Ni ngumu sana kuhukumu kesi ambayo haujasikiliza pande zote mbili. Lakini kwa ushahidi wa kimazingira na maelezo tulinayo mpaka sasa na jinsi picha zinavyojionyesha inaonekana huyo mwenye nyumba nyeupe ana matatizo sana japo kuna watu wanajaribu kumtetea. Watu wa aina hiyo ukipakana nao wanapenda sana kuangalia muonekano wa mtu na kumdharau hasa akishatangulia kujenga anakuona wewe huna kitu kwa sababu unakuja "site" na kuondoka miaka na miaka kwa hiyo anazidisha nyumba akijua huna ujanja utamuuzia taka usitake. Kumbe masikini ya Mungu una mipango yako mingine kabisa labda kuja kujenga hapo mahali baada ya miaka hata 10. Viwanja vyenyewe hivi "20 x 20" mara nyingi tunanunua kipindi tunaanza anza kazi/biashara. Sasa tukija kupata hela kidogo tunatamani kiwanja hicho hicho yatokee mazingaombwe kiwe "40 X 40" lazima tu yatatukuta yaliyomkuta huyo mwenye nyumba nyeupe. Kitu cha msingi kipato kikiongezeka nenda kanunue shamba kabisa huko Kibaha, Mkuranga, Kisarawe, n.k. kuepuka aibu hiyo ya kuja kejengewa ukuta dirishani halafu picha zinazunguka kwenye mitandao yote ya kijamii dunia nzima.
Kikubwa kwenye maisha tufanye mambo yatakayotupa amani ya roho sasa hivi na hata baadae na kuangalia faida na hasara ya maamuzi tunayofanya sasa hivi kwani maisha yenyewe haya mafupi sana. Unaweza kukuta huyo jamaa mwenye nyumba nyeupe alijenga wakati huo ana uwezo/nafasi sasa mambo yamebadilika unaweza kukuta huo uwezo/nafasi tena hana. Maana yake hata kurekebisha nyumba yake kwa kuweka hata AC hawezi si atakufa na joto maana mjenga ukuta kashaliziba . Mbaya zaidi unakuta walijenga wazazi na wameshatangulia mbele za haki si unawaachia msala watoto wako ambao hauwahusu kabisa.