Ushairi

Ushairi

ORESTA TADEY

New Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
2
Reaction score
0
UKIMWITA MAMA ATAITIKA?

1 Kuna hii nasikia, ati mjomba ni mama
Hii ndio nashangaa, hivi nani alisema?
Kila nikifikiria, n'ona moyo waniuma
Hivi ukimwita mama, ya kweli ataitika?

2.Mama mzazi wa kike, kamusi imeeleza
Shida ni kwa kaka yake, waja wakajiongeza
Ni huzuni tusicheke, si kitu cha kupendeza
Hivi ukimwita mama , ya kweli ataitika?

3.Hii kwangu iko hasi, dhahiri nimekataa
Naona kama ni tusi, jumla na reja pia
Inanipa ukakasi, mdomoni kuongea
Hivi ukimwita mama, ya kweli ataitika?

4.Ameoa ana mke, awezaje kuwa mama?
Baba wa watoto wake, hata wao yawauma
Nye watoto wa dadake, muoneeni huruma
Hivi ukimwita mama, ya kweli ataitika?

5.Haneni kwa kinywa chake, wacha leo niwambie
Yeye sio mwanamke, semi zisiwazuzue
Mjomba ndo jina lake, heshimuni jinsie
Hivi ukimwita mama, ya kweli ataitika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom