Ushauri: Chadema jaribuni kumtumia Prof Lipumba kutengeneza Bajeti Mbadala.

Acha ujinga wewe, kma tz inao wachumi km lipumba, nchemba na wengineo tz isingekuwa maskin namna hii. Nchi ni ya tatu kwa umsiki dunian, halafu we mkigoma unaandika ujinga kuwa mna wachumi, wemesaidia nini tz?. Umaskin unazidi kuongezeka halafu unaandika ulimbwende humu. Acha hizo.

jamaa umechoka kweli unaweza kuongea juu ya lipumba ongea kwa mchemba lipumba hajakaa kwenye system alikuwa mshauri tuu. Watu kama profesa hawathaminiwi hapa tz wanathamani ulaya
 
Watu wengine akili kama ya panzi. Ulishaambiwa hakuna kitu kinachoitwa BAJETI MBADALA. Kilichopo ni maoni kuihusu bajeti ya serikali. Wabunge, wasomi, wananchi, vyama vya siasa n.k wanaweza kutoa maoni yao na mapendekezo. CUF pia wanaweza kutoa maoni yao. Kama ameshindwa kukiandalia chama chake atawezaje kuwaandalia wengine?

kuandikia chama chake kivipi?
 
Hakuna kitu kinachoitwa budget mbadala, tuna kitu kinaitwa maoni ya kambi ya upinzania. Tatizo CUF mmetusaliti mkaolewa na CCM. Tunamuhitaji lipumba, lakini hatuna tabia ya kuchemba.
 
FJM

Kwa hiyo Prof Lipumba hawezi kutoa msaada wowote kwa Chadema? Wakati mwingine ukiangalia unaona hakuna tofauti kati ya Chadema na CCM wote wamejaa ubinafsi, uwezi kumtumia Lema au Sugu kwenye kuandaa bajeti ukamuacha Prof Lipumba.

Mbona huwa anatoa msaada, na hajanyimwa kufanya hivyo.
 
acha ubinafsi hujui hiv juzi prof. ametoka marekani akiwa mwenyekiti kuwaongoza wenzake kwa ajili ya uchumi wa dunio au ufaham hilo
 
tatizo hatuwatumii kwa ubinafsi wa viongoz wetu na wakitoa mchango wao hauthaminiwi.hivyo tatizo ni viongozi na sio maprof.
 
FJM

Kwa hiyo Prof Lipumba hawezi kutoa msaada wowote kwa Chadema? Wakati mwingine ukiangalia unaona hakuna tofauti kati ya Chadema na CCM wote wamejaa ubinafsi, uwezi kumtumia Lema au Sugu kwenye kuandaa bajeti ukamuacha Prof Lipumba.

Kwani unatulazimisha? Wewe vipi wewe?

Huyo Lipumba mtumieni nyinyi wenye imani naye. Nani alikwambia bajeti iliandaliwa na sugu na lema? CHADEMA ina wasomi, wanasheria kwa wachumi. Si kila mmoja wao awe ni mpanda jukwaa ili wewe umtambue.

Tungeni ya CUF, na msisahau kuweka bajeti ya petrol ya kuchomea makanisa Zenj
 
FJM

Kwa hiyo Prof Lipumba hawezi kutoa msaada wowote kwa Chadema? Wakati mwingine ukiangalia unaona hakuna tofauti kati ya Chadema na CCM wote wamejaa ubinafsi, uwezi kumtumia Lema au Sugu kwenye kuandaa bajeti ukamuacha Prof Lipumba.
Ritz, ya CDM yanakuwasha nini? Ushauri wako wapatie ccm dhaifu.
 
kutokana na aibu iliyotufika kambi ya upinzani katika kikao cha bajeti kilichomalizika jana, kwa kutengeneza bajeti mbovu na isiyoeleweka, mpaka wabunge wa CCM kuifananisha na bajeti ya Harusi, hii inaonesha kuwa kambi ya upinzani bado hatujajipanga kuongoza serikali na ilhali kambi ya upinzani tunao wachumi wazuri mf. Prof Lipumba kulikuwa na ugumu gani kumshirikisha katika kuandaa Bajeti mbadala? au ndio ubinafsi ule ule unaofanywa na ccm dhidi ya kutowashirikisha wapinzani, Prof kahigi kalisema hili wakati akichangia, serikali inaona ugumu gani kumtumia Prof Lipumba? na upinzani nasi tunafanya yale yale, je? kwa hali hii watanzani tutapata Maendeleo?

Chama ni taasisi. Mbona ameshindwa kuijenga chama chake? Badala ya chama kukua ndiyo inazidi kupotea. Silly season!
 
quote_icon.png
makwesa

acha ubinafsi hujui hiv juzi prof. ametoka marekani akiwa mwenyekiti kuwaongoza wenzake kwa ajili ya uchumi wa dunio au ufaham hilo
Mie naona CCM ndio hawafahamu kama Lipumba katoka Marekani juzi kuwaongoza wachumi wa dunia, wangemtumia yeye, labda hawakumuona kama amerudi.
 
Lipumba hawezi kutusaidia cdm wakati kafu yake imefunga ndoa na magambaz

huu ni uj.nga mmejazwa kichwani na viongozi, mnashindwa kupambanua hata huu ni uongo na ukweli?. kwa hili la budget hamuwezi kukwepa ubinafsi wenu umetuletea aibu sisi ni lazima tuwaseme, sugu na mdee mbumbumbu washirikishwe kuandaa budget kweli embu acheni UTANI!!
 
FJM

Kwa hiyo Prof Lipumba hawezi kutoa msaada wowote kwa Chadema? Wakati mwingine ukiangalia unaona hakuna tofauti kati ya Chadema na CCM wote wamejaa ubinafsi, uwezi kumtumia Lema au Sugu kwenye kuandaa bajeti ukamuacha Prof Lipumba.

Lakini we huoni nivibaya kuchemba vitu vya watu. Mume wa watu kajikalia kimya, ungeomba rusa kwa mumewe kwanza. ua unaogopa kukatwa mkono.
 
licha ya chdm kutokua na uhusiano mzuri na cuf kwa ss, lkn lipumba asichafuliwe kiuwezo! siyo sahihi. maprofesa wengi wa chuo kikuu mlimani wanamkubali sn na wanamuita mara kwa mara kushauriana kuhusu mambo ya uchumi. kimataifa anakubalika sn! museveni alimtumia kwa miaka 2 na kweli uchumi wa uganda ni mzuri sn. nyerere alikiri kuwa ujamaa ulifeli. alipoona umaskini umekithiri akang'atuka! NYERERE AMEIFANYIA MENGI NCHI YETU. HANA MFANO! LKN MWENYEWE ALIKIRI KUWA KIUCHUMI ALIFANYA VIBAYA. mwinyi alishauriwa na lipumba kufuata mtindo awa soko huria na kuondoa vikwazo. uchumi ambao tunauona angalau unakua, chanzo chake ni mwinyi. tuache udini tunapochangia. JF NI HOME OF GREAT THINKERS! tusipotoshe sera ya JF. mkapa aliendeleza pale mwinyi alipoachia. na mkapa aliweka misingi mizuri ya uchumi licha ya matatizo ya hapa na pale.


kuhusu ubinafsi wa zitto siyo yeye peke yake. chdm kuna hali ya kuviziana kwa kutafuta sifa. watu 4 wanachuana sana kujijenga kama wao. zitto, mbowe, slaa na lissu. juzi lissu aliiokosoa bajeti kuwa haiitwi mbadala bali MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU BAJETI YA SERIKALI. mbowe akmuunga mkono. lilikua kombora kwa zitto. zitto hakuwa bungeni siku hiyo. nadhani hilo lilimkera sn. kama viongozi wa juu wa chdm wanapigana madongo hadharani, umoja utakuepo kweli! natabiri kuwa chdm kitayumba sana kabla ya mwishoni mwa 2013
 
tatizo hatuwatumii kwa ubinafsi wa viongoz wetu na wakitoa mchango wao hauthaminiwi.hivyo tatizo ni viongozi na sio maprof.

Mkuu nakuunga mkono 100%. Tatizo sio wachumi au wataalam kwa ujumla wake. Tatizo ni siasa kama wengi katika thread hii wanavyomwaga siasa. Prof Lipumba kwa mtu anayependa maudhui ya uchumi ni mchumi mahili sana. sikiliza uchambuzi wake kiuchumi na achana na masuala ya siasa. Wachumi wa kuheshimika waliowahi tokea nchi hii ni marehemu Prof. Rweyemamu na ndo huyu Haruna.

wachumi huwa wanakupa ushauri ambao ni empirical na ambao unatazama mbali - ni juu yako kuukubali au kuukataa - bahati mbaya wanasiasa wetu wengi huamua kuukataa. Mfano Prof Rweyemamu (Havard graduant) RIP alimshauri Nyerere irudishwe kodi ya kichwa na malipo ya elimu - mzanaki aligoma kata na kumshambulia prof kwenye mkutano wa hadhara kule Kigoma akidai hawezi kugeuka nyuma na kuwa mlima wa chumvi. Haikupita miaka mingi akarudisha kodi ya kichwa na kuibatiza "kodi ya maendeleo" na shule zikaanza kulipiwa toka msingi hadi chuo kikuu!!!. Prof Rweye. akajiondokea na badae mauti kumfika kule marekani. Mh. mtei vivyo hivyo yalimsibu ya prof Rweyemamu.

Huenda tuna wachumi wazuri nchi hii lakini hatuwatumii - acha hawa wanaotamba kwenye vyombo vya habari kuwa walifaulu kiwango cha "A".
 
nimeleta hoja tuchangie kwa kuwa ikiwa bajeti ya upinzani ingekuwa ni kishawishi tosha kwa wanainchi kuzidi kuamini wapinzani wana uwezo, Prof Lipumba hii ni taaluma yake na ameishazishauri hata nchi za ulaya, mf. sweden, Denmark na Finland na Dunia, mtu kama ana uwezo apewe sifa zake na apewe kazi azifanye, tuache ubinafsi, na huu ubinafsi ndio unaofanya Taifa hili lisisonge mbele.

Huyu mchumi wetu kazisaidia hizo nchi lini na kwenye nini?

Au hiyo ni mwaka huu, maana yake mwaka jana alienda kusaidia uchumi wa Marekani ulioanguka.....
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom