Duh! Serikali yetu bana, sasa kipi kinatangulia salary slip au mshahara wenyewe??????? How do you pay someone kabla ya salary slip!!!! Hii yote ni dalili ya ubabaishaji!
Una utapiamlo wewe!!!!!Nadhani haukuelewa ,taatizo halikuwa pesa , inaonekana kulikuwa na makosa yawezekana katika mfumo wa Compyuta na vitu kama hivyo usipotoshe watu. Kati ya Serikali ambayo imejitahidi kujali watu wake na hasa suala a kuwahisha mishahara.
Kwani hiyo nembo ya Halmashauri hujaiona? We wa wapi bwana?hakuna muhuri wala msikubaliiii wakuuuu ,na poleni kwa yaliyowapata.....
Louis Ottaru,
Ni vugu kuelewa ni vipi serikali imefulia kama ufuatilii kwa umakini kile alichokisema Zitto last time kuhusu serikali kukopa pesa zaidi ya US$ 700 Million (kama sikosei) kutoka Stanbic Bank kwa ajili ya kulipa mishahara.
Hata hivyo, kwa wenzetu ambao hamfanyi kazi serikalini nadhani ni vugumu pia kuoanisha ushahidi huu na yale yanayoendelea serikalini hivi sasa.
Ukweli ni kwamba kwa mwezi huu wa October 2011 serikali imelipa kwa mbinde sana mishahara ya watumishi wake. Kwa mara ya kwanza katika utumishi wangu serikalini this month tumelipwa mshahara tarehe 28 badala ya tarehe 19 hadi 23 kama ilivyozoeleka.
Ukiwauliza wa idara ya mishahara wanakwambia serikali imeshaleta payroll lakini exchequer kwa ajili ya malipo bado haijaleta kwa sababu bado wanaendelea kukusanya fedha. Hata sasa hivi ninavyokwambia OC (Operating Cost) exchequer ya mwezi wa kumi haijaja katika kituo changu cha kazi. Exchequer iliyokuja ni ya mishahara tu.
Pia tunasema serikali imefilisika kutokana na mazoea tuliyoyapata katika serikali zilizotangulia. Mfano wakati wa utawala wa Mkapa, OC zilikuwa zinakuja kwa Quarter tena in advance wakati sasa hivi zinakuja kwa Mwezi. Na zikija ni kidogo sana na saa nyingine haziji kabisa. Ukiwauliza watu wa Hazina wanasema hawana pesa. So kwa nini tusisema serikali yetu imefilisika wakati vitendo vinajionyesha??
Mfano kwa sasa hivi tunakaribia kumaliza nusu ya financial year ya 2011/2012. Nakwambia hakuna idara au taasisi yoyote ile ambayo ikifika tarehe 31 December itakuwa imepewa fedha za nusu ya bajeti yake. Hii ndiyo hoja na huo ndio ushahidi ndugu.
Hata ukitaka tukubali kwamba kuna makosa yametokea kwenye payroll system kwa mwezi huu bado inatakuwa ni vigumu kuturidhisha baadhi yetu maana uzoefu wetu unaonyesha hakuna mwaka ambao matatizo haya yametokea. Na kama yametokea kwa nini watumishi wapunguziwe tu? Iweje hiyo system haikuongeza kwa baadhi yao? Na kwa nini itokee katika sehemu nyingi? Huoni kama ilikuwa ni tactic ya ku-offset deficit ya mishahara kwa mwezi huu ambayo imeshindwa kukusanya?[/QUOTE
Mkuu upo sahihi kabisa.Mimi mpaka sasa sijalipwa mshahara wa mwezi Oktoba na leo ni tarehe 29. Haijapata kutokea na tunakoelea sio kuzuri. Kuna watu wengi ninao wajua mpaka leo tupo ndani ya mkumbo mmoja kitu ambacho hakijapata kutokea kwa kweli!!!! Kuna shughuli nzito miezi ijayo
Asiyejua maana haambiwi maana. Haya niambie wewe kwanini mpaka sasa sijalipwa wakati mwezi umekwisha? au nalo ni tatizo la computer?hapo haihitaji usome sanaaa! hakuna uhusiano wa unachotaka kusema na hiyo attachment yako!! nafikiri unapenda sana kuona unawachonganisha wananchi na viongozi wao si vizuri anza upya tafadhali
Eh! kumbe aliyosema Mkulo kuwa serikali ina fedha za akiba ilikuwa geresha!
mkuu umenikumbusha ya Tarik Aziz akitangaza kuwa majeshi ya adui yanazidiwa na kurudi nyuma wakati ni kinyume chake, mpaka alipokamatwa na jeshi la upinzani