Ushauri: Amepewa talaka, afanyeje apewe mali zake?

interface

JF-Expert Member
Nov 3, 2016
221
178
Kuna dada yangu aliolewa na ameishi na mume wake kama miaka 6 hivi wamebahatika kupata watoto na wako na mali nyingi sana kwa kweli, sasa juzi kumetokea mgogoro kati yao juu ya mali.

Mume alimpigia simu make wake na akamuamuru mali zote ampe mtoto wake (wa mke mwengine) yule dada akatoa mali nyingi kumpa lakini baadae akaone haelewi kuna mali kidogo akazuia baada ya kuzuia ikamsababishia talaka tatu na kumwambia toka hapo haraka sana, mke akatoka na hakutoa kitu kwa siku ile.

Jana ameenda na kukuta nyumba wamevunja vitasa vyote na kuweka vipya (watoto wa mambo hao na mama yao) mume mpaka leo hajulikani alipo na hana mawasiliano.

Ushauri wenu nini afanye huyu mwanamke kupata vitu vyake vilivyokuwemo ndani? Na juu ya hudumu za watoto?

Tafadhalini sana
 
Lipo kisheria zaid.

Kwa kuwa alishaolewa (ina mana cheti cha ndoa kipo)

Ameshazaa na huyu muhusika,

Very simple, hapo tafuteni wakili wa kuaminikia mkafungue jalada mahakamani kila mtu apewe chake, mkizubaa imekula kwenu.

Mkileta stori za mambo ya padri/sheikh itakua hamna jipya.
 
Asanteni sana kwa ushauri wenu.sasa uyo mume hayupo na Hanna mawasiliano sasa VP hapo ?mahakama inaweza kupitisha uwamuzi?sababu mlalamikiwa hayupo..
 
Kuna dada yangu aliolewa na ameishi na mume wake kama miaka 6 hivi wamebahatika kupata watoto na wako na mali nyingi sana kwa kweli, sasa juzi kumetokea mgogoro kati yao juu ya mali.

Mume alimpigia simu make wake na akamuamuru mali zote ampe mtoto wake (wa mke mwengine) yule dada akatoa mali nyingi kumpa lakini baadae akaone haelewi kuna mali kidogo akazuia baada ya kuzuia ikamsababishia talaka tatu na kumwambia toka hapo haraka sana, mke akatoka na hakutoa kitu kwa siku ile.

Jana ameenda na kukuta nyumba wamevunja vitasa vyote na kuweka vipya (watoto wa mambo hao na mama yao) mume mpaka leo hajulikani alipo na hana mawasiliano.

Ushauri wenu nini afanye huyu mwanamke kupata vitu vyake vilivyokuwemo ndani? Na juu ya hudumu za watoto?

Tafadhalini sana
katafute za kwako, wengi wenu, mnafikiri wanaume wanawachumia pesa!!
 
Ni jambo la kisheria. Lakini kwanza lazima ujue ndoa yako ilikuwa ya Kikristi, kiislamu au Kimila kwa maana kila dini ina namna inavyogawa mali. Waislamu wapo wazi na hakuna dhuluma sana ila mgao kwa mke ni kiduchu.
 
nenda ustawi wa jamiii......kumbuka cheti cha ndoa ni mali ya serikali....... na serikali ndio inayoweza kusimamia haki, achana na mambo ya dini au kimila......huko ni dhuluma tuu.......
 
umemjibu vzr ila ustawi wajamii nao ni kimeo kingine, bora angeenda kituo kikubwa cha polisi kwenye sehemu inaitwa DAWATI.

nahisi hii atasaidiwa kirahis zaidi.
 
hapana,,, ustawi ndo mahali salama kabisa,,,,, dawati wale ni wasuluhishi tuuu.......wakiona hamuelekei,.... wanawaambia muende ustawi wa jamii.....tena uzuri ni wanawake werevu,,,,, hapo hachomoi kabisa....wale ndo wanafile to court, na ndio watasimamia kila kitu to end....
 
ohooo na kama mmetengana more that 7 yrs ila mwanaume hataki kutoa talaka watu waende wapi.
 
ule usemi wa mume/ mke /mpenzi wako ndo atakuwa adui wako mkubwa kesho unadhiilika kwenye hali kama hii.
 
Aende tamwa, tawlae ama legal human rights center. Kuna ushauri wa bure wa kisheria kuhusiana na haya mambo
 
Kipimo chepesi cha ujinga wa wanawake wa kibongo haswa waliolewa wao wakiachika badala ya kuwaza wataanzaje life mpya wao huwaza mali za mtalaka,mali ya mtalaka utaitumia vbaya na itakudumaza akili...ww na rafiki yako wote hamna maana!
Kwa suala hili ata ikiwa no Dada yako haungekubali.A .alimuachisha kazi na akamuahidi kumlipa kila mwezi na ahadi kibao lkn hakutimiza hata moja
 
Nashkuru Leo nimefika sehemu mulizonishauri na nimeanza kupata mwanga mzuri juu ya hili .kesho nitaenda sekta za wanawake na watoto.nitaleta marejesho
 
Kipimo chepesi cha ujinga wa wanawake wa kibongo haswa waliolewa wao wakiachika badala ya kuwaza wataanzaje life mpya wao huwaza mali za mtalaka,mali ya mtalaka utaitumia vbaya na itakudumaza akili...ww na rafiki yako wote hamna maana!
Umri wako ni mdogo hujui lolote kuhusu ndoa, funga domo lako chafu au kapige mswaki.

Haya maneno unaweza kumwambia mama yako mzazi akiachwa na Baba'ko?
 
mmmh japo alikosea ila mama ake anahusika vp
 
Back
Top Bottom