Charliemic
JF-Expert Member
- Feb 17, 2019
- 604
- 979
Hakika usaliti katika mapenzi ni jambo linaloumiza mno, linaacha majeraha makubwa mno ndani ya mioyo ya watu. Na hakuna kinachouma kama kutendwa. Na lina athari kubwa saana katika mahusiano ya mbeleni kwa wote yaani msaliti na msalitiwa! Asikuambie mtu hata kama una mpnz bora saana ila awali ni awali tu wengi hubaki na picha za x wao akilini! Ndio maana ni rahisi kwa walioachana kukumbushia enzi au kupasha kiporo.