Ushauri: Ana mgogoro wa muda mrefu na jirani yake

Ushauri: Ana mgogoro wa muda mrefu na jirani yake

pangakali 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
239
Reaction score
221
Habari wana jamvi, jamaa amekua na mvutano wa muda mrefu na jiran yake juu ya mipaka yao ya viwanja. Kutokana na mvutano huo jamaa kaamua kujenga fensi mwisho wa kiwanja chake. Je ni sahihi kwa maamuzi haya kama inavyoonekana katika picha hizi?
IMG-20200718-WA0027~2.jpeg
IMG-20200718-WA0027~3.jpeg
IMG-20200718-WA0025~2.jpeg
IMG-20200718-WA0026.jpeg
 
Mkuu mimi naona yuko sahihi kuna Mabila ukipakana nao unaweza juta kununua sehemu ukasema bora upange dawa yao ni hiyo hakuna nyingine ...
Kuna wahaya hawa wakorofi sana ukipakana nao na bila kujenga fensi kila siku itakuwa mizozo na kupelekana serikali za mitaa ama mahakamani
 
Jamaayako ni mpuuzi na anaakili za kitoto kabisa.
Yaani jamaa yako amesahau kwamba huyo jirani ndio wataishi nae hapi kwa miaka mingi na watoto wao watacheza pamoja..
Mkuu hujakutana na majirani wakorofi huwa hawabebeki kila siku itakuwa kesi bila kuwakazia mtasumbuana sana ,
Sasa wakati mwingine namna ya kuizima shari ni kufanya shari zaidi
 
Mkuu hujakutana na majirani wakorofi huwa hawabebeki kila siku itakuwa kesi bila kuwakazia mtasumbuana sana ,
Sasa wakati mwingine namna ya kuizima shari ni kufanya shari zaidi
Ingekua ni Mimi, nadhani ningeacha walau mita mbili kutoka kwenye ukuta wa nyumba ya huyo jirani mkorofi na kisha ningeweka ukuta.
Mkuu, ubaya hua haulipwi kwa ubaya. Na kosa huwa halifutwi kwa kutenda kosa tena.
 
Ni kweli kiongozi ila kuna watu hawabebi kiongozi mie yashanikuta ,kila unavyojitahidi kuyafanya mambo kiiungwana na ustarabu wenzako hawajali hivyo wataendelea kukuchokoa ,
Sasa wakati mwingine unaona kama mbwai bora iwe mbai ,ila kama una moyo kama wako wakuendelea hivyo basi ni bora ,ila si vyema kumlaumu mtu anapofanya maamuzi magumu kama hayo maana huwezi jua msukumo gani amepata mpaka kufikia hivyo ...
Pana watu mkuu kama utaendelea kuwa nyonge basi utajikuta kila siku unadhurika
 
Back
Top Bottom