SoC02 Usanidi wa programu ya lugha ya Kiswahili

Stories of Change - 2022 Competition

sue bae

Member
Aug 16, 2022
21
13
Habari wana Jamii Forum.

Naitwa Suzana, fani yangu ni uandishi wa habari mbali na hilo, ni mtunzi wa kazi za fasihi na zisizo za kifasihi. Moja kati ya changamoto zinazonikumba ni suala la kupata wahariri wazuri wa kuhariri kazi zangu kabla ya kuzisambaza kwa watumiaji.

Wataalamu wa kazi ya uhariri wengi wana gharama kiasi kwamba natumia wahariri wasiokuwa na taaluma hiyo (watu wangu wa karibu), hivyo kusababisha kazi kuwa chini ya ubora.

Kiswahili ni lugha inayokua kwa kasi sana ulimwenguni, licha ya mataifa mengine kutaka kujifunza lugha hiyo lakini pia kama waswahili tunapaswa kujifunza lugha yetu kwani si kila mswahili hutumia kiswahili ipasavyo hasa kwenye uandishi.

Waandishi wengi, (ikiwemo nami) hukumbwa na changamoto nyingi kama gharama za uhariri wa kazi zao, kuchelewa kuchapisha kazi zao, kazi kuhaririwa vibaya na kazi kuhaririwa na wasiokuwa wataalamu katika fani hiyo.

Hivyo, kutokana na changamoto hizo, usanidi wa programu ya lugha ya kiswahili itasaidia waandishi wengi kuhariri kazi zao wao wenyewe na kutatua changamoto kama sarufi, msamiati, ufafanuzi, muhtasari, matamshi, alama za uandishi, kuepuka wizi wa kazi za waandishi wengine na kadha wa kadha.

Programu hii ita ainisha maneno yote yenye changamoto na kuya pigia mstari.

Haitawasaidia tu waswahili bali pia watu wote ulimwenguni wataweza kuandika makala zao na hadithi zao kwa kujiamini.

CHANGAMOTO ZITAKAZO TATULIWA NA PROGRAMU HII NI;

E6881959-47A0-46BE-A123-8A8F1D8839AC.jpeg

Picha na Freepik

Sarufi.
Hizi ni kanuni na sheria zinazopaswa kufuatwa katika uandishi na utamkaji wa lugha husika. Kila lugha ina sheria na taratibu zake, hivyo kiswahili pia kina sheria zake. Si wote wazijuazo sheria hizo, hivyo programu hii itasaidia waandishi kurekebisha maandiko yao kulingana na sheria na kanuni za lugha ya kiswahili. Kama vile, Upatanisho wa kisarufi. Mfano, Mama ana kula na sio Mama wana kula.

Msamiati.
Haya ni maneno yanayotumika katika lugha fulani. Programu hii itasaidia waandishi kurekebisha maandiko yao endapo maneno watakayo tumia sio ya kiswahili fasaha, pia, itapendekeza maneno ya kutumika kama mbadala. Mfano, Chuki na sio Chuka.

Ufafanuzi kwa kutumia maneno mbadala.
Programu hii itasaidia waandishi kupata maneno ya ufafanuzi zaidi ya yale waliyokwisha kuyatumia. Mwandishi akishaweka andiko lake kwenye programu, programu itapendekeza andiko lingine lenye maana ile ile likiwa lenye kuvutia zaidi ya lile la awali pasi na kubadili mantiki. Mfano, Anna alifariki kwa ajali ya gari na sio Ajali ya gari ilimuua Anna akafariki.

Kufupisha maneno.
Programu hii itasaidia waandishi kuwasilisha jumbe zao kwa kutumia maneno machache yenye kueleweka zaidi. Kuandika maneno mengi sio kueleweka hivyo itawasaidia kuainisha mambo ya msingi tu na kuacha yale yasiyo na umuhimu wa kuwepo kwenye andiko. Mfano, Kesho nitakula, kunywa na kusaza na sio Kesho nita kula, kesho nita kunywa na kesho nitasaza.

Wizi wa maandiko ya waandishi wengine.
Programu hii itasaidia waandishi kujua maandiko yao kama yana fanana na ya waandishi wengine ili kubadilisha namna ya uwasilishaji, lengo kuepuka kesi za mtandaoni na kufuata sheria ya mtandao ipasavyo. Mfano, Andiko hili lilichapishwa na Suzana Otaigo Mwaka 2018.

Matamshi na uandishi wa neno.
Programu hii itasaidia waandishi kwenye suala zima la fonolojia. Elimu kuhusu utamkwaji wa maneno. Programu itasahihisha maandiko yote yaliyoandikwa kulingana na matamshi na wala si uandikwaji wake kwani, kuna baadhi ya maneno utamkwaji wake ni tofauti na uandikwaji wake. Mfano, Watu hutamka heri lakini kiuandishi ni kheri.

Alama za uandishi.
Programu hii itasaidia kusahihisha makosa yote yatokanayo na kutozingatia alama za uandishi kama vile koma, nukta, nukta pacha, mabano, n.k mfano, Baba Anna, Anna ana lia. na sio Baba Anna Anna ana lia.

Kumalizia neno kabla halijamalizwa kuandikwa.
Programu hii itasaidia kumalizia maneno na sentensi ili mwandishi aweze kuchagua haraka maneno yampasayo kuweka. Hii itasaidia kuandika kwa haraka na kukumbuka maneno kama atakuwa amesahau. Mfano, Njoo uchukue ki…. (kiatu), (kitambaa), (kigoda), (kiti) n.k

Tafsiri ya maneno.
Programu hii itasaidia kutoa tafsiri ya maneno aliyotumia mwandishi ili kumsaidia kujua maana halisi ya neno kimantiki na kimuktadha kabla hajalitumia. Mfano, faragha (mahali pa siri, isiyojulikana, iliyofichwa)

Visawe.
Programu hii itasaidia kutoa msamiati/ maneno mbadala ili mwandishi achague neno litakalo mfaa zaidi. Mfano, Chutama na sio Chuchumaa.

Uchanganuzi.
Programu hii itasaidia kufanya uchunguzi wa maneno yanayotumika sana kwenye mitandao ili kumsaidia mwandishi kutumia maneno hayo. Hili litasaidia kazi zao kusambaa zaidi na kuwafikia watu wengi. Mfano, siri hutumika sana kuliko faragha.


MATOKEO YA PROGRAMU HII NI;

EF02605F-CD8D-4D19-977C-10B40C3CDBC9.jpeg

Picha na Freepik

  1. Uwepo wa machapisho mengi kwa lugha ya kiswahili mtandaoni. Programu hii itaamsha watu wengi wenye vipaji vya uandishi kuchapisha kazi zao kwa kujiamini.
  2. Wageni wataandika kwa lugha ya kiswahili kwa kujiamini. Watu wa mataifa mengine pia watapata fursa ya kuchapisha maandiko yao kwa kujiamini hata kama si wazungumzaji asilia wa lugha ya kiswahili.
  3. Kuepuka gharama za uhariri. Wahariri wenye taaluma hiyo ni wachache sana nao hufanya kazi hiyo kwa gharama, hivyo waandishi wengi kuchelewa kutoa kazi zao sababu ya kukosa fedha za kuwalipa. Programu hii itasaidia waandishi kuepukana na gharama hizo sababu itahariri kazi zao kwa usahihi zaidi.
  4. Kujifunza lugha ya kiswahili. Programu hii itawasaidia watu wote, waswahili na wasio waswahili kujifunza zaidi lugha hii. Kuanzia kujua miundo ya sentensi, matumizi ya maneno, sarufi, matamshi na kila kitu. Itakuwa mwalimu wa kuwafundisha watu lugha ya kiswahili.
  5. Kutunza muda. Programu hii itasaidia kutunza muda na waandishi kupata muda wa ziada kufanya mambo mengine ya maendeleo. Wahariri hutumia muda mwingi kuhariri kazi za waandishi na kusababisha uzalishaji kuwa chini, lakini programu hii itamsaidia mwandishi kutumia muda mchache katika kuhariri kazi zake.


Ili kuipata programu hii, Mtumiaji atapaswa kuwa na kifaa kilicho unganishwa na intaneti, kama vile simu janja, kompyuta, n.k

Mchakato wake, Wapatikane wataalamu wa kuweza kusanidi programu hii pia Wapatikane wataalamu wa lugha ya kiswahili kwa ajili ya kuweka maneno katika programu hiyo.


HITIMISHO
Wahariri tunawahitaji lakini pia tunapaswa kula tunda hili. Hili ni zao zuri litokanalo na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia. Zao hili litarahisisha maisha ya watu wengi na kukitukuza kiswahili ulimwenguni.

Tofauti kati ya programu na mwanadamu ni kwamba, binadamu huchoka, na akili ikishachoka ubunifu na ufanyaji kazi hupungua. Programu hii itasaidia waandishi kufanya kazi zao hata kama umakini wao utakuwa umepungua.

Ahsante.
 

Attachments

  • 0FD94A0A-BFE3-4254-9ECD-F0734C1735FA.jpeg
    8.8 MB · Views: 13
Habari yako ndugu

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
Asante sana. Nakarbia
 
Back
Top Bottom