Ushabiki huu ni wa hatari!

Ushabiki huu ni wa hatari!

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,772
Juzi nilikuwa kijijini Jaribu mpakani - Rufiji.
Sijui Simba ilikuwa inacheza natimu gani siku hiyo. Jamaa mmoja
ambaye ni maarufu kwa jina la Messi alikuwa amechukua redio
yake ndogo chooni huku akisikiliza mpira huo.
Kama unavyojua vyoo vingi vijijini milango yake ni ya gunia.

Balaa ilikuja baada ya Sunzu kama sikosei kufunga bao, Jamaa
kajisahau kuwa yuko Chooni, kakurupuka pale kwenye shimo
huku akiwa kama alivyozaliwa na kutoka nje na kiredio chake
huku akishangilia.......
Duh! huu ushabiki!
 
Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mashabiki wa simba ni mataahira!
 
Nifuraha tu jamani mbona wachezaji ulaya wanavua nguo na kutakuwa na chupi tu hamsemi mwacheni aonyeshe furaha yake ya ushindi kwa simba. Simba hoyeeeeeeeeeeeee Fc Barcelona juuuuuuuuuuuuuuuuu zaidi
 
Nadhani sio ajabu,mbona ulaya watu wanavua nguo na kuingia katikati ya uwanja. ''kipendacho roho,ula nyama mbichi.
 
mamammaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kama namuona vile hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa maskini loh!
 
Nifuraha tu jamani mbona wachezaji ulaya wanavua nguo na kutakuwa na chupi tu hamsemi mwacheni aonyeshe furaha yake ya ushindi kwa simba. Simba hoyeeeeeeeeeeeee Fc Barcelona juuuuuuuuuuuuuuuuu zaidi

Nadhani sio ajabu,mbona ulaya watu wanavua nguo na kuingia katikati ya uwanja. ''kipendacho roho,ula nyama mbichi.

Sawa lakini kuacha shimo la choo na kutoka nje! Huyu hakukusudia kama
wale wa ulaya kwa sababu badae alishtuka na kurudi chooni mbio!
 
Dah, Umenikumbusa Bungu, Lualuke, Ndundu, Ikwilili na Somanga Uko ni Bendera za Yanga tu.
 
Back
Top Bottom