Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,479
- 40,120
Mdogo wangu ana umri wa kati sasa.Alipokuwa mdogo alidekezwa mno kiasi kufikia kuamini kama vile yeye ndo last born. Lakini baadaye wakaja wadogoze watatu fasta fasta na dogo aliendelea kudeka.
Alipomaliza darasa la Saba akisubiri matokeo aliingia katika vikundi rika na seems alishawishika kuonja mneli. Such days nilikuwa ndo nakaribia kumalizia kidato cha nne. Nilianza kuona mabadiliko ya kitabia kwa bwana mdogo, kila nikiongea na wazazi kuhusu hali hiyo walichukulia poa na kutochukua hatua yoyote ile.
Inasemekana alifanya ugomvi na wenzake wakamtandika vyema kisawasawa, na inasemekana walimpiga kichwani pia. Tokea wakati huo hadi leo amekuwa mtu wa kudata mara kwa mara. Hivi ninavyoongea ni zaidi ya miaka 18 tunauguza ndugu yetu ambaye anadata kila baada ya kipindi fulani.
Lakini kuanzia miaka ya hivi karibuni nimegundua kitu, huyu bwana mdogo ni kama vile hapendi kupona maana kila akidata anapokelewa hospitali na kuanzishiwa tiba na ushauri, lakini mara nyingi kama si mara zote amekuwa akipewa dawa na madokta huificha chini ya ulimi na anazuga kama ameimeza kisha akienda chooni anaitema. Hili amekuwa akijitamba nalo kila atokapo hospitali na amekuwa akipata nafuu hataki kabisa kusikia habari za dawa.
Sasa ninachoomba ushauri ni hiki, Kila akiugua huwa so aggressive kwa nduguze hususani mama, Baba alifariki miaka minne nyuma hivyo mama amekuwa akitaabika na dogo kwani kila mara akipandisha kudata humfanyia vurugu kubwa. Akiumwa huwa anaharibu mali za home hata majirani, Pia amekuwa anatembea na visu akitishia watu...
Je, nini kinaweza kusaidia kumuondoa katika tatizo hili maana ameishawahi kulazwa hata Mirembe kwa miezi sita lakni akitoka huwa analianzisha.Pili, mtu akiugua akili huwa anakuwa na chuki na nduguze au hali inakuwaje?
Nauliza haya maana kihistoria kwetu hatuna watu waliowahi kuwa nusu mwezi.
Naomba msaada pls