Ushajiuliza! Oxygen ingekuwa kama LUKU?

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,743
5,480
Sijiui kama na wewe ulishawahi kujiuliza juu ya hili? Hivi hewa ya Oxygen ingekuwa inalipiwa na watumiaji kwa mtindo kama wa LUKU. Yaani tungekuwa na kitu kinaitwa LOKU (LIPIA OXYGEN KADIRI UNAVYOTUMIA) .

Hivi binadamu wangapi wangeweza kumudu gharama za kutumia hii hewa? Hata kama gharama yake ingekuwa ya chini kabisa bado kuna watu wangeshindwa kulipia kwa wakati, na wengine wangeshindwa kabisa kulipa.

Hivyo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hekima na busara zake kwa kufanya matumizi ya hii hewa kuwa bure. Tajiri, mfalme, maskini na hohehahe wote tunavuta hewa sawa
 
Wiki iliyoisha tu nilijiuliza hilo swala!.. nikauliza na komamanga fulani hata haikunijibu maana ilijua kabisa ingekuwa imeshaga kwenda na maji Kama ingekuwa hivyo..😂

Vitu vingi tu natural tumepewa vya bure hata chakula ila sisi tu ndo tunavifanya kuvipa gharama due to the system.. in natural gharama ya vitu inalipwa na nguvu pamoja na akili.. so niuwezo wako tu.
Kama ingekuwa hewa nayo niyakulipia nafikiri hata idadi ya watu duniani ingekuwa ni ndogo maana mzazi wa kuzaa watoto weengi hiyo gharama ya kuwapa hewa,chakula,malazi,mavazi na makazi bado na elimu si ni mtihani huo.. Sasa shughuli ingekuwaje kwa ng'ombe na wanyama wengine..😅

Jibu ni no hicho kitu hakitakiwi kutokea.
 
Back
Top Bottom