Ushahidi wa serikali yetu kufilisika huu hapa

Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia serikali ikikwama kuendesha shughuli zake kwa madai kuwa hakuna fedha. Shughuli zilizokwama ni pamoja na kutoajiri walimu waliohitimu mafunzo ya ualimu, kufanya maandalizi ya mtihani wa kidato cha pili na darasa la nne kwa wahusika kujitolea, kuendesha kesi, kuchelewesha mishahara kwa baadhi ya watumishi wake, nk,nk.

Swali la kujiuliza ni kwamba serikali imeshindwa kukusanya kodi au ni hujuma kwa Rais Kikwete kutoka kwa baadhi ya watendaji ili ionekane kwamba ameshindwa kuongoza nchi?

Jibu unalo mkubwa halafu unauliza nini??? Kama kuna watendaji wanao hujumu anasubiri nini kuwachukulia hatua??? Anawaogopa nini asiwatimue!!?? Hayo ndo matatizo ya uswahiba katika kazi za watu!!!!! Ni uzembe na ufisadi tu!!!.. Hakuna lolote!!!!...
 
Rais kikwete alianza kuhujumiwa sikua nyingi tangu 2008.Wanaomhujumu wamo serikalini na ktk chama chake.amekuwa akipewa taarifa za uongo hivyo kumpelekea kuonekana kituko kwa watz.Baada ya kuonekana anagusa mafisadi hapo hujuma ndo zilianza.Mafisadi wamekuwa wakitumia wapinzani kama vipaza sauti vyao kumkaba koo Kikwete,wamekua wakitoa siri za serikal kwa kushirikiana na maafisa wa serikali.jambo la maana ni kumuunga mkono RAIS wetu na sio kumkatisha tamaa kwa kumpinga kumbe anahujumiwa.ndg zangu vita dhidi ya rushwa ni vibaya sana kuliko ugonjwa wa ukimwi.
Dah.. Sasa kama amekuwa anapata wrong information,naye alitufundisha tuwe na akili kama Mbayuwayu..si ina maana he doesn't practice what he preaches..
 
Kikulacho ki nguoni mwako. Tusidanganyane kuna hujuma. Ni kukosa maarifa ndio kunatusumbua tunatoa jahazi tulilolipanda katikati ya bahari iliyochafuka. Tunategemea nini?
 
Hela zipo sana sema ni kwa ajili ya matumizi ya CCM tu,ni za kuzururia akina Nape pamoja na yeye mwenyewe.
 
Na hasa ukizingatia hawa wanaopambana nao wamejilimbikizia mali ajabu na wanatumia mali hizo kutekeleza ajenda zao, vita ni ngumu sana kwa Mh Raisi kiasi kwamba hata mfumo wa Usalama nao umeingiliwa, Mh Raisi amka toa kauli mambo yaende, najua itakuwa na gharama ila ni bora maana hali ni tete, hawa watu wanatumia ukimya wako kuburuza mambo wanavyotaka sasa hatujui lipi ni lipi
 
Dah serikali ni nini sijui? Ni mfumo mbaya tu ambao unamfanya Raisi aonekane ndio muamuzi wa kila kitu sio sera na taratibu... Nchi haitakiwi kuongozwa na raisi kama final designer inatakiwa iundwe in such a way kwamba hata kama Rais ana udhaifu wowote basi iende kama inavyotakiwa, mipango iliyopagwa ya kitaifa ya muda mrefu inakuwa ya kitaifa haiguswi, haiwi ya kisiasa au ya Rais kusema huyu akiondoka kila kitu kinabadilika, au aliyepita alikosea au sijui nini; No! inakuwa haimuhusu ni mipango ya muda mrefu ya kitaifa basi! Raisi anakuwa na maeneo yake ambayo yanamfanya atawale kwa kipindi chake akisimamia mipango hiyo bila kuiathiri na ile anayoona inafaaa kuiweka kwa kipindi hicho. Ni dhamana ya kuongoza akisimamia na kuweka yaliyo mema kwakuwa anapita tu. Muda wa miaka 10 ni michache kufanya Miracles from the scratch, hakuna, inatakiwa mfano misingi iliyojengwa na Mh Ben ingekuwa ni ya kitaifa siyo ya Ben, inalindwa kwa mfumo wa kisheria na taratibu na mfumo unakuwa unamnyima Raisi anaefuata kuibadili ovyo, mfano mipango ya kiuchumi wa kujitegemea ya muda mrefu, haitakiwi iguswe kabisa, na anayeingia hana nguvu ya kuigisa wala kuivuruga. Sasa shida ni kwamba anapobadilika raisi kila kitu kina change hii haifai kabisa kabisaaaa! Hii ingesaidia kupunguza hili la kusema sijui kodi haikuswanywi... ssijui nani alaumiwe sijui Rais kafanya au hajafanya hili... tungepambana nae kwenye sera za kijamii na kisiasa ambazo huwa zinaenda na wakati na zinaenda zikichange direction kila siku ila uchumi unabaki unalindwa na kuimarishwa ili usiathirike na siasa... an kama ni mabadiliko yawe to the advantage
 
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia serikali ikikwama kuendesha shughuli zake kwa madai kuwa hakuna fedha. Shughuli zilizokwama ni pamoja na kutoajiri walimu waliohitimu mafunzo ya ualimu, kufanya maandalizi ya mtihani wa kidato cha pili na darasa la nne kwa wahusika kujitolea, kuendesha kesi, kuchelewesha mishahara kwa baadhi ya watumishi wake, nk,nk.

Swali la kujiuliza ni kwamba serikali imeshindwa kukusanya kodi au ni hujuma kwa Rais Kikwete kutoka kwa baadhi ya watendaji ili ionekane kwamba ameshindwa kuongoza nchi?

Wacha kusingizia watendaji Fisadi papa anajihujumu mwenyewe.
 
Wacha kusingizia watendaji Fisadi papa anajihujumu mwenyewe.

Waambie Hao ...maana kuna watu wanatafuta sababu tu za kushindwa wakati ziko wazi..........mnategemea nchi itoe wapi pesa wakati viwanda havina umeme......
Wafanyabiashara wachache ambao angeweza kulipa kodi kabisa wanapewa misamaha ya kodi kwa Msaada wa ikulu.....au WaMa...ie home shopping..etc.....
Pesa itoke wapi wakati hata hiyo kidogo iliyopo inatumika kwa matumizi yasiyo ya lazima......
 
I paid the government Tsh. 12,500,000 in Tax just last week and I am a very small businessman in TZ, wanazolipa wafanyabiashara wakubwa zinaenda wapi. Wakubwa wanakula
 
kama imefikia hali hiyo basi Tanzania hali ni mbaya. Nalog off

Washawasha, napenda conclusion ya mawazo yako kila mara una log off alafu nakukuta sehemu nyingine. I like it. Angalia Mabasha wa UK au US wasikutembelee.
 
Hakuna hujuma,yeye na chama chake ndiyo wamefikia mwisho wa maarifa. Hawana maarifa mapya ya kusogeza nchi mbele.
 
Mfumo tulionao unamtegemea saana rais. Siitaji darubini kuona udhaifu wa tunaye muita rais, kwakua bado yupo tutazamie matatizo zaidi na huu ni mwanzo tu
 
kweli itafikia kipindi watu tutaichoka hii serikali,leo tarehe 5 novemba sijapata mshahara.ina maana nimeikopesha serikali? na kama nimeikopesha basi tuandikiane mkataba ili serikali inilipe na RIBA basi.mwezi uliopita nilipokea mshahara tarehe 9.leo hii tena hamna kitu.kuna nini huko kwenye siri kali? eti JK?
 
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia serikali ikikwama kuendesha shughuli zake kwa madai kuwa hakuna fedha. Shughuli zilizokwama ni pamoja na kutoajiri walimu waliohitimu mafunzo ya ualimu, kufanya maandalizi ya mtihani wa kidato cha pili na darasa la nne kwa wahusika kujitolea, kuendesha kesi, kuchelewesha mishahara kwa baadhi ya watumishi wake, nk,nk.

Swali la kujiuliza ni kwamba serikali imeshindwa kukusanya kodi au ni hujuma kwa Rais Kikwete kutoka kwa baadhi ya watendaji ili ionekane kwamba ameshindwa kuongoza nchi?
mkuu serikali ya JK imeongeza mahitaji zaidi ya 100% kuliko ilivyokuwa kwa mtangulizi wake. Jiulize leo kuna shule za sekondary ngapi na zinawanafunzi wangapi? unajua watu walioajiriwa ni wangapi mpaka leo. Kwa kifupi Serikali ya JK imeongeza vitu vingi sana vizuri ila imeshindwa kwenda sambamba na kuvihudumia. msijifanye vipofu.
 
Hamna kizuri hata kimoja alichoongeza zaidi ya shida. Kile unachokiona ndo kizuri toka serikali hii ni vile vitu vilivyofanywa kwa unafiki ili kuua vya wale waliotangulia. Unaikumbuka TASAF ilivyo fanya kzai nzuri wakati wa Ben? Lakini jamaa alipoingia akaipiga chini na sijui akaja na yakwake ambayo hatahaijulikani hata leo. Unajua ujenzi wa chuo cha Dodoma ulivyoharibu chuo kikuu cha UDSM? Watu mnashangilia eti watoto wetu wanansoma, kaulize elimu inayotolewa uDOM kama ni ya chuo kikikuu kweli! Chuo hiki hakitofautiani na zile secondary za kata maana kinalazimishwa tu kuwepo lakini uwezo wa kukihudumia kitoe elimu ya hadhi ya chuo kikuu hamna. Ngoja baada ya 2015 utaonana kama kitasimama. Hiki ni chuo cha kisiasa zaidi na mwisho wake ni 2015.
 
298300_235711069822806_100001517431958_656545_872221945_n.jpg

uvumilivu huu mpaka linii.............

Endeleeni kuchagua CCM, inawafaa!
 
Back
Top Bottom