Ushahidi wa kupigwa/kutopigwa mawe mtu huu hapa.

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,899
4,623
Wiki mbili zilizopita katika ripoti mojawapo ya magazeti yetu, yaliripoti mkutano wa maombi ya mamoja kwa madhehebu yote ya kikristo mjini Moshi kuombea Taifa. Na agenda kuu ilikuwa ni kuhusu uchaguzi. Askofu mmoja wa assemblies of God, jina nimelisahau ila mwenye kulikumbuka anaweza kutukumbusha kasema hivi:- Wagombea woote watakaoenda kwa waganga wa kienyeji(sangoma) hawatashinda hata mmoja, na kapo yupo atakaeshinda nipo tayari kupigwa mawe kama ilivyokuwa desturi ya agano la kale mtu yeyote akitoa neno la unabii na lisitimie maana Mungu hakumwagiza kulisema alipigwa mawe hata kufa. Huu ni unabii mzito uliotolewa na Askofu ila binafsi nilipata shida ya ni kigezo kipi kitakacho proof kwamba hao wate watakaoshinda hawakuenda kwa sangoma kutafuta namna. Sasa Mungu ni mwaminifu, hiki hapa kigezo(ushahidi) alichotupa. Jimbo la Korogwe vijijini, ccm wamempitisha mgombea wa jimbo hilo sii tu aliye enda kwa sangoma bali sangoma mwenyewe gwiji la siku nyingi Steven Ngonyani AKA. Maji marefu kupeperusha bendera yao. Hivyo basi huyu sangoma ni kigezo tosha cha kupigwa mawe kwa Askofu kama atashinda, na au ni kigezo tosha kwa Mungu wa askofu kutukuzwa na kila mtu kama huyu sangoma atashindwa. Wadau JF nawakilisha!
 
Back
Top Bottom