Ushauri boti za Azam

Scaramanga

JF-Expert Member
Aug 19, 2020
401
539
Kwanza kabisa niwapongeze kwa kuwa na usafiri mzuri na wa uhakika ila niwape ushauri kidogo.

Hata kama ni daraja la Economy tambueni kuna watoto, wazee na wanaohitaji msaada. Tiketi hata za basi siku hizi kuna namba ya siti ila kwenye boti zenu daraja la economy kiukweli mnakose. Boti inajaza kuliko uwezo imekuwa kama daladala watu mnalipa nauli unakuta hakuna nafasi mnasimama na mnakimbilia boti kama daladala za mbagala kweli Azam ndiyo tumefikia huku?

Inasikitisha sana kuona wazee na watoto wanaminywa ili watu waweze kuwahi siti. kwanini kusiwe na mpangilio kama nafasi ni 100 msiuze tiketi tena? mtu kalipa nauli unakuja msimamisha toka mwanzo wa safari hadi mwisho.

Watu wanagombania kuingia kwenye boti kweli ? Hebu tujirekebishe kwenye hili
 
Tumelipokea hili na litawasilishwa kwa mkurugenzi.

Ushauri: kuwe na seat walau 10 za watu wenye uhitaji maalumu kama ilivyo kwa mwendokasi
 
Mimi Nina muda Sasa sipandi Kilimanjaro za Azam,jaribu Hawa ZANZIBAR1/ZANFAST FERRIES,boti zao ni nzuri sana full ac,hakuna vurugu,stuff wao hawana maringo,halafu zina speed balaa,Azam akasome.
 
Back
Top Bottom