Ushabiki kumpamba Lowassa leo: Ujinga halisi wa Watanzania au laana ya fedha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushabiki kumpamba Lowassa leo: Ujinga halisi wa Watanzania au laana ya fedha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Jun 1, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Siamini! siamini! siamini!

  Ushabiki huu ulipoanza nilidhani kejeli. Baadhi walianza kwa kusema Lowassa bado ana nguvu sana ndani ya CCM nikaamini (nakubaliana na hilo 100%), Wengine wakasema yeye ni mkali kidogo kuliko JK nikakubaliana na hilo na mengine mengi yakaja ya ukweli na ya uongo. Sikudhania itafika siku watokee watu wa kumkweza Lowasa kufikia hatua ya kuanza kampeni za kumtafutia urais mapema kiasi hiki.

  Mmoja kaamua kumlinganisha Lowassa na Dr. Slaa akidai mmoja kati ya hawa pekee ndiye angefaa kuongoza nchi yetu (kama itakuwapo bado) ifikapo 2015 Oktoba. Nimeshtuka sana kuiona hali hii ya ushabiki wa ghafla-ghafla kumuunga mkono Lowasa.

  Hawa watu wanaotaka Lowassa (ambaye yupo tayari kufanya lolote kupata urais) awe na hadhi sawa na Dr. Slaa (aliyesubiri watu wengine waseme anafaa urais na kumwomba agombee) wanatumia kigezo gani?

  Lowassa aliyedai wabunge wamemwandama kwa habari za magazeti ya udaku na kushindwa kuthibitisha hilo leo anafaa vipi kuwa rais wa Tanzania? Kwanini kama tunaipenda nchi yetu kwa dhati tusimtupilie mbali jumla ili akija kiongozi mwingine awe na nidhamu na kujua kuwa watanzania ukiokosea wanakutimua na ajizuie kukosea maksudi?

  Je, ni kweli kwamba tumefilisika viongozi wanaofaa na kubakiwa na Lowasa pekee huko kwenye Magamba? Is it possible kwamba tu wajinga kiasi hicho au ni laana ya fedha ili tuamini kuwa wanaompigia debe wanatarajia kupata fadhila zake mzee huyo, asiyecheka na wanyonge kama watendaji katika wilaya na kuwanyenyekea wenye fedha kama Rostam hata kufikia kupindisha sheria maksudi ili watajirike zaidi kwa gharama za wanyonge? Ya Richmond si madogo lakini naamini vyombo vyetu vya dola vingekuwa huru vingegundua madudu mengine zaidi.

  Nawatahadharisha watanzania kutofanya kosa la kumfagilia Lowassa, si kwa ajili ya kumwadabisha tu bali kuweka msingi imara kwa waroho kama yeye endapo watajitokeza next time. Viongozi wajao wanatakiwa kujifunza kutokana na adabu tutakazoamua kuwatia kina Mkapa, JK na wapambe wao kwa makosa ya kukusudia waliyofanya ili kujitajirisha.

  Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu atuasaidie kupata viongozi bora na kutuepusha na watu wa "Zamu Yetu" kama Ridhiwan, JK, Lowassa na wengine wengi ambao tutazijua habari zao vema baada ya serikali ya wanamtandao kuondoka madarakani.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ofcourse kiutendaji jamaa anapiga kazi kuliko hao... just imagine pinda kafanya maamuzi yapi maguu? hata huyo mkwereee, so kuchapa kazi lowasa poa ila...
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sifa zote apewe huyo Lowasa lakini hili la urais wetu watanzania HAPANA amepoteza sifa. Anahusika na ufisadi wa EPA kupata pesa za kumpigia kampeni swahiba wake, dowan anahusika pia, mvua ya thailand nao ulikuwa ni wizi tu hafai hatufai
   
 4. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naona wazembe wanamwogopa Lowassa kweli, ndio lakini ndie kiongozi makini, jasiri, mkali, mwenye uzoefu, ana utajiri safi na wa siku nyingi na siio kama wa Ridhiwani na babake, pekee anaweza kutuvusha kwenye ulimwengu wa watanzania kuonewa ndani na nje au nchi jirani.

  Peke yake ataweza kupambana na kina Kibaki, kumbukeni alivyoikoromea Egypt walipotutisha kupeleka maji ya Ziwa Victoria Shinyanga, eti maji ya Misri, sasa Kenya wanajenga airport karibu na KIA mbona Sitta hasemi kitu akiwa waziri wa EAC?

  Aliitembelea Zanzibar mara kwa mara, je Pinda alienda lini? je Zanzibar si sehemu ya Tanzania? basi wapewe uhuru wao kamili ikiwa waziri mkuu anaogopa kwenda, Lowassa aliwapenda nao walimkubali, mafisadi ni wahindi lakini wao hawatajwi, ila kila mzalendo mwenye vihela vyake anaandamwa na kuzingiziwa mpaka akimbie, Ukomunisti unaangamiza tanzania!

  Long Life President Lowassa!!!
   
 5. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe katika hilo lakini huoni kumpa nafasi kubwa zaidi ni sawa na kuweka Precedent mbaya kwa watakaofuatia. Yaani kiongozi anatumia nafasi ya uwaziri mkuu kwa manufaa yake na rafiki zake na kuitia nchi nzima umasikini halafu baada ya muda mnampa madaraka makubwa zaidi?

  Tukimchagua Lowassa kuwa rais leo halafu akaleta miradi kibao yenye sura ya Richmond na kwa ukali wake vyombo vya habari vinavyojaribu kutusaidia vikabanwa sana unadhani wenzetu wanaofanya kweli kama Rwanda tutawakuta wapi baada ya yeye kumaliza muda wake pengine 2025?

  Jamani jamani jamani haya mapenzi ya ghafla kwa Lowasa yanatokea wapi? Mfukoni mwake au juu, angani? Nimekuwa mjinga sana siku hizi au wenzangu ndiyo mmepotea? Yaana kwa kosa au makosa aliyofanya bado anafaa kuwa rais kweli? Mmesahau sifa za JK wakati wanamtandao wanamwandalia Rostam ulaji?.... Alionekana chaguo la Mungu ujue wakati ule!

   
 6. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pesa za EPA zipo kwa ndugu wa Nyerere NIMROD MKONO na bosi wake JEETU PATEL na kampuni yake ya BANK M LIMITED ambayo mkono ni bosi mkuu wa bodi, zilitumika pesa za epa kuianzisha. nyinyi msiseme ovyo
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Kama mtu hakutumwa kufanya hivyo basi ana matatizo ya akili.
  Hawa watu wawili kamwe si wakuwafananisha.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  It does not matter. Nina hakika kuna Wajerumani watakwambia hivyo hivyo kuhusu Hitler. Huyu kishahukumiwa na historia.
   
 9. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Juzi nimetoa mada ya jinsi Lowassa alivyo na chuki na baadhi ya makabila ikiwa ni sehemu ya kuelezea huyu jamaa alivyo na sifa ambayo haikubaliki, huyu jamaa hawezi kuongoza hii nchi kwani malengo yake ni mawili makubwa:

  1. Kuja kuwakomoa mahasimu wake na kulipiza kisasi
  2. Kuja kujineemesha kwa rasilimali za watanzania kwani ni mtu mwenye tamaa ya mali sana na asiyeridhika. wakati wa utawala wake tutegemee ongezeko la kubinafsisha viwanja vya watu kwa maslahi yake.

  Tutegemee assets za institutions mbalimbali kubinafsishwa kwa watoto wake. Naona bado anaota ndoto ya utotoni na hata alipogundua kwamba amechemsha bado anataka kuitimiza. hivi alishasema anataka kuchangia nini katika uchumi wa nchi yetu anapotaka kuja kwa kasi kubwa namna hiyo?
   
 10. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  The Analysit, Bora afadhali au potelea mbali?

  Hebu kipi ni bora kati ya hivyo viwili. Mbona mna chuki sana na Lowassa? Kama mna chuki ya kweli na ufisadi mngemchukia Jk, Ben, Mwinyi and etal kwa ujumla CCM hao hao mnaowatetea ni mafisadi kuliko Lowassa na kwa uchapa kazi hapo aliye level za Lowassa, sema tu aliangushiwa jumba bovu na kuwa victimased na kufanywa symbol ya ufisadi unataka kuniambia Lowassa ndo kasababisha CCM ikapoteza umaarufu?

  Hao walimsukia majungu kwa matakwa yao kisiasa na always ukweli unasimama, time will tell utajua tu ni nani alimframe mwenzake na kwa nini?
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  MCHONGANISHI

  Tunawachukia wote. Ndiyo maana mtu yeyote aliye na harufu ya kifisadi tunasema hatufai. Tanzania deserves better. Na Lowassa atakuwa worse than Kikwete, worse than Mkapa, worse than Mwinyi.

  Afadhali tujiepushe naye mbali kwa sababu naamini kuna Watanzania wenye uwezo wa kuongoaza nchi hii mbali na Lowassa. Akae pembeni ale mali zake (kama hazitakamatwa na mwendawazimu mmoja).
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mnahangaika nini? Lowassa ndie Rais na tupo hapa hapa jamvini msijekimbia, hapa hapatikani kiongozi msafi, isipokuwa wa kuweza kutukomboa ni Lowassa au Slaa tu
   
 13. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Pharaoh,

  Is everything okey? Kilichomwondoa madarakani ndiyo sababu ya upinzani dhidi yake. Kama huuoni kuwa tatizo basi, unaweza kuendelea na kampeni yako lakini binafsi naogopa sana ushabiki blind kama huo.

  Unajua mtu anayepindisha sheria ili kujipatia fedha hawezi kushindwa kuvunja au kubadili katiba ili aendelezeze udikteta. Anaweza kuwa mkali sana lakini kwa miradi ya ulaji binafsi ninamdisqualify moja kwa 1.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wanajamvi tusaidiane katika hili, Lowasa anaonekana afadhali anapolinganishwa na nani? Amewazidi magamba wanamtandao wenzake au ni bora kuliko kiongozi gani? Hizi lugha za watu wa magamba zitaisha lini? Mara mikataba mibovu iliingiwa katika serikali ya awamu ya nne kwa hiyo si kosa lao mara tumejenga mabarabara tangu uhuru. Tuwaeleweje? Magamba ni Magamba tu!

  Mkimpenda sana Lowasa, mchagueni lakini msigeuke kuanza kuhoji uwezo wake kama mnavyofanya kwa JK. Nashukuru Mungu sikumpigia kura JK tangu mwanzo na Lowasa sitampigia.

  Watu wengine bwana, mnasababisha watu wahoji hadi kifo cha mwalimu utadhania waliahidiwa na Allah kwamba Mwalimu hatakufa.

  Mmewahi kusikia hofu ya uwezekano wa wanamtandao kuwa walimuwahi Mzee wa watu kwa kuwa angewachelewesha kwa miaka mingine kumi (10) kuingia madarakani baada ya Mkapa. Inasemekana mmoja wa walinzi wa marehemu ni mlinzi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Richmond na Dowans. Mimi sijui! Kama rais wa nchi yangu vile!

   
 15. m

  mjombajona JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 262
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huu mpango wa sasa zamu yetu eti watu wamekaa kwenye foleni wanangoja akitoka huyu mimi niwe Rais hebu Watanzania tuushtukie.

  Watu wanaotafuta Urais kwa udi na uvumba hawafai. Nyerere alishatuonya hivi kwa nini hatusikii?haiingi akilini mtu kusema anajitayarisha kuwa Rais hata kwa miaka mitano mpaka kumi.

  Hivi kwanini wa magamba hamuigi mfano wa Dr wa ukweli kukaa kimya hadi watu wanakuomba kuwa unatufaa tusaidie uwe mgombea?
   
 16. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi naona kumfagilia Lowassa ni sawa sawa na kukubali ku-settle for less.

  Watanzania tusijishushe kiasi hiki kwakweli we can do better than this ( We do not need JK and we do not need Lowassa either; wote ni hao hao tu sema strategies na uelewa umetofautiana lakini kama grade one is -F na mwingine +F (if it exist).

  Kweli CCM wameishiwa kabisa? Kama CCM wako serious lazima waelewe this is not a popularity contest ni lazima wamteue kiongozi mzalendo, mwenye uchungu na nchi sio kuendeleza usanii.
   
 17. J

  John W. Mlacha Verified User

  #17
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  akipewa urais mimi nahama nchi
   
 18. J

  John W. Mlacha Verified User

  #18
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  hiyo ya kwanza hapo ni kweli kabisa hata Nape analijua hili , na Lowasa akikamata nchi basi Nape inabidi ahamie India na arudi baada ya miaka 10
   
 19. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,792
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  wadogo zake lowassa tumewaona
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kazi za PM haazipimi kwa yale yanaondikwa magazetini mkuu. Ndio maana watu wanamsifia Lowasa sababu yeye alikuwa mtu wa kujua kutumia media.

  Nyuma ya pazia kiofisi Ulizia uupu na mambo anayosign na kuagiza Lowasa na yale aliyoasign na kuagiza pinda nyuma ya pazia. I mean kiofisi.

  Watazania hawatakiwi kudanganywa toto na PM anayeffokea fokea DC au RC mbele ya TV. Ni kutaka sifa . Good manager a good leader anajua anatakiwa kufanya nini . Lowasa is neither He is just an opportunist na ni Hatari kwa Taifa

  Tuwaogope watu wanapata umaarufu kwa kutumia Media.So far tumeona kutoka Kwa JK. I expect the worse from Lowasa.....
   
Loading...