu namna hiyo!

Kajibu kienyeji sana kama mwendawazimu!

Sijui walimuokota wapi huyu mwanasiasa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom