R Kelly angemuiga Dully Sykes yasingemkuta haya

Eminem jr

JF-Expert Member
May 21, 2018
1,993
4,554
NIMETAZAMA mfululizo wa documentary ya “Surviving R Kelly” na nyingine kuhusu unyanyasaji wa kimapenzi wa R Kelly kwa wanawake hasa mabinti wadogo. Stori ni nyingi zenye kuumiza na kufundisha. Haziburudishi hata kidogo. Ngoja nianze na Jerhonda Pace. Ilikuwa mwaka 2008 Jerhonda akiwa na miaka 15, ndipo alipokutana na R Kelly.

Jerhonda na R Kelly walikutana kwenye viunga vya Mahakama ya Cook Count Circuit, Chicago, Illinois. R Kelly alikuwa na mashitaka ya kumfanyia unyama wa kingono mtoto wa miaka 14, jina lake ni Reshona Landfair, akamrekodi na video. Ni video chafu iliyojaa ukatili. Video ikaonwa na Sparkle, mwanamuziki aliyekuwa msaidizi wa R Kelly. Sparkle ni anti wa Reshona na ndiye alimtambulisha kwa R Kelly ili amkuze kimuziki.

Jerhonda alipojua kuhusu kesi hiyo, akawa anatoroka shule kwenda mahakamani ili amuone R Kelly. Na kweli alikutana naye, akapata namba ya simu na kilichofuata Jerhonda akawa anadanganya kuwa anakwenda kulala kwa rafiki yake, kumbe alikwenda kulala kwa R Kelly.

Mwisho Jerhonda akawa mateka wa kimapenzi. Alifungiwa chumbani, akawa hana mawasiliano na wazazi wake. Alilazimishwa kushiriki mapenzi ya watatu (three some). Yaani R Kelly, Jerhonda na binti mwingine mdogo. Jerhonda pia ameandika kitabu “A Life Beyond Abuse”, yaani maisha yaliyokubuhu manyanyaso. Ndani yake anaeleza kuwa haikuwa rahisi kutoroka nyumbani kwa R Kelly, mpaka siku moja iliyokuwa na “party”, akamdanganya staa huyo kuwa anakwenda kwa anko wake kuchukua nguo za kuvaa na angerudi. Alipoondoka ikawa kimoja.

Februari 18, 2003, R Kelly alitoa albamu yake ya tano “Chocolate Factory”. Wakati albamu hiyo inatoka, Jerhonda alikuwa na miaka 10. Jerhonda alivutiwa na muziki wa R Kelly, akaanza kumpenda. Siku zilivyosogea alitamani sana kumuona. Mwaka 2008, aliposikia R Kelly ana kesi Mahakama ya Cook County Circuit, alikwenda kumuona. Wakati Jerhonda akidata kwa R Kelly, tayari shutuma nyingi zilishatolewa kuwa anachezea watoto wa kike kimapenzi. Jerhonda aliziba masikio. Alimfikia R Kelly. Kilichompata kinaacha simulizi leo. Si hivyo tu, kupitia vyombo vya habari ndiyo Jerhonda alijua kuhusu uwepo wa kesi hiyo. Mrembo Lisa Van Allen, alitoa ushahidi mahakamani kuwa alishiriki na Reshona pamoja na R Kelly katika mapenzi ya watatu. Lisa alisema, wakati huo alikuwa na miaka 17.

Katika Surviving R Kelly, Lisa anasema kuwa akiwa mdogo alimpenda sana R Kelly na alidhani naye anampenda. Muda ulivyokwenda ndipo aligundua kuwa R Kelly hakumpenda, ila alipenda wasichana wadogo.

Mwanamuziki Aaliyah alifariki dunia Agosti 25, 2001. Simulizi kuhusu Aaliyah ni kuwa mwaka 1994, alipokuwa na miaka 15, alifunga ndoa na R Kelly, aliyekuwa na miaka 27. Mwaka 1995, wazazi wa Aaliyah waliivunjilia mbali ndoa hiyo, maana binti yao alikuwa mtoto. Wakati Jerhonda akichanganyikiwa kwa R Kelly kuanzia mwaka 2003, tayari stori za Aaliyah zilishazeeka kabisa.

Mwaka 1996, ilivuja taarifa ya Tiffany Hawkins ambaye yeye ni wa mwanzoni, kwani mwaka 1991, akiwa na miaka 15, alianza mapenzi na R Kelly na kuishiwa kufanyiwa ukatili wa kingono. Zilikuwepo stori nyingi sana, lakini Jerhonda hakuogopa. Alikuza shauku na R Kelly, mwisho yalimkuta kama ya wenzake.

Mwaka 2008, R Kelly aliposimama kizimbani kujibu mashitaka ya kumnyanyasa kingono mtoto Reshona, 14, ndani ya Bongo, ndiyo mwaka ambao Dully Sykes, alitoa ‘hit song’ yenye jina “Baby Candy”. Maudhui ya wimbo ni kuwa Candy alikuwa ni mtoto mdogo, lakini akawa anampenda sana Dully. Ndani ya wimbo huo, Dully anamwambia Candy asome kwanza, mambo ya mapenzi yatafuata baadaye akishakua. Ni wimbo wenye maana kubwa kwa anayopita R Kelly leo na maisha ya usupastaa kwa jumla. Nilizungumza na Dully kuhusu Baby Candy, akasema: “Ule wimbo ni kisa cha kweli. Kuna msichana jina lake Fatma, lakini akawa anajiita Baby Candy. Alikuwa ananipenda sana. Nikawa namkwepa kwa sababu ni mdogo. Pancho Latino (marehemu), alikiwa prodyuza wa studio ya Dhahabu Records, akashauri kisa cha Baby Candy tukifanye wimbo, ndiyo ikawa hivyo.”

Ujumbe gani unaupata baada ya ufafanuzi wa Dully? Maisha ya umaarufu yana changamoto nyingi. Huwezi kuyajua maisha ya watu maarufu kama wewe sio maarufu. Hivyo, unaweza kushangaa kwa nini Baby Candy alimganda Dully wakati ni mdogo, au kivipi watoto wa kike wamfukuzie R Kelly na kashfa zake.

Ukweli ni kuwa maisha ya usupastaa yana vishawishi vingi. Ulimwengu wa sasa wa mitandao ya kijamii, akaunti za masupastaa kwenye mitandao hujaa ujumbe wa warembo sehemu ya faragha (DM) au Facebook Messenger. Wamo akina mama kabisa, wake za watu, warembo wa umri wa kati na wengine ni watoto.

Unakuta masupastaa wengine ni vijana wadogo ambao wametokea kwenye maisha ya mbanano. Starehe nyingi walikuwa wanazisikia tu au kuzitolea udenda kwa watu. Sasa wanapopata usupastaa na kufukuziwa na warembo, wao huona ni fursa na kuwatumia kwa fujo, wakiwemo watoto. Hivi sasa inaelezwa waendesha bodaboda na bajaji wanawatumikisha kimapenzi wanafunzi wa kike. Wapo makondakta na watu wengine mbalimbali. Wanatumia udhaifu wa watoto kutojitambua, kuwanyanyasa na kuwaingiza kwenye mapenzi kabla ya umri. Imekuwa hatari kiasi kwamba mpaka watoto wa kiume wanalawitiwa. Wahuni hawatambui kuwa watoto hawajawa na uwezo mzuri wa kuchanganua mambo kwa akili zao. Mara nyingi huendeshwa na hisia. Mtoto akikuganda, mwambie kama Dully alivyomwambia Baby Candy. Watoto waachwe wasome na wakue bila manyanyaso ili waje kuwa watu bora.

Docuseries ya Surviving R Kelly inatuma lawama nyingi kwa wazazi. Kwa kutoa uhuru mkubwa kwa watoto wao, kuwaamini bila kufuatilia. Mwisho, yote hayo yanawekwa kwenye neno moja; uzembe!

Mfano, Aaliyah alipelekwa kwa R Kelly na mjomba wake, Barry Henkerson ambaye alikuwa prodyuza mwenzake kwenye studio za Chicago Music Company. Barry alimfahamu vizuri R Kelly, lakini alimwacha awe jirani na Aaliyah na matokeo yake yakashuhudiwa makubwa ya R Kelly kumuoa Aaliyah aliyekuwa na miaka 15 tu.

Sparkle alifanya kazi na R Kelly tangu miaka ya 1990. Alikuwa ‘back vocalist’ wake, vilevile aliingiza sauti katika nyimbo za R Kelly. Hata albamu ya Age Ain’t Nothing but a Number, Sparkle amejaza sauti karibu nyimbo zote. Sparkle pia alishirikiana na R Kelly katika “Be Careful”, ambayo ni bonge la hit. Hivyo, Sparkle anamjua vizuri R Kelly, lakini akakubali kumkabidhi Reshona.

Jerhonda stori yake ni jinsi wazazi wake walivyomwamini na kumpa uhuru. Joycelyn anatamani kuwa mwanamuziki. Wazazi wa Joycelyn wapo vizuri kimaisha. Jumba la kifahari, magari makali. Hawana njaa. Walipoona mtoto wao kipaji chake ni muziki, waliamua kumtafuta R Kelly ili amsaidie mtoto wao kumuingiza kwenye lebo.

Tunarudi kulekule, wazazi wa Joycelyn walijua kila stori iliyokuwa inaendelea kuhusu R Kelly, lakini waliona uzushi, wakampeleka kwake. Mpaka leo wanaendelea na mapambano ya kumpata bila mafanikio. Mtoto kaganda kwa R Kelly. Inaumiza sana.

Nimefuatilia kesi karibu 25 za R Kelly kuwanyanyasa kimapenzi watoto wadogo. Mambo yenye kuzungumzwa ni yaleyale;

Mosi, R Kelly anawapiga wanawake. Mtalaka wa R Kelly, Andrea Lee, naye amelizungumza hili, kwamba ndiyo kisa cha kuomba talaka. Andrea na R Kelly waliachana mwaka 2009 wakiwa na watoto watatu.

Pili, R Kelly anawaambukiza magonjwa ya ngono watoto.

Tatu, watoto hawana hiari, kwani huwaamrisha kuliko kuwaomba. Akifika anasema vua na ukibisha unapigwa. Nne, ukishaingia kwa R Kelly anahakikisha huwasiliani na ndugu zako.

Tano, sheria ni kumwita R Kelly daddy (baba), ukimwita tofauti na hapo unachezea mkong’oto. Tuhuma dhidi ya R Kelly ni za muda mrefu, mbona haachi? Alishafikishwa mahakamani lakini akaachiwa huru kwa kukosekana ushahidi. Mbona hajifunzi? Hapo utaona kuwa R Kelly anahitaji msaada wa kisaikolojia. Ameshaathirika kwelikweli.

Historia inaonesha kuwa R Kelly alikulia kwenye nyumba ya wanawake watupu na alipokuwa mdogo alitumikishwa kimapenzi na mwanamke aliyekuwa mkubwa sana kwake. R Kelly alikuwa na rafiki wa kike aliyeitwa Lulu, waliyependana sana tangu akiwa na umri wa miaka nane. Lulu aliuawa akiwa mdogo na kumuumiza sana R Kelly. Lingine, R Kelly alipokuwa na umri wa miaka 11, alipigwa risasi ya bega. Mpaka leo risasi hiyo ipo mwilini. Je, haiwezi kuwa sababu ya tabia ya sasa?

Inakuwaje kijana aliyetoka kwenye umaskini mkubwa. Aliyelelewa na mama bila baba. Aliyeanza maisha ya muziki kwa kuimba kanisani, kisha mtaani, akiwaburudisha wasafiri wa treni za kampuni ya Chicago “L”, anapata mafanikio makubwa. Yupo juu ya ulimwengu. Tajiri, maarufu, anapendwa, lakini anaharibu sifa zote kwa tabia yake ya kunyanyasa wanawake hasa watoto?

R Kelly anahitaji msaada.
Akina R Kelly wapo wengi sana nchini. Wengine kwa sababu ya umaarufu au fedha, na kwa kuona ni kimbilio la wanawake wengi, basi wanawatumia, wanawanyanyasa kadiri wanavyojisikia. Tatizo wanawake huwa hawasemi mpaka wachushwe. Hata wanaosema kuhusu R Kelly sasa, ni baada ya kuchushwa
.
Chondechonde, watoto wadogo hapana. Waachwe wakaue bila kuathiriwa kisaikolojia. Kuwanyanyasa leo ni sababu ya kuwafanya wawe watu wa hovyo miaka ijayo. Nampenda R Kelly, ila naunga mkono kampeni ya “Mute R Kelly”, yenye maudhui ya kuuondoa muziki wa R Kelly kwenye mzunguko.

Celine Dione ameshauondoa wimbo “I’m Your Angel”, alioshirikiana naye. Lady Gaga kauondoa “Do What You Want” alioimba na R Kelly. Chance The Rapper kaiweka kando “Somewhere In Paradise” aliofanya na R Kelly pamoja na Jeremih. Docuseries ya Surviving R Kelly imekuja kuamsha harakati za kutaka mwanamuziki huyo achukuliwe hatua, baada ya kuona kila kesi mahakamani anashinda na kuonekana anasingiziwa, wakati kweli anaumiza watoto.

Mute R Kelly.
kwa ajili ya party na angerudi. Alipoondoka ikawa kimoja.
Februari 18, 2003, R Kelly alitoa albamu yake ya tano “Chocolate Factory”. Wakati albamu hiyo inatoka, Jerhonda alikuwa na umri wa miaka 10. Jerhonda alivutiwa na muziki wa R Kelly, akaanza kumpenda. Siku zilivyosogea alitamani sana kumuona. Mwaka 2008, aliposikia R Kelly ana kesi Mahakama ya Cook County Circuit, alikwenda kumuona.

Wakati Jerhonda akidata kwa R Kelly, tayari shutuma nyingi zilikuwa zimeshatolewa kumwandama mwanamuziki huyo kuwa anachezea watoto wa kike kimapenzi. Jerhonda aliziba masikio. Alimfikia R Kelly. Kilichompata kinaacha simulizi leo.

Si hivyo tu, kupitia vyombo vya habari ndiyo Jerhonda alijua kuhusu uwepo wa kesi hiyo. Mrembo Lisa Van Allen, alitoa ushahidi mahakamani kuwa alishiriki na Reshona pamoja na R Kelly katika mapenzi ya watatu. Lisa alisema, wakati huo alikuwa na umri wa miaka 17.

Katika Surviving R Kelly, Lisa anasema kuwa mwanzoni alipokuwa mdogo alimpenda sana R Kelly na alidhani naye anampenda. Muda ulivyokwenda ndipo aligundua kuwa R Kelly hakumpenda, ila alipenda wasichana wadogo.

Mwanamuziki Aaliyah alifariki dunia Agosti 25, 2001. Simulizi kuhusu Aaliyah ni kuwa mwaka 1994, alipokuwa na umri wa miaka 15, alifunga ndoa na R Kelly, aliyekuwa na umri wa miaka 27. Mwaka 1995, wazazi wa Aaliyah waliivunjilia mbali ndoa hiyo, maana binti yao alikuwa mtoto. Wakati Jerhonda akichanganyikiwa kwa R Kelly kuanzia mwaka 2003, tayari stori za Aaliyah zilishazeeka.

Mwaka 1996, ilivuja taarifa ya Tiffany Hawkins ambaye yeye ni wa mwanzoni, kwani mwaka 1991, akiwa na umri wa miaka 15, alianza mapenzi na R Kelly na kuishiwa kufanyiwa ukatili wa kingono. Zilikuwepo stori nyingi sana, lakini Jerhonda hakuogopa. Alikuza shauku ya kukutana na R Kelly, mwisho aliyakuta yaliyosimuliwa na watangulizi wake.

Mwaka 2008, R Kelly aliposimama kizimbani kujibu mashitaka ya kumnyanyasa kingono mtoto Reshona,14, ndani ya Bongo, ndiyo mwaka ambao Dully Sykes, alitoa ‘hit song’ yenye jina “Baby Candy”. Maudhui ya wimbo ni kuwa Candy alikuwa ni mtoto mdogo, lakini akawa anampenda sana Dully.

Ndani ya wimbo huo, Dully anamwambia Candy asome kwanza, mambo ya mapenzi yatafuata baadaye akishakua. Ni wimbo wenye maana kubwa kwa anayopita R Kelly leo na maisha ya usupastaa kwa jumla.

Nilizungumza na Dully kuhusu Baby Candy, akasema: “Ule wimbo ni kisa cha kweli kabisa. Kuna msichana jina lake Fatma, lakini akawa anajiita Baby Candy. Alikuwa ananipenda sana. Mimi nikawa namkwepa kwa sababu ni mdogo. Pancho Latino (marehemu), alipokuwa prodyuza wa studio yangu ya Dhahabu Records, akashauri kisa cha Baby Candy tukifanye wimbo, ndiyo ikawa hivyo.”

Ujumbe gani unaupata baada ya ufafanuzi wa Dully? Maisha ya umaarufu yana changamoto nyingi. Huwezi kuyajua maisha ya watu maarufu kama wewe siyo maarufu. Hivyo, inawezekana ukashangaa kwa nini Baby Candy alimganda Dully wakati ni mdogo, au kivipi watoto wa kike wamfukuzie R Kelly na kashfa zake.

Ukweli ni kuwa maisha ya usupastaa yana vishawishi vingi. Ulimwengu wa sasa wa mitandao ya kijamii, akaunti za masupastaa kwenye mitandao ya kijamii hujaa ujumbe wa warembo sehemu ya faragha (DM) au Facebook Messenger. Wamo akina mama kabisa, wake za watu, warembo wa umri wa kati na wengine ni watoto.

Unakuta masupastaa wengine ni vijana wadogo ambao wametokea kwenye maisha ya mbanano. Starehe nyingi walikuwa wanazisikia tu au kuzitolea udenda wanapoziona kwa watu. Sasa wanapopata usupastaa na kufukuziwa na warembo, wao huona ni fursa na kuwatumia kwa fujo, wakiwemo watoto chini ya umri wa miaka 18.

Leo hii jamii inaumizwa na watu wa kada mbalimbali. Hivi sasa inaelezwa waendesha bodaboda na bajaji wanawatumikisha kimapenzi wanafunzi wa kike. Wapo makondakta na watu wengine mbalimbali. Wanatumia udhaifu wa watoto kutojitambua, kuwanyanyasa na kuwaingiza kwenye mapenzi kabla ya umri.

Imekuwa hatari sana kiasi kwamba mpaka watoto wa kiume wanalawitiwa. Washenzi hawatambui kuwa watoto hawajawa na uwezo mzuri wa kuchanganua mambo kwa akili zao. Mara nyingi huendeshwa na hisia.

Ule msemo kuwa mtoto wa mwenzako ni wako vema kuushika. Usimfanyie kitu mtoto wa mwenzako ambacho wa kwako akifanyiwa utatamani ushike bunduki uue. Mtoto akikuganda, mwambie kama Dully alivyomwambia Baby Candy. Watoto waachwe wasome na wakue bila manyanyaso ili waje kuwa watu bora.

Docuseries ya Surviving R Kelly inatuma lawama nyingi kwa wazazi. Kwa kutoa uhuru mkubwa kwa watoto wao, kuwaamini bila kufuatilia, ni sababu ya watoto wao kuwa na watu ambao siyo wazuri. Mwisho, yote hayo yanawekwa kwenye neno moja; uzembe!

Mfano, Aaliyah alipelekwa kwa R Kelly na mjomba wake, Barry Henkerson ambaye alikuwa prodyuza mwenzake kwenye studio za Chicago Music Company. Barry alimfahamu vizuri R Kelly, lakini alimwacha awe jirani na Aaliyah na matokeo yake yakashuhudiwa makubwa ya R Kelly kumuoa Aaliyah aliyekuwa na umri wa miaka 15.

Sparkle alifanya kazi na R Kelly tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990. Alikuwa ‘back vocalist’ wake, vilevile Sparkle aliingiza sauti kwenye nyimbo ambazo R Kelly alizitengeneza akiwa prodyuza. Hata albamu ya Age Ain’t Nothing but a Number, Sparkle amejaza sauti karibu nyimbo zote. Sparkle pia alishirikiana na R Kelly katika “Be Careful”, ambayo ni bonge la hit.

Hivyo, Sparkle anamjua vizuri R Kelly, lakini akakubali kumkabidhi Reshona.

Jerhonda stori yake ni jinsi wazazi wake walivyokuwa wanamwamini na kumpa uhuru kupita kiasi. Alipowaambia anakwenda kwa rafiki yake, wakamkubalia bila kufuatilia, matokeo yake aliangukia kwenye mikono ya R Kelly. Labda ndiyo mnaita malezi ya Kizungu, mimi naita malezi ya uzezeta. Mtoto lazima alindwe mpaka akue.

Katika documentary ya BBC yenye jina, “Sex, Girls, STDs: R Kelly Sex Scandal”, wameguswa Lisa Van Allen, Faith Rogers, Kitti Jones na Joycelyn Savage. Hapa pia nisimulie kuhusu Joycelyn alivyonasa kwa R Kelly, akanogewa na kugoma kurejea kwa wazazi wake.

Joycelyn anatamani kuwa mwanamuziki. Wazazi wa Joycelyn wapo vizuri kimaisha. Jumba la kifahari Atlanta, wanaendesha magari ya bei mbaya. Hawana njaa. Walipoona mtoto wao kipaji chake ni muziki, waliamua kumtafuta R Kelly ili amsaidie mtoto wao kumuingiza kwenye lebo.

Baba wa Joycelyn, Tim Savage na mama yake, Jonjelyn Savage, walipata namba ya R Kelly ambaye alikubali kumpokea binti yao. Faith Rogers alipofanikiwa kuchomoka kwenye jengo la R Kelly, aliwatafuta wazazi wa Joycelyn na kuwaeleza kinachoendelea mjengoni kuwa mtoto wao anashiriki mapenzi ya kikundi na R Kelly.

Faith aliwaambia kuwa R Kelly ana maambukizi ya magonjwa ya ngono (STDs). Na alithibitisha hivyo kwa kuwa baada ya kutoroka, alipima na kukutwa na STDs.

Baada ya hapo, wazazi wa Joycelyn walitumia jitihada nyingi kumpata binti yao bila mafanikio. Mamlaka za usalama Marekani, wakiwemo FBI, ziliingia kati lakini Joycelyn mwenyewe akawa hataki kurudi kwa wazazi wake.

Tunarudi kulekule, wazazi wa Joycelyn walijua kila stori iliyokuwa inaendelea kuhusu R Kelly, lakini waliona uzushi, wakampeleka kwake. Mpaka leo wanaendelea na mapambano ya kumpata bila mafanikio. Mtoto kaganda kwa R Kelly.

Nimefuatilia kesi karibu 25 za R Kelly kuwanyanyasa kimapenzi watoto wadogo. Mambo yenye kuzungumzwa ni yaleyale; Mosi, R Kelly anawapiga wanawake. Mtalaka wa R Kelly, Andrea Lee, naye amelizungumza hili, kwamba ndiyo kisa cha kuomba talaka. Andrea na R Kelly waliachana mwaka 2009 wakiwa na watoto watatu.

Pili, R Kelly anawaambukiza magonjwa ya ngono watoto. Tatu, watoto hawana hiari, kwani huwaamrisha kuliko kuwaomba. Akifika anasema vua, geuka mbele, geuka nyuma, ukibisha unapigwa. Nne, ukishaingia kwa R Kelly anahakikisha huwasiliani na ndugu zako. Tano, sheria ni kumwita R Kelly daddy (baba), ukimwita tofauti na hapo unachezea mkong’oto.

Tuhuma dhidi ya R Kelly ni za muda mrefu, mbona haachi? Alishafikishwa mahakamani lakini akaachiwa huru kwa kukosekana ushahidi. Mbona hajifunzi? Hapo utaona kuwa R Kelly anahitaji msaada wa kisaikolojia. Ameshaathirika.

Historia inaonesha kuwa R Kelly alikulia kwenye nyumba ya wanawake watupu na alipokuwa mdogo alitumikishwa kimapenzi na mwanamke aliyekuwa mkubwa sana kwake. R Kelly alikuwa na rafiki wa kike aliyeitwa Lulu, waliyependana sana tangu akiwa na umri wa miaka nane. Lulu aliuawa akiwa mdogo na kumuumiza sana R Kelly. Lingine, R Kelly alipokuwa na umri wa miaka 11, alipigwa risasi ya bega. Mpaka leo risasi hiyo ipo mwilini. Je, haiwezi kuwa sababu ya tabia ya sasa?

Inakuwaje kijana aliyetoka kwenye umaskini mkubwa. Aliyelelewa na mama bila baba. Aliyeanza maisha ya muziki kwa kuimba kanisani, kisha mtaani, akiwaburudisha wasafiri wa treni za kampuni ya Chicago “L”, anapata mafanikio makubwa.

Yupo juu ya ulimwengu. Tajiri, maarufu, anapendwa, lakini anaharibu sifa zote kwa tabia yake ya kunyanyasa wanawake hasa watoto? R Kelly anahitaji msaada.

Akina R Kelly wapo wengi Tanzania. Wengine kwa sababu ya umaarufu au fedha, na kwa kuona ni kimbilio la wanawake wengi, basi wanawatumia, wanawanyanyasa kadiri wanavyojisikia. Tatizo wanawake huwa hawasemi mpaka wachushwe. Hata wanaosema kuhusu R Kelly sasa, ni baada ya kuchushwa.

Chondechonde, watoto wadogo hapana. Waachwe wakaue bila kuathiriwa kisaikolojia. Kuwanyanyasa leo ni sababu ya kuwafanya wawe watu wa hovyo miaka ijayo. Nampenda R Kelly, ila naunga mkono kampeni ya “Mute R Kelly”, yenye maudhui ya kuuondoa muziki wa R Kelly kwenye mzunguko.

Celine Dione ameshauondoa wimbo “I’m Your Angel”, alioshirikiana naye. Lady Gaga kauondoa “Do What You Want” alioimba na R Kelly. Chance The Rapper kaiweka kando “Somewhere In Paradise” aliofanya na R Kelly pamoja na Jeremih. Docuseries ya Surviving R Kelly imekuja kuamsha harakati za kutaka mwanamuziki huyo achukuliwe hatua, baada ya kuona kila kesi mahakamani anashinda na kuonekana anasingiziwa, wakati kweli anaumiza watoto.
 
Mtihani wa ngono ni mgumu sana, acha umjadili mwenzako tu lakini kama unakukuta mwenyewe mbele yako Duh !!!!!!! nihatari na ngumu kusalimika.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom