Ushabiki kumpamba Lowassa leo: Ujinga halisi wa Watanzania au laana ya fedha?

Mleta uzi utajibu haya:
  • Wakati nyumba za serikali zinauzwa unamaanisha tulikuwa na viongozi wabovu? (Serikali kwa sasa inaingia takribani gharama ya sh. 50bilioni) kuwalipia viongozi pango za nyumba kwa mwaka. Sasa je nani alihusika wakati huo, ni LOWASSA au Magufuli?
  • Leo hii umezuka mtindo wa kujenga barabara za lami ambazo baada ya mwaka mmoja zinaharibika (kumbuka barabara hizo ujenzi wa kilomita moja hugharimu wastani wa sh. 500milioni). sasa je barabara hizo anazijenga au kuzisimamia LOWASSA au Magufuli?
  • Kumbuka kipindi nyumba za watu maskini zinabomolewa na nyingine zikitaka kubomolewa Pinda aliagiza waziri wa ujenzi Magufuli kutumia ubinadamu wakati wa kutekeleza shughuli zake sasa je, wakati pinda anasema hayo alimaanisha nini kwa msimamizi huyo wa barabara?

Mengi yapo, nadhani hapa watu tuamue uchaguzi kwa kujenga hoja (wagombea ubunge wengi ni kundi lilelile ambalo KINANA analiita MAWAZIRI MIZIGO, wabunge Mizigo na baadhi yao ndo wamo kwenye ESCROW, n.k
 
Watanzania washazoeshwa rushwa. Mwizi ndo mjanja. Wezi hawafungwi. Kutwa kucha wako kwenye mavogue na magorofa.
Miaka na miaka imekuwa hvo. Sasa umekuwa mtindo wa maisha. Lowasa anaonekana mjanja kuliko magufuli maana yeye kalamba zaid.
Ni watu kama mimi tunaofikiria tofauti ndo hatukubaliani na ujinga huu na hvo tunabaki kwenye mstari

Piga chini lowasa. Inua heshima ya Mtanzania
 
Siamini! siamini! siamini!

Ushabiki huu ulipoanza nilidhani kejeli. Baadhi walianza kwa kusema Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya CCM nikaamini (nakubaliana na hilo 100%), Wengine wakasema yeye ni mkali kidogo kuliko JK nikakubaliana na hilo na mengine mengi yakaja ya ukweli na ya uongo. Sikudhania itafika siku watokee watu wa kumkweza Lowasa kufikia hatua ya kuanza kampeni za kumtafutia urais mapema kiasi hiki.

Mmoja kaamua kumlinganisha Lowassa na Dr. Slaa akidai mmoja kati ya hawa pekee ndiye angefaa kuongoza nchi yetu (kama itakuwapo bado) ifikapo 2015 Oktoba. Nimeshtuka sana kuiona hali hii ya ushabiki wa ghafla-ghafla kumuunga mkono Lowasa.

Hawa watu wanaotaka Lowassa (ambaye yupo tayari kufanya lolote kupata urais) awe na hadhi sawa na Dr. Slaa (aliyesubiri watu wengine waseme anafaa urais na kumwomba agombee) wanatumia kigezo gani?

Lowassa aliyedai wabunge wamemwandama kwa habari za magazeti ya udaku na kushindwa kuthibitisha hilo leo anafaa vipi kuwa rais wa Tanzania? Kwanini kama tunaipenda nchi yetu kwa dhati tusimtupilie mbali jumla ili akija kiongozi mwingine awe na nidhamu na kujua kuwa watanzania ukiokosea wanakutimua na ajizuie kukosea maksudi?

Je, ni kweli kwamba tumefilisika viongozi wanaofaa na kubakiwa na Lowasa pekee huko kwenye Magamba? Is it possible kwamba tu wajinga kiasi hicho au ni laana ya fedha ili tuamini kuwa wanaompigia debe wanatarajia kupata fadhila zake mzee huyo, asiyecheka na wanyonge kama watendaji katika wilaya na kuwanyenyekea wenye fedha kama Rostam hata kufikia kupindisha sheria maksudi ili watajirike zaidi kwa gharama za wanyonge? Ya Richmond si madogo lakini naamini vyombo vyetu vya dola vingekuwa huru vingegundua madudu mengine zaidi.

Nawatahadharisha watanzania kutofanya kosa la kumfagilia Lowassa, si kwa ajili ya kumwadabisha tu bali kuweka msingi imara kwa waroho kama yeye endapo watajitokeza next time. Viongozi wajao wanatakiwa kujifunza kutokana na adabu tutakazoamua kuwatia kina Mkapa, JK na wapambe wao kwa makosa ya kukusudia waliyofanya ili kujitajirisha.

Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu atuasaidie kupata viongozi bora na kutuepusha na watu wa "Zamu Yetu" kama Ridhiwan, JK, Lowassa na wengine wengi ambao tutazijua habari zao vema baada ya serikali ya wanamtandao kuondoka madarakani.

Upuuzi mtupu, unataka apambwe nani sasa mkuu mbona hujamtaja, hujaeleweka, ushauri gani wa namna hii.
Yaelekea mleta mada ni mtu ambaye hujitegemei kifikra.
 
Ushabiki kwa Lowasa ni UJINGA uliokithiri wa Watanzania. Ni kweli kuna wanaohongwa pesa, ila hao ni wachache. Hawazidi 2000. Wengine wooote, upumbavu tu
je unadhani wanaoshabikia CCM akili zao ziko sawa?Jibu unalo.Ni nani kawafanya watanzania wajinga tena wapumbavu
 
Nashukuru siasa za mwaka huu. Zinaashiria kuzaliwa kwa Tanzania Mpya kabisa. Kwa wanaotafakari vyema CCM haitakuwa tena ile ile wala upinzani hautakuwa ule. Something really really great has just transcended our politics!!
 
The Analyst

Hilo neno ujinga tumeshalisikia from Mkapa, so si kitu kigeni,

Wajinga na wapumbavu tupo tu, time will tell
 
Last edited by a moderator:
Upuuzi mtupu, unataka apambwe nani sasa mkuu mbona hujamtaja, hujaeleweka, ushauri gani wa namna hii.
Yaelekea mleta mada ni mtu ambaye hujitegemei kifikra.
Ukawa wanampamba kingunge ndo maana Jana mkampa dakika 40, lowasa 7 akili zenu hivyo,
 
Siamini! siamini! siamini!

Ushabiki huu ulipoanza nilidhani kejeli. Baadhi walianza kwa kusema Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya CCM nikaamini (nakubaliana na hilo 100%), Wengine wakasema yeye ni mkali kidogo kuliko JK nikakubaliana na hilo na mengine mengi yakaja ya ukweli na ya uongo. Sikudhania itafika siku watokee watu wa kumkweza Lowasa kufikia hatua ya kuanza kampeni za kumtafutia urais mapema kiasi hiki.

Mmoja kaamua kumlinganisha Lowassa na Dr. Slaa akidai mmoja kati ya hawa pekee ndiye angefaa kuongoza nchi yetu (kama itakuwapo bado) ifikapo 2015 Oktoba. Nimeshtuka sana kuiona hali hii ya ushabiki wa ghafla-ghafla kumuunga mkono Lowasa.

Hawa watu wanaotaka Lowassa (ambaye yupo tayari kufanya lolote kupata urais) awe na hadhi sawa na Dr. Slaa (aliyesubiri watu wengine waseme anafaa urais na kumwomba agombee) wanatumia kigezo gani?

Lowassa aliyedai wabunge wamemwandama kwa habari za magazeti ya udaku na kushindwa kuthibitisha hilo leo anafaa vipi kuwa rais wa Tanzania? Kwanini kama tunaipenda nchi yetu kwa dhati tusimtupilie mbali jumla ili akija kiongozi mwingine awe na nidhamu na kujua kuwa watanzania ukiokosea wanakutimua na ajizuie kukosea maksudi?

Je, ni kweli kwamba tumefilisika viongozi wanaofaa na kubakiwa na Lowasa pekee huko kwenye Magamba? Is it possible kwamba tu wajinga kiasi hicho au ni laana ya fedha ili tuamini kuwa wanaompigia debe wanatarajia kupata fadhila zake mzee huyo, asiyecheka na wanyonge kama watendaji katika wilaya na kuwanyenyekea wenye fedha kama Rostam hata kufikia kupindisha sheria maksudi ili watajirike zaidi kwa gharama za wanyonge? Ya Richmond si madogo lakini naamini vyombo vyetu vya dola vingekuwa huru vingegundua madudu mengine zaidi.

Nawatahadharisha watanzania kutofanya kosa la kumfagilia Lowassa, si kwa ajili ya kumwadabisha tu bali kuweka msingi imara kwa waroho kama yeye endapo watajitokeza next time. Viongozi wajao wanatakiwa kujifunza kutokana na adabu tutakazoamua kuwatia kina Mkapa, JK na wapambe wao kwa makosa ya kukusudia waliyofanya ili kujitajirisha.

Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu atuasaidie kupata viongozi bora na kutuepusha na watu wa "Zamu Yetu" kama Ridhiwan, JK, Lowassa na wengine wengi ambao tutazijua habari zao vema baada ya serikali ya wanamtandao kuondoka madarakani.

Lowasa sasa Kahamia CDM....uchafu umegeuka kuwa usafi kisa mchafuzi kabadili nguo ilhal moyo na damu ni ile ile
 
Nashukuru siasa za mwaka huu. Zinaashiria kuzaliwa kwa Tanzania Mpya kabisa. Kwa wanaotafakari vyema CCM haitakuwa tena ile ile wala upinzani hautakuwa ule. Something really really great has just transcended our politics!!

Una akili nyingi sana ungefaa kugombea hata urais maana hizi point zako ukianza kizieleza ni kama 30 mnt zaidi ya lowasa wa DKK 5
Ccm ya majizi ndo unakufa inazaliwa ccm mpya na upinzani wa nguvu bungeni unaongezeka hapo WENGINE wanasema itakuwa dhaifu,
 
Upuuzi mtupu, unataka apambwe nani sasa mkuu mbona hujamtaja, hujaeleweka, ushauri gani wa namna hii.
Yaelekea mleta mada ni mtu ambaye hujitegemei kifikra.

Mleta mada aliandika uzi huu mwaka 2011 kipindi ambacho ww na Kubenea Mlikuwa mnamuita Fisadi....uwe unatumia akili kidogo
 
Lowasa sasa Kahamia CDM....uchafu umegeuka kuwa usafi kisa mchafuzi kabadili nguo ilhal moyo na damu ni ile ile

Wanajua tu Jana wamefanya kituko cha karne arusha, kingunge dakika 40, lowasa 7,
 
Mleta mada aliandika uzi huu mwaka 2011 kipindi ambacho ww na Kubenea Mlikuwa mnamuita Fisadi....uwe unatumia akili kidogo
Mkuu manyumbu haya achana Nao wangu kuwa na akili Jana arusha wangempa kingunge kueleza Sera dakika 40, na lowasa dakika 7, aibu ya karne,
 
je unadhani wanaoshabikia CCM akili zao ziko sawa?Jibu unalo.Ni nani kawafanya watanzania wajinga tena wapumbavu

Nyie mgekuwa na akili timamu, mgefanya haya,
1,slaa wa nini kingunge safi sana?
2,kingunge dakika 40 za kumwaga Sera, lowasa dakika 7?
Nafikiri sio nyie kuna shida mnayo akilini sio bure,
 
Lowasa sasa Kahamia CDM....uchafu umegeuka kuwa usafi kisa mchafuzi kabadili nguo ilhal moyo na damu ni ile ile
Sasa CCM imekuwa safi baada ya Lowassa kutoka? Chenge, Ngeleja na wengine vipi? Halafu kama mnaamini ni mchafu kwanini hakushughulikiwa? Maana yake CCM ni dhaifu haiwezi kupambana hata na mtu mmoja tu kwa faida ya Taifa-hakika imechoka, ipumzishwe.
 
Nyie mgekuwa na akili timamu, mgefanya haya,
1,slaa wa nini kingunge safi sana?
2,kingunge dakika 40 za kumwaga Sera, lowasa dakika 7?
Nafikiri sio nyie kuna shida mnayo akilini sio bure,

Hivi umejiuliza kwanini watu wanamfurahia licha ya kuongea dakika chache? Watu wamechoka na maneno mengi yasiyo na utekelezaji, wamekata tamaa. Hii yote imesababishwa na CCM.
 
Back
Top Bottom