Ushahidi huu unatosha kumtia hatiani mke!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushahidi huu unatosha kumtia hatiani mke!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kapotolo, Aug 20, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wana MMU habari,
  Nina kaka yangu alioa miaka sita iliyopita, mke aliyemuoa alikuwa na mtoto tayari, walikuwa wanafanya kazi pamoja, walipendana na wakaoana, mwanamke aliamua kumuacha mwanaume waliezaa nae na akawa na kaka yangu, mke ni nurse na mume ni daktari.

  Baada ya miaka miwili ya ndoa ya furaha, wote wawili walikwenda shule kuongeza taaluma zao. Wakawa wakikutana wakati wa likizo au mara nyingine wakiomba ruhusa za dharura na kukutana. Siku moja mke alikwenda kumtembelea mume na akiwa huko bahati mbaya/nzuri mume alikuta sms kwenye simu ya mke imeandikwa 'ukiwa peke yako nipigie'. Mume akauliza kama mke anajua ile namba, mke akakataa kata kata kwamba haijui. Mume akapiga ile namba ikapokelewa na mwanaume nae akajitambulisha kama mwalimu wa mke huko chuoni alikokuwa anasoma, mume alipouliza kwa nini amemuandikia sms ya aina ile mkewe na kuna siri gani ya kuongea akiwa peke yake, yule mwalimu (mwanaume), akashtuka na akajibu kwamba atakuwa amekosea namba. Lakini mumu akajiuliza imekuwaje mke asijue namba ya mwalimu wake? Mume alipatwa na wasiwasi na kuanza kufuatilia. Tabia za mkewe alipokuwa shule pia zilikuwa zimebadilika, hata tendo la ndoa likawa la pinde. Mume akaanza kuwa na wasiwasi. Ilikuwa ni vigumu kufuatilia yanayoendelea chuoni kwa kuwa mume alikuwa busy chuoni na japo alikuwa na wasiwasi lakini aliendelea kumuamini mkewe akijua hawezi kumsaliti na hivyo hakuona umuhimu wa kumfuatilia, na isitoshe mkewe alimwomba radhi kwa ile sms.

  Walipomaliza chuo, wakarudi kazini, ambako walikuta maneno yakisemwa kwamba huyo mke (shemeji yangu) alikuwa hajatulia chuoni na alikuwa akitoka na wanaume wawili, mmoja mwanafunzi mwenzie na mmoja mwalimu. Mume(kaka yangu) akaamua kuyachunguza maneno yale, kwa bahati mbaya akagundua mwalimu wanaesema alikuwa anatembea nae ni yule aliyekuta sms yake kwenye simu. Jamaa (kaka yangu) ilimuuma lakini hakutaka kuamini kama mkewe aliyemwamini anaweza kufanya hayo, aliamua kuchunguza. Mmoja kati ya watu waliosoma na mkewe wakampa namba ya mke wa yule mwalimu aliyekuwa na uhusiano nae. kaka yangu akampigia simu yule mke wa mwalimu (mwanaume wa shemeji yangu) aliyekuwa na uhusiano na mke wake (shemeji yangu). mwanzoni yule mwanamke aliogopa kumweleza chochote kaka yangu kwa kuwa ailhofia reaction ya kaka kwa yule mume wake. Lakini baadae aliamua kumweleza kaka kila kitu anachokijua kuhusu uhusiano wa shemeji yangu na mume wake. Ni habari ndefu lakini kifupi yule mke wa mwalimu anasema alianza kupata wasiwasi wa mahusiano yasiyo ya kawaida baina ya shemeji yangu na mumewe baada ya wawili hawa kuwa karibu sana isivyo kawaida. Kwani walikuwa wakiitana ofisini hata usiku na kukaa mpaka usiku sana, mke wa mwalimu alipouliza aliambiwa na mumewe kwamba yule mwanafunzi (shemeji yangu) anamsaidia kusahihisha na kuanda somo kule ofisini. Mke alizidi kuwa na wasiwasi pale ambapo mume akiwa ofisini na shemeji yangu simu yake either itakuwa imefungwa au itapigwa bila kupokelewa. Siku moja aliamua kufuatilia ofisini na kukuta wakiwa ndani wamezima taa na akasikia sauti zinazoashiria watu wakifanya mapenzi. Aligonga mlango, ulikuwa umefungwa, wakatulia, akasubiri nje akiwa anatetemeka asijue cha kufanya, baadaye wakaendelea tena, na baada ya saa moja ya kusubiri nje akatoka mumewe na condom mkononi iliyotumika anakwenda kuitupa, bila kujua kama mkewe alikuwa yuko nje anasubiri na baadae akatoka huyo shemeji yangu na kurudi bwenini. Mume siku hiyo alimpiga sana mkewe kwa kudai kwa nini anamfuatilia sana. Mke akaamua kumfuata shemeji yangu kesho yake kumuonya asitembee na mumewe, kwa jeuri shemeji yangu akamwambia asimfuate fuate, mumewe ndio kamfuata yeye. Akamuonya kuwa na yeye ni mke wa mtu, asikie uchungu wa kufanyiwa yale. Anasema hawakuacha ukawa ndio mchezo kufanyia mapenzi ofisi na amewakuta zaidi ya mara mbili. Mpaka walipotaka kufumaniwa na mabosi wa chuo ndio wakabadilisha venue, wakawa wanakutana guest mjini. (chuo kiko nje ya mji kidogo), hata guest pia aliwahi kuwakuta. Alimweliza kaka yangu mambo mengi ikiwa ni pamoja na shemeji yangu kuondoka chuoni ghafla anapogundua amekutana na yule mwanaume siku mbaya ( inaonekana baadae labda aliaacha kutumia condom - hii haina uhakika - lakini kaka anasema ni kweli aliwahi kwenda kwake kama mara mbili kwa ghafla).

  Na pia akamweleza kaka yangu kuwa kuna mwanafunzi mwenzake ambaye nae alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na shemeji yangu. Na huyo mwanafunzi baada ya kuonywa alikiri ni kweli alikuwa na uhusiano nae na hawakuanza jana wala juzi.

  Habari hizi zilimuumiza sana kaka yangu, alimuuliza mkewe, kuhusu haya, mkewe alikataa na kusema wanamsingizia. Uzuri mmoja kati ya waliokuwa wanajua haya mahusiano ni sister (nun) ambaye nae alikiri kumfuata yule mwanafunzi na kumuonya kuhusu huo uhusiano na mke wa mtu (shemeji yangu). Kijana alikiri na kuomba radhi. kaka yangu aliwarekodi watu wote aliokuwa anaongea nao, so aliamua amsikilizishe mkewe maneno yaliyokuwa yanasemwa na mke wa yule mwalimu pamoja na yule sister, lakini shemeji yangu aliendelea kukataa na kusema wanamsingizia. Na hakuonyesha dalili za kukiri na kuomba radhi. Kaka aliamua kumpigia simu yule mke wa mwalimu ili aongee na shemeji yangu, ili shemeji yangu amkanushe kwamba anayosema mke wa mwalimu si kweli, lakini shemeji alichofanya alipokea simu, akamwambia yule mwanamke, 'asante kwa kunivunjia ndoa na kukata simu'. Je alimaanisha nini?

  Pia kulikuwa na minong'ono kuwa alikuwa na uhusiano na mwanaume aliyezaa nae akienda kwao likizo. Ingawa hii imekuwa ngumu kuithibisha.

  Kaka yangu alimwita mzee wake na akamweleza kila kitu, baba mtu akasema ushahidi huu hautoshi kusema mkeo ana tabia hiyo. Kaka alichukia kwa kuwa alitegemea mzee amuonye huyo mwanamke lakini akashangaa ana-side nae.

  Mbaya zaidi huyo mke wa mwalimu anasema wanaendelea na mawasiliano, na kaka anasema mkewe ana line kama sita za simu na nyingine hazijui.

  Labda ni kweli au ni uongo, hatujui, Lakini ninachouliza kwenu ndugu wana MMU, ushahidi huu unatosha kumtia huyu shemeji yangu hatiani? Kaka amechanganyikiwa hajui afanye nini? Na kama ushahidi huu unatosha, kaka amfanye nini huyu mke aliyemsaliti japo alimpenda na kumuoa akiwa tayari ameshazaa?

  Ni mengi lakini nisiwachoshe, naomba ushauri kwa huyu kaka yangu, yuko devastated, hajui afanye nini kwa sasa. wana mtoto mmoja.

  Naomba usichoke, soma habari yote na ushauri wako unaweza kumsaidia kaka yangu, ningefurahi kupata constructive advices.

  Asanteni.
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  inaonyesha huyo kaka ako ni mume *****!!!!!kwani wanawake wameisha mpaka ang'ang'anie huo msiba?????
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,840
  Trophy Points: 280
  Daaaah! Hizi ndoa hizi! Kifupi ni kwamba huyo mwanamke atamletea magonjwa kaka yako!
  Ni vyema akachukua huamuzi mgumu(kumuacha)

  Nampongeza sana kaka yako kwa busara alizonazo!
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,319
  Trophy Points: 280
  Kuna ushahidi wa aina mbili................ila wa kaka yako ni wa mazingira.......................Kifupi kadri muda unavyoenda anapoteza ushahidi lakini wakati huohuo anaumia sana.......................Ni yeye tu ndiye anayejua uzito wa ushahidi wa mazingira. Otherwise sie wengine tunapapasa tu!
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,230
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  ni habari ya kusikitisha sana...kwa upande wangu hapo siwezi kufanya kitu kingine zaidi ya kumpiga chini man siwezi kukubali kuendelea kuumizwa...huo ushahidi unatosha sana. kwa taarifa yako hakuna mwanamke anayeweza kukubali kuwa amemegwa kamahujamkuta kitandani live! kama anaweza kuvumilia kuchangia na wengine aishi naye lakini kama inamuuma kuliwa mke basi aangaliealternative maana nahisi huenda akawa hata huyo anayesema ni mwanae ikawa ni geresha tu!...nampa pole sana kaka yako...hata hivyo nampongeza kwa kuwa mvumilivu...kwa upande wangu siwezi hata kuomba ushauri ikishafikia hatua hiyo maana walio wengi watasema nisimwache na wakati ninayeumia ni mimi...
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kaka hii ni ndoa lakini, sio rahisi kama unavyosema, lakini nimekuelewa.
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Hivi mtu kama umejiridhisha kuwa mkeo ni cheater..unatakiwa u prove kwa nani tena??? Maana nashangaa anaposema wazee hawaamini. Why is it important kwa wazee 'kuamini'. Kwani kuna mahakama na hao ndio majaji?

  Huyo ni mume 'b.w.e.g.e' tu. Hakuna cha watu hawaamini wala nini ...huyo ni mkewe au mke wa 'wazee'
   
 8. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Mi ni mwanamke lakini siku ntakapoamua kufanya maamuzi magumu hao 'wazee' watapewa taharifa tu wala wasitegemee mimi kuwaomba ruhusa.
   
 9. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  talaka uwa wanapewa walio kwenye ndoa, yani mimi kama napata ushahidi wa namna hiyo hakuna majadiliano hakuna kuita wazee wala nini, nikumtimua tu, kwanza mwanamke anaonekana jeuri
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Nyani Ngabu hebu njoo huku kutoa ushauri.

  Ataacha wangapi? Teh teh teh
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Ni heri kukaa bila Mke au Mume, kuliko kung'angania na Kufa na Ukimwi!!
  Mume/Mke anatafutwa Uhai je?
  Hata maandiko yanaruhusu Kuachana/Kutengana iwapo mmoja wa wanandoa ni Mzinzi!!
  Uamuzi/Ushauri wa mwisho anao kaka yako sisi hapa JF, uwezo wetu utaishia kwenye KeyBoard tu.
   
 12. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,230
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  hata akiiacha 100 sioni tabu kuliko kuishi kwa kujuta kwa nini ulioa mke!
   
 13. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,230
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  hata kama ni ndoa kuna kipindi kinafika inabidi ufanye maamuzi magumu..kwani Mungu yeye anapenda uishi kwa tabu ati kwa sababu tu mmefunga ndoa? kama mwenzio siyo mwaminifu hiyo inatosha tu kupoteza sifa ya kuwa kwenye ndoa...
   
 14. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Mimi huko alikofika kaka yako ni mbali sana, kwenye lile tatizo la sms tuu ningeweza kupata majibu na kutoa maamuzi magumu. Dawa ilikuwa ni kumtema. Wamsingizie kwa lipi alilonalo wote hao?? Kaka yako atakuwa ni mume aliyeshikwa masikio na mkewe. Kwanini wasiwaseme wenzie na awe yeye?? Huo ushahidi wa mazingira hautofautiani na ushahidi wa live maana vielelezo vyote vinaashiria ukweli tupu. Mwache akubali kumegewa ila awe mvumilivu na mpole kwa wanaume wenzie, si kaamua kuishi na kimeo ndani??
   
 15. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Aisee mwambie kaka yako "uamzi mgumu unatakiwa"tena hata leo maana hapo sasa ni kukaribisha magonjwa kwa kuendelea kuwa na huyo mwanamke
   
 16. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Mimi mke wangu anatoka nje ya ndoa, nimeamua kutomfanya chochote akiridhika ataacha.
  atafanywa weeeeeeeee...... akichoka atarudi.
  ikumbukwe kunguru hafugiki.
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  du asanteni wote, nitamshauri, naona yuko njia panda, kwa ushauri huu atapata njia ya kwenda!!!
   
 18. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60

  Ulikuwa na haja gani ya kumuoa sasa?
  Hakuna ndoa hapo.
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Akichoka, mawili, mtoto wa nje au ukimwi. Sidhani kama kaka yangu atamwacha afanyweee, no i dont think so, so far wametangana vyumba, the next step nadhani ni kuachana.
   
 20. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Mimi katika kuangalia na uzoefu wangu, manesi wengi wako loose sana sijui kwanini. Yaani kwa ushahidi wa huyo mke wa mwalimu, sms na huyo nun. Kaka yako akiendelea kukaa na huyo kahaba ataumia muda si mrefu kama bado.Na akitaka ushahidi kamili aombe kukutana na yule mwanafunzi ila amhakikishie kuwa anachotaka si ugomvi ila amsaidie tu ushahidi na amrekodi.Ataambiwa uchafu wa mkewe!
   
Loading...